Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Huwa najiuliza watu wanaokuwa kwenye mamlaka wanaotoa maoni ya ajabu ajabu wanatokea wapi, kumbe wengine mpo hapa JF.Njia rahisi ya kupunguza foleni kwenye majiji, ingawa itaumiza wengine, ni kuwepo na kodi au tozo ya kila mwezi kwa magari yote binafsi yasiotoa huduma kwa umma, pamoja na kuongeza tozo maeneo ya kupaki hayo magari; Mfano, kama utatumia usafiri binafsi ndani ya jiji na ukawa unatozwa shilingi milioni 1 kwa mwezi, na sehemu yoyote utakayopaki au kusimama kutozwa kodi...hapo lazima magari mengi binafsi yatabaki majumbani, na hapo utakuwa umepunguza foleni kwa asilimia kubwa...kwa sababu kwenda katika shughuli zetu tutatumia usafiri wa umma.
Hivi ndugu kwanza nikuulize tu, huwa unasali?! Maana kwa namna umeongea sidhani kama hata MUNGU unamtambua. Umetumia fikra za ubinafsi wa hali ya juu. Hivi unadhani watu wanapenda kuja mjini na magari ili kujaza foleni?!
Hivi umewazia watu wanaoishi huko kimanzichana, chanika, kibaha, kivule, kitunda, kinyerezi, kifuru, malamba mawili, kibamba, goba, umeshaona idadi ya watu wanaoishi hayo maeneo kwa wingi wao....?!
Hivi unadhani hawa watu wote wanapenda shida kama wewe, yaani tuishi kwa shida kwasababu tunaogopa maendeleo?!
Wewe na ndugulile Mnaweza kuwa mnatokea ukoo m'moja, maana na yeye ana mawazo kama yako, watu wanapofikiria maendeleo na kuongezeka yeye kwake anaona ni tatizo, heri watu wateseke na kupata shida kuliko kubadilisha utaratibu wa maisha.