Florent Ibenge amvuta kocha wa Tabora United, aliyewafunga Yanga na kumpa jukumu

Florent Ibenge amvuta kocha wa Tabora United, aliyewafunga Yanga na kumpa jukumu

Tabora alimfunga yanga kutokana na kukosa wachezaji wake wengi eneo la defense, wangekuwa full mkoko Tabora angepigwa kama ngoma
sasa kama shida ilikuwa ni mabeki, kwanini washambuliaji hawakufunga matano, na wao kufungwa hayo matatu.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Vita yetu ni dhidi ya Kolo tukimfunga yeye tu inatosha [emoji16]
 
Wakati zikisalia saa chache kabla ya Yanga kushuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kupambana na Al Hilal ya Sudan, kocha wa Waarabu hao Florent Ibenge amemvuta mjini kocha mmoja aliyewatibulia wenyeji wake.

Ibenge amemuita jijini Dar es Salaam haraka kocha Anicet Kiazmak ambaye ni kocha wa Tabora United iliyoichapa Yanga wiki chache zilizopita kwenye mchezo wa Ligi.

Ibenge alifanya kazi na Kiazmak pamoja wakiwa Al Hilal ambapo taarifa ambazo Mwananchi imezipata ni kwamba kocha huyo anatakiwa kuja kufanya uchambuzi wa mwisho wa kiufundi kuelekea mchezo wa timu hizo mbili utakaoanza saa 10:00 jioni.

Tayari Kiazmak ameshatua jijiji Dar es Salaam asubuhi hii kwa treni akitokea Tabora akipitia Dodoma tayari kwa kikao hicho na bosi wake wa zamani.

Ibenge anamuamini Kiazmak kwenye eneo la kuwachambua wapinzani ambapo Wakongomani hao wawili watajifungia kwa lengo moja la kuwatafutia dawa wenyeji.

Na imetiki
 
Kwa ukweli kabisa hizi game hata angekuwepo kipara angepigwa tena , watu wameshausoma uchezaji wao na wakaja na solution tu basi
 
Back
Top Bottom