Flora Mbasha kufunga ndoa wiki ijayo

Flora Mbasha kufunga ndoa wiki ijayo

Mathayo 19:9
[9]Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Kwa hiyo Mbasha alimuacha mkewe kwa uasherati kwa hiyo akioa mke mwingine si kwamba anazini. Na bibi kaachwa kwa uasheratiii 😀😀😀
 
Kwani jina la Mbasha ni lake? Nadhani atengeneze tena brand mpya na aachane na hiyo brand ya Mbasha!

Zaidi nikuuharibu ukristo na jamii yake, nitashangaa atakayenunua album au mchungaji atakayemualika kutumbuiza kwa lengo la kumsifu Mwenyezi MUNGU.
 
Kibiblia huyo Daudi, haitajiwi kumwoa flora, mpaka mbasha Mungu amchukue!!

Imeandikwa wanandoa wasiachane isipokuwa Kwa habari ya uasherati , maana Yake ikithibitika kuwa mmoja wa wanandoa amefanya uasherati /zinaa kuachana ruksa! Naomba yasomeni Yale maandiko Kwa utulivu kisha muombe Roho awasaidie kuyaelewa ! Na Kulikuwa na tuhuma za mumewe kumbaka shemejie kitu ambacho kinashabiliana na maswala ya zinaa na uasherati Kama maandiko yalivyosema.
 
Amrudishie jina mbasha kwa mume wa zamani.

Ndo maana wadada wa Siku hizi hawataki Kabisa kubalisha majina kuanza kutumia ya wanaume zao kuepuka Kama hayo ya Frola Mbasha, ukitumia jina la Mume akikuzingua kiasi cha kuachana Kama hao huwa inaboa sana, hata Kama anasema Siku hizi tumuite
Madam Flora lakini Watu bado watakuwa wakimwita Flora Mbasha coz ndilo lililozoeleka miongoni mwa Watu . Bora kumuezi baba yako kuliko mwanaume!
 
Hebu someni maandiko vizuri najua alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe isipokua kifo au uzinzi so ukithibitisha mwezako anachepuka talaka tu ingawa Mungu haipendi kwakua hapendi kuachana.
Yap,yap, uko sawa kabisa. Uzinzi ukithibitika ndoa huvunjwa.
 
Mbasha nae inabidi aoe faster ili iwe ngoma droo!! Akimwaga mboga unamwaga makandee!!
 
Talaka kibiblia imeruhusiwa under some conditions Matharan hiyo ya uasherati , Mimi nimekuwa nikiwahoji wachungaji /Askofu Kwa nini huwa mnaweka vikwazo ktk Watu kuachana? Wakati maandiko yameeleza wazi Kabisa vigezo na masharti lakini nyie hata vikiwa dhahiri hamtaki? Wengine wakaniambia ooh unajua sisi tunasimamia kwenye neno la " kusameheana" kwamba tunapenda wasameheane, sasa mfano mwanaume ambae ni mzinifu/ mwasherati na ndiyo life style Yake vimada anazaa nao na kuwajengea nyumba Magari na imethibitika pasipo Shaka na hata jamii na ndugu zako wanajua hivyo, halafu eti uendelee kuvumilia maudhi ya namna hiyo maisha yako yote, stress maisha yako yote Kwa nini?,
 
Usikute ndo Daudi Bashite.... Sipati picha povu LA Gwajima lingekuaje...
 
Nawapenda wazungu akikwambia napenda inatoka Moyoni siyo sisi ndo maana mmoja akiasi na ikathibitika hivyo wanamwagana maisha yanaendelea
 
Kwamba mwanaume hana uwezo wa kuamua kama aendelee na ndoa au la? Umedanganya.
Mwanaume hana uwezo,mwanamke ndo anaemaua,binafsi mme wangu hawezi kuaniacha kamwe,labda mimi ndo nimuache.
 
Back
Top Bottom