Fitness and wellness


Daah braza pole sana aisee!
Mungu akutie nguvu uwe kamili gado.
 
squarts zinasaidia nn mkuu??
Mkuu hiyo Unakua na deadly kick miguu inakua na na nguvu na ukifikia kupiga hadi 500 unaona kabisa juu ya paja panavyojazia Warning for the first siyo easy unaweza kunya umesimama kwa wiki nzima then utaskia kawaida tuu baadaye inajaza paja na kua lenye nguvu.
 
Nimeanza zoezi ila nakumbana na changamoto zifuatazo mfano nikitaka kupiga "push up" mikono inatetemeka sana au nikisema nibebe chuma mikono inatetemeka sanaa hii ni nn wakuu au ndio kuto kuzoea!?
 
Ni kwamba misuli yako bado haijazoea hizo shurba.

Kwa hiyo wala usishituke sana. Ni hali ya kawaida kabisa.

Mimi mwenyewe nimeanza tena mazoezi mwezi uliopita baada ya kuwa kwenye hiatus kwa miezi miwili na siku mbili tatu za mwanzo mikono ilikuwa inatetemeka sana na sikuwa na nguvu kivile.

Lakini kwa vile nimekuwa nikifanya mazoezi haya ya resistance training kwa zaidi ya nusu ya maisha yangu, tayari nina muscle memory nzuri inayonifanya nirudi kwenye shape ndani ya muda mfupi sana.

Ukiwa na muscle memory nzuri basi hata retraining nayo inakuwa rahisi mno na gains zinaonekana ndani ya wiki chache tu.

Sasa kinachotokea kwako ni kwamba misuli yako bado haijawa na nguvu [ strength] wala ustahimilivu [endurance] wa kutosha.

Kwa hiyo nenda mdogo mdogo na taratibu utaona tofauti inakuja...nguvu zitaongezeka na ustahimilivu nao utaongezeka.

La nyongeza, pia zingatia sana form unapopiga hizo push ups na kunyanyua hivyo vyuma.

Form ni muhimu sana. Jingine la muhimu ni range of motion.

Kwa hiyo usibebe tu ili mradi umebeba. Beba kwa mpangilio maalumu.

Ni matumaini yangu haya maelezo yatakusaidia.

Ukihitaji ufafanuzi zaidi usisite kusema.

Kila la kheri.


Nimeanza zoezi ila nakumbana na changamoto zifuatazo mfano nikitaka kupiga "push up" mikono inatetemeka sana au nikisema nibebe chuma mikono inatetemeka sanaa hii ni nn wakuu au ndio kuto kuzoea!?
 
pamoja sana mkuu
 

Shukrani mkuu!
 
Uko sahihi dawg
 
kuna anayefanya contact/collision sports kama martial arts? Je unafanya mara ngapi kwa wiki? Na unafanya na mazoezi gani ya ziada?
 
Nina kilo 70 nimeanza diet, target nifike 65 ila dooh mazoez nashindwa kabisa nilifanya mara moja cku ya pili nikaamka mgonjwa kabisa. Huu uzi utakua msaada kwangu sana kwa kipindi hiki.
 
Nina kilo 70 nimeanza diet, target nifike 65 ila dooh mazoez nashindwa kabisa nilifanya mara moja cku ya pili nikaamka mgonjwa kabisa. Huu uzi utakua msaada kwangu sana kwa kipindi hiki.
unataka kupunguza uzito au mafuta (weight or fats) what is your target? ama vyote?
 
Wakuu nataka kidogo niutengeneze mwili wangu uwe mkubwa na uliojengeka kimisuli, Nataka kufahamu vitu vya kimsingi ili nifanikishe hili...
 
Wakuu, salaam.

Hivi ni kweli wanawake wakimaintain figure, kuna baadhi ya viungo vya mwili huwa vinagoma kupungua ukubwa na matokea yake huongezeka zaidi ya mara mbili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…