Talaka kibiblia imeruhusiwa under some conditions Matharan hiyo ya uasherati , Mimi nimekuwa nikiwahoji wachungaji /Askofu Kwa nini huwa mnaweka vikwazo ktk Watu kuachana? Wakati maandiko yameeleza wazi Kabisa vigezo na masharti lakini nyie hata vikiwa dhahiri hamtaki? Wengine wakaniambia ooh unajua sisi tunasimamia kwenye neno la " kusameheana" kwamba tunapenda wasameheane, sasa mfano mwanaume ambae ni mzinifu/ mwasherati na ndiyo life style Yake vimada anazaa nao na kuwajengea nyumba Magari na imethibitika pasipo Shaka na hata jamii na ndugu zako wanajua hivyo, halafu eti uendelee kuvumilia maudhi ya namna hiyo maisha yako yote, stress maisha yako yote Kwa nini?,