Kataa ndoa ni uchaguzi wa vijana wa kisasa ulioibuka sababu ya kukosekana wazee waliodhibiti maadili ya vijana wanaopevuka.
Jamii imekuwa huru kupitiliza, vijana wana uhuru wa kujiongoza bila kujali, hakuna tena kuwajibika kwa wazee wa ukoo wala watu waliowazidi umri, ukishamaliza shule unaamua wewe atakalo na hakuna mtu anayeweza kukufanya uhoji tafsiri ya maamuzi yako.
Kama ni binti ukiamua uishi kwa mwanaume ni sawa tu hata kama mwanaume hajulikani. Lile Swali linalozua hofu tulilokuwa tukijiuliza kuwa "itakuwaje wazee wakijua" halipo tena matokeo yake kukaibuka mabinti wasioitunza miili yao na vijana wasiojali familia.
Wanawake wanaothamini ndoa wapo Ila wengi ni WASHAMBA, hawana muonekano wa ukisasa, hawajui social media, bata na hawana ujanja wa wanawake wengi ambao vijana huwataka, si wanamke ambao kijana utajivunia kuwa una pisi kali, misimamo na woga wao wa ngono na kuishi kwa mwanaume huwafanya wasiwe options za vijana wengi, wale wachache wanaojua kuspot mke chap huwaoa hawa na maisha huwa yanaenda sawa tu.
Ni kweli, ila na vijana nao wamekuwa dhaifu. Hawajui kuchagua mke na mama wa watoto, wengi wanawakimbilia mabinti wajanja wajanja wenye vidigrii halafu wanafanya kosa moja kubwa mno kuoa huku kipato hakitoshi na hapo hapo binti ana ajira na malengo ambayo ni expensive plus na ni Pisi kali.
Wanawake wa 70's na 80's kidogo hili halikuwa tatizo. Hapa 90's kuendelea ni tatizo.
NAUNGA MKONO HOJA. Na naongeza, majukumu yako ni yako usimpe mwanamke ayafanye.
NAUNGA MKONO HOJA.
Hapa nakupinga, Mwanaume anamuhitaji mwanamke tena pengine kuliko hata mwanamke anavyomuhitaji mwanaume. Mwanamke anaweza kuachwa mjane na asiolewe na akaishi bila shida ila si sisi wanaume, utatafuta tu mke. Esp ukiwa kwenye 50's na kuendelea. Mwanamke anaweza kaa bila mume na watoto ila ni vigumu sana mwanaume kukaa bila mwanamke.
Hii ni kwasababu ya jukumu la mwanaume katika jamii. Lazima iulizwe iwapo ameacha watoto sababu wanabeba jina lake na yeye alipaswa kuwa mlinzi wa hao watoto na kwasababu hayupo basi ni lazima ndugu na marafiki wachukue hilo jukumu. Tatizo ni kuwa kwa jamii ya sasa vijana wanazaa na wala hawawalindi watoto wao, hawajali na mara nyingine hawawatambulishi kwa wazee wao wa ukoo kuwa hii ni damu yetu.
NDOA NI ZAWADI KWA MWANAUME SABABU MKEO ANAKUZALIA WATOTO WENYE JINA LAKO, ANAWALEA NA KUWAKUZA KWA HESHIMA YAKO, ANAKUHUDUMIA MAHITAJI YAKO YA KIMWILI NA KIJAMII NA ZAIDI YA YOTE ANAKUOMBEA KWA MUNGU ABARIKI KAZI YA MIKONO YAKO ILI UWEZE KUWATUNZA NA KUWALINDA IKIWA NI SEHEMU YA JUKUMU LAKO SABABU UMEUMBWA MWANAUME.