Foleni ya Tabata - Tazara imeanza kuwa tishio kwa uchumi wa nchi, nini kifanyike?

80% ya jiji ni squatter barabara kubwa ziko chache sana
 
Kwa hiyo mzee kila huduma muhimu ya kijamii ipelekwe nje ya mji mbali na makazi ya watu walipo?

Faida yake msongamano utapungua, athari yake je! ni ipi? Aisee si rahisi kama unavyodhani, ukitafuta picha ya kariakoo enzi hizo haikua na mafuriko ya watu kama unayoyaona sasa, mambo hubadilika kadiri miji inavyokua. Muhimu ifanyike study ya uhakika ili kuja na solutions za uhakika kulingana na hali na mazingira yetu na sio kusema nchi flan wanafanya hivi au vile wamefanikiwa halafu unasahau utamaduni, desturi na mazingira ya kiuchumi tunatofautiana.
 
Malori yale sijui ,yaani kutoka mwananchi mpaka Tazara ni kero sana.Nchi inaingia hasara kwa maeneo yale tuu
Yaani muda mwingine foleni inaaniza external hadi uhasibu, hii nchi hii, wajenge flyover juu ya Tazara flyover , masaa matatu mtu hujavuka hata Tazara!!??
 
Kuondoa biashara barabarani itakuwa na matokeo chanya kwa Sana!! Ila hawa Tanroad Kama hayana msaada kabisa
 
Halafu vituo vya mafuta vife? Mafundi magari na wauza vipuli warudi mtaani na car wash zote zifungwe.
 
Napendekeza wajenge flyover juu ya Tazara flyover ili zinazotokea Buguruni kwenda bandarini nazo zipite juu. Nakaribisha maoni
NAUNGA MKONO, ijengwe fly over nyingine juu ya TAZARA, kwa upande wa Tabata serikali wakati wa mwenda zake ilikuwa imeahidi kujenga flyover pale, sijui kama bibi mkubwa kapotezea au la
 
NAUNGA MKONO, ijengwe fly over nyingine juu ya TAZARA, kwa upande wa Tabata serikali wakati wa mwenda zake ilikuwa imeahidi kujenga flyover pale, sijui kama bibi mkubwa kapotezea au la
Tatizo pesa yote inaenda kwenye chanjo, ile sehemu imefikia critical level, ijengwe kama walivyofanya ubungo
 
Hali ni mbaya sana muda huu, malorry ni mengi mno, foleni ni kali, uchumi utakua vipi kwa style hii?!
 
Hali ni tete, je, serikali inampango wowote wa kutatua janga hili hapo Tazara?, kama upo, ni upi? Na kama haupo, watupe sababu ni kwanini tuendelee kuwaacha madarakani?!
 
Napendekeza wajenge flyover juu ya Tazara flyover ili zinazotokea Buguruni kwenda bandarini nazo zipite juu. Nakaribisha maoni

Foleni haitokei Tazara ile foleni ni ya buguri pale junction ya manyanya na kwenda ilala
 
Napendekeza wajenge flyover juu ya Tazara flyover ili zinazotokea Buguruni kwenda bandarini nazo zipite juu. Nakaribisha maoni
Foleni ktk eneo tajwa kwa kiasi kikubwa lina chochewa na malori mengi yatokayo na yaingiayo bandarini ....binafsi nikiona vile ni indicator ya kuwa bandari yetu ina piga kazi kwa maana wateja wana ikubali

Lkn pia solution ni ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na ujenzi wa bandari kavu kule mkoa wa pwani kwa kiasi zitapunguza huu msururu wa malori...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…