FISTULA inatibika na kupona kabisa bila gharama/bure!

FISTULA inatibika na kupona kabisa bila gharama/bure!

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kuna hili tatizo linalopata wanawake wakati wa kujifungua hasa wale waliopata Uzazi pingamizi na kuwafanya washindwe kuzuia haja (kubwa na ndogo).

Tatizo hilo linatibika na Kupona kabisa na huduma hii kwa sasa inatolewa bure kabisa. Kama mgojwa yupo kijijini na akawa hana nauli ya kwenda kwenye hospitali kubwa, atasaidiwa nauli (gharama za usafiri pamoja na matibabu).

Wajulishe na wengine na kama unafaham mwanamke mwenye changamoto hii anaweza kupiga namba zifuatazo kupata msaada wa maelekezo ya kupata matibabu.

0800752227 au 0765770770 na kufuata maelekezo. ukikwama unaweza dm kwa msaada zaidi....
WAJULISHE NA WENGINE!

Tafadhali usipige namba hizo kama huhusiki na hiyo changamoto kwani lengo ni kusaidia wagonjwa!!!
 
Back
Top Bottom