Foleni usiku huu Morogoro Road Ubungo - Kimara

Foleni usiku huu Morogoro Road Ubungo - Kimara

Generetaion Z

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2022
Posts
343
Reaction score
874
Hii foleni sijawahi ishuhidia kabisa, kama upo mjini sasa hivi na unampango wa kwenda Mbezi au Kimara basi endelea kuagiza bia maana hutoboi.

Au kama uko vyema chukuwa boda boda au kama umenasa katika foleni shuka tu tafuta namna nyingine, kamba imeanzia Kimara stendi hadi Ubungo mataa na haisogei hata kidogo.

Panda mwendokasi angalau, ila kama unagari binafsi au daladala hutoboi, Mbezi utaiona saa kumi asubuhi!
 
Hii foleni sijawah ishuhidia kabisa kama upo mjini saiv na unampango wa kwenda mbezi au kimara basi endelea kuagiza bia maana hutoboi

Au kama uko vyema chukuwa boda boda au kama umenasa katk foleni shuka tu tafuta namna ingine kamba imeanzia kimara stendi hadi ubungo mataa na haisogei hata kidogo

Panda mwendokasi angalau ila kama unagari binafsi au daladala utoboi mbezi utaiona saa kumi asubuhi
Kwa tunaoijua hiyo Njia hii nayo ni Taarifa / Habari Kwetu ya Kutuambia mpaka tushtuke au tuogope kama utakavyo?
 
Shida nini ?
Kuna ajali sehemu au?
 
Afadhali umesema. Ngoja niagize Tena after all ni wknd
 
Tanroad pia wangalie uwezekano wa kutoa lile bams pale kimara. Kuna kona kali then mbele kuna bams lazima magari yakifika eneo lile yapunguze mwendo then inaperekea foleni. Hao watu wa Barabara sjui haliobni hili tatizo?
 
Mwendokasi itapunguza na kuondoa kabisa foleni, pumbavu kweli hawa Jamaa, Sijui huwa wanatuonaje
 
Back
Top Bottom