MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Nikisoma thread za watu kufanya mazoezi napata uchungu sana. Nilikuwa mtu wa mazoezi, nafanya jogging mara tatu kwa wiki, nacheza basketball mara tatu kwa wiki. Nilikuwa napiga push ups 400 kila asubuhi at least mara tatu kwa wiki. Kwa kifupi nilikuwa fit sana (sio kujazia mamisuli). Ila mchana mmoja ulibadili maisha yangu, minor accident ikanipa serious backbone damage.
Kutoka a very fit guy mpaka kuwa mtu ambae hawezi kutembea mita hamsini bila kukaa chini ni experience ngumu sana. Nashukuru Mungu nimepona kiasi kwamba naweza kufanya vitu vyote kasoro kufanya mazoezi niliyozoea kufanya. Na kwa uwezo wa Mungu natumaini siku moja nitarudi kama zamani.
Daah braza pole sana aisee!
Mungu akutie nguvu uwe kamili gado.