Fisi aliyeuliwa amekutwa na chapa ya jina kwenye paja lake

Fisi aliyeuliwa amekutwa na chapa ya jina kwenye paja lake

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwamigagani, Kata ya Mwalushu, amewataka wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa wahusika wa uhifadhi haraka iwezekanavyo ili kuepuka hatua kali za kisheria.
Huko Waganga wamejaa wengi sana
 
Itirima huko waganga ni wengi kuliko wakazi wa kawaida .hapo usikute kuna tatizo la kiufundi limetokea
 
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
View attachment 3244143
Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori kwa kushirikiana na TANAPA na Jeshi la Polisi wamefanikiwa kumuua fisi mmoja katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, baada ya kuingia katika makazi ya wananchi. Cha kushangaza, fisi huyo alikutwa na maandishi kwenye paja lake la kushoto, yakisomeka MALLA N 7, ingawa maana yake haijafahamika.

Operesheni hiyo maalumu imeanzishwa kufuatia matukio ya fisi kushambulia watoto nyakati za usiku, ambapo baadhi yao wamepoteza maisha. Fisi huyo aliuliwa katika kijiji cha Kimali, Kata ya Nyamalapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti wanyama hao hatari.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwamigagani, Kata ya Mwalushu, amewataka wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa wahusika wa uhifadhi haraka iwezekanavyo ili kuepuka hatua kali za kisheria.

Tangu operesheni hiyo ianze, jumla ya fisi 16 wamekwisha kuuawa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Itilima na kikosi kazi cha askari wa TAWA, TANAPA na Jeshi la Polisi.
Da!!!,,,hatari sana,,,alaf utasikia m2 anasema hakuna uchawi...
 
Kwani fish hafugiki unaweza mfuga tu

Ova
 
Back
Top Bottom