For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?

For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, ni keshokutwa tuu, siku ya Jumatano ijayo, kwa mazingira ya the political dynamics za siasa za nchi yetu, hali halisi ya uwanja wetu wa siasa ulivyo, katiba yetu ilivyo, sheria yetu ya uchaguzi ilivyo, Tume yetu ya uchaguzi ilivyo, hali ya political awareness ya Watanzania in terms of political awakening, there is no way, upinzani anaweza kushinda urais wa nchi hii, hivyo tunaposema CCM itatawala milele, naomba mtuelewe.

Katika uchaguzi huu, kwa upande wa urais, ushindani mkali ni wagombea mawili tuu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli wa CCM na Tundu Antipasi Lissu wa Chadema.

Mimi Paskal Mayalla najisikia very proud kwasababu ni mmoja wa watu wa mwanzo, kumshauri Tundu Lissu agombee na rais Magufuli, kwasababu kuna sifa fulani ya Lissu anayo ambayo anamzidi Magufuli, Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Kutokana na sifa hiyo ambayo Lissu anamzidi Magufuli, ni kweli mikutano ya kampeni ya Tundu Lissu, ina hamasa kubwa na makundi makubwa ya watu, ambayo kisasa wanayaita nyomi, hali inayopelekea watu wajinga wajinga wasiojua siasa za kweli za nchi hii zinakwendaje, kudhani hayo makundi ya watu ndio kura hizo! hivyo kujiaminisha Tundu Lissu ndiye anakwenda kushinda urais!, masikini hawa, hawajui decisive votes kwa uchaguzi wa Tanzania, zinatoka wapi!.

Determinant ya kura za ushindi kwa uchaguzi wa Tanzania, ni kura za watu wa vijijini. Chama pekee kilichowafikia Watanzania wote hadi vijijini ni CCM pekee, hivyo ni CCM pekee ndio inakwenda kushinda.

Vyama vya upinzani ni maarufu maeneo ya mijini tuu, hizo nyomi za hayo makundi ya watu kwenye mikutano ya kampeni, sio kura hizo, kura zenyewe halisi ziko vijijini na huko ndiko CCM ilipo, hivyo kura zote za vijijini ni za CCM.

Ukiondoa hizo kura za vijijini ambazo tayari ziko kibindoni kwa CCM, na kama hii hoja ya TPSF hapo mbele ni kweli.

Then there is no way Upinzani unaweza kushinda uchaguzi huu, hivyo mshindi wa uchaguzi Mkuu huu ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli na CCM. Kwa vile there's no way Tundu Lissu anaweza kushinda uchaguzi huu, kuna mwana jf mwenzetu huyu Kishimbe wa Kishimbe , amatoa mawazo mazuri sana kwenye bandiko hili.
ameshauri

3) We can always have a clause, in our new constitution, which will make it a RIGHT for the first and second runner-ups of the presidential contest to be members of the parliament by merit and thus give no room for tyrants TO SHOW THEIR SYMPATHY!!!
Mkuu Kishimbe wa Kishimbe , kwanza asante kwa objectivity
3. Hoja yako ya tatu, ni hoja ya msingi sana, nakuunga mkono asilimia 100% chini ya 100%, tubadili katiba, tuweke clause, wagombea wote wa urais, watakao pata kura zaidi ya asilimia 10%, wawe wabunge wa taifa automatically.

Mimi kwenye bandiko langu hili,

nimemshauri rais Magufuli, kwa vile atashinda kwa kishindo, na ushindi wa kishindo wa Magufuli na CCM, na kufuatia good track record ya utendaji wake, na kukubalika kwake na CCM, upinzani utabwaga chini na kuragazwa sana, kiasi cha kupata Bunge la CCM tupu.

Kufuatia kipigo hicho cha upinzani kitaacha makovu ya maumivu kwa upinzani, then tunamuomba rais Magufuli, aingie huruma, atangaze kuwa ata wateua Lissu, Zitto, Mbowe, Lipumba na Mbatia, wawe wabunge wa kuteuliwa ili angalau wakalete msisimko Bunge la CCM.

Kutokana na Watanzania wenzetu wengi kuwa na too great expectations kuwa Tundu Lissu atashinda uchaguzi huu wakati sisi tunaojua the reality ya ushindi wa uchaguzi hautokani na kura tuu zilizopigwa, yaani the votes casted, but the votes counted!, hivyo the determinant of victory is not vote cast but vote count!.

Nalisema hili mapema ili kuwasaidia Watanzania wenzetu, kwa kuwaandaa kisaikolojia kwa kitakacho tokea, ili watakapo kutana na ukweli huu kwenye matokeo, wasije kuchanganyikiwa kwa stress na despair kwa kutoamini macho yao na masikio yao kwa kitakacho tokea, hivyo bandiko hili ni msaada mkubwa kwao, kuzuia panic na kupata pressure, na depression ya kushindwa kwasababu they knew before, na waliambiwa.

Kumpigia kura mtu ambaye hatashinda, ingawa hiyo nayo ndio kutumia haki yako ya kidemokrasia kuwachagua viongozi unaowataka, lakini in terms of utawala wa nchi, unakuwa umepoteza tuu bure kura yako!.

Sasa ili kuwasaidia Watanzania wenzetu wasipoteze bure kura zao, Jee mnaonaje tumshauri Rais Magufuli ambaye yeye ndiye mgombea wa chama cha ushindi, CCM, atoe a solid promise kwa Watanzania, kuwa atamteua Tundu Lissu kuwa Mbunge wa kuteuliwa, kwenye zile nafasi zake kumi za wabunge wa kuteuliwa, hivyo waliopanga kumpigia kura Tundu Lissu, wasiwe na wasiwasi, Tundu Lissu hata asiposhinda urais, bado atakuwa ni Mbunge wa kuteuliwa na kuwatumikia wananchi, hivyo natoa wito, badala ya kumpigia kura Tundu Lissu, hizo kura za Lissu, bora mumpigie Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kisha Magufuli atamteua Tundu Lissu kuwa Mbunge wa kuteuliwa, hivyo hapo unakuwa hujapoteza kura yako!.

Hii hoja ya wagombea wote wa urais watakaopata zaidi ya asilimia 10% ya kura za urais, kuingia Bungeni automatically, kutajenga sana a national unity.

Mnaonaje hili, la kura za Lissu apigiwe Magufuli?.

Paskali
 
Capture.JPG
 
Mkuu P
Bandiko lako lote limejikita kwenye Para ya 1 na ya 11... very objective and very fair. The Economist ya juzi waliandika kitu kinachofanana na hicho wakisema "President Magufuli likely to win unfair vote in Tanzania"

Tuseme ukweli nchi yetu na wazalendo wa nchi hii wafanye jambo. CCM ni chama kikubwa mno kutishiwa na vyama vya 90s ... hakukuwa na haja ya kutoifanya tume kuwa huru au too much use of state apparatus kuisaidia CCM uchaguzi ambao ni "obvious " inawaza shinda most of the time... CCM has all it takes kuanzia resources mpaka mifumo bila kuathiri credibility ya democracy...

Sasa huo uoga wa kutishia amani na Marsha ya watu na mabunduki na mabon CCM inatoa wapi?
Something wrong somewhere

Ubunge kwa mgombea urais mwenye possibility ya more than 30% of total voters ni dhihaka. May be awe makam wa kwanza wa rais au something similar... au awe guaranteed basdhi ya mambo kama ilivo kwa Executives wengine.
 
Nilichogundua watu wengi kipindi hichi cha kampeni wamekuwa wanafiki kwa Jiwe,lakini moyoni hawako nae kabisa na watampigia Lisu..kinachowafanya wawe hivyo ni kutokana na tabia ya Jiwe ilivyo Mzee Wa mavisasi,ikitokea akarudi tena madarakani atalipa visasi kwa wale hawakuwa upande wake.so ili kuwa in safe side sana fake upendo kwa Jiwe.
Mmoja wapo hiyo hapo.
 
Umetumia maneno meeeeengi kukwepa kuwaita CCM ni Waizi wa Kura. Ooooh votes casted not votes counted. Wiiiizi mtupu.

Umeelezea kuwa Kura zote za Vijijini ni za CCM. Una uhakika gani kwenye hili?? Wewe ni mkazi wa Huku vijijin?? Nakusihi usiishi kimazoea, Mwaka huu JPM ana upinzani mkubwa Vijijini na Mijini.
 
Back
Top Bottom