Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nikitembea katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengi ya Tanzania jambo kuu linalonijia kichwani ni kwamba, Tanzania tutapata maendeleo ya kweli pale tu tutakapopata Viongozi wenye akili na wasioendekeza rushwa.
Haiingii akilini kwa upana wa kujenga barabara uliopo kati ya Gongo la Mboto hadi Posta ila bado viongozi wetu wanajenga barabara za njia mbili kila upande kwenye mradi unaendelea.
Ujinga huo huo umefanyika kilwa road hadi posta na unafanyika tena barabara ya Tegeta hadi Posta.
Haingii akilini pia kwa upana uliopo kuanzia Mwenge hadi Bandarini kupitia ubungo bado viongozi wetu wanajenga barabara zenye upana wa njia mbili kila upande.
Foleni inayolalamikiwa katika Jiji la Dar es Salaam sio jambo lililoshindikana kupatiwa ufumbuzi bali ni ujinga na uvivu wa kufikiri wa Viongozi wetu ndio unaosababisha haya.
Pia Rushwa ni chanzo kingine knachosababisha tuwe na miradi ya kurudia rudia maana viongozi wetu wanadhani wakijenga barabara za uhakika za njia 3 au nnne kila upande watakosa sehemu za kutengeneza miradi ya kupiga pesa.
Naionea huruma sana Tanzania.
Kuchelewa kwetu kupata maendeleo ya kweli na uhakika kunatokana na kukosa viongozi wa kweli wenye akili na wanaofikiri vizuri kwa maslahi mapana ya nchi.