Njia rahisi ya kupunguza foleni kwenye majiji, ingawa itaumiza wengine, ni kuwepo na kodi au tozo ya kila mwezi kwa magari yote binafsi yasiotoa huduma kwa umma, pamoja na kuongeza tozo maeneo ya kupaki hayo magari; Mfano, kama utatumia usafiri binafsi ndani ya jiji na ukawa unatozwa shilingi milioni 1 kwa mwezi, na sehemu yoyote utakayopaki au kusimama kutozwa kodi...hapo lazima magari mengi binafsi yatabaki majumbani, na hapo utakuwa umepunguza foleni kwa asilimia kubwa...kwa sababu kwenda katika shughuli zetu tutatumia usafiri wa umma.