For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?

Mkuu post kubwa isiyo na ubongo. Sasa kama mmeshinda kihalali NATIONAL UNITY ni ya nini? Uzuri mnafiki huwa anajisema mwenyewe.
 
Hapana. Kunakuwa hakuna maana ya ushindani. Lissu arudi tu ubelgiji akaendelee na maisha yake.
 
kwan alipokuwa ulaya nchi ilimsubilia?? Tutasonga mbele bila yeye🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Wewe ni mtumwa na ni mtu usiejielewa. Yaani wewe unakaa unasapoti dhulma kufanyika, tena ukitambua kabisa dhulma inafanyika! Wewe sio mtu wa kuaminika kabisa ni rahisi sana kuwauza wenzako kwa vijikaratasi vilivyochorwa nambari.
 
Kaka Mkubwa! Awamu hii nimekubaliana na kauli ya kwamba CCM itatawala milele! Uchafu uliofanyika ni Siri yangu tu! Sisi Wana CCM hatuna cha kujivunia hapa,furaha yetu itakuwa machoni tu ila mioyo yetu imejaa huzuni.
Kwa heri upinzani,haki na furaha Tanzania.
 
Wanabodi,
..
Katika uchaguzi huu, kwa upande wa urais, ushindani mkali ni wagombea mawili tuu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli wa CCM na Tundu Antipacy Lissu wa Chadema.
...

Mnaonaje hili, la kura za Lissu apigiwe Magufuli?.

Paskali

Mkuu Paskali sikubaliani na wewe Lissu kuteuliwa na Rais awe mbunge, kwa sababu hafai kabisa hata ujumbe wa nyumba kumi. Kwa kuwa CCM imepata wabunge wengi, na inaongoza Halmashauri zote, kuna wagombea wa upinzani walioonesha kuwa na hoja nzito zenye kujenga nchi. Hivyo basi, nashauri nafasi10 za Rais kuteua wabunge, awateue hao wa upinzani hasa kutoka vyama vidogo ili kuvipa msukumo wa kisiasa
 
Magufulu amteue Lissu kwenye serikali yake ili iweje? Itakuwa ni kumkaribisha shetani kwenye kazi ya kutumikia wananchi
 
Mkuu mwengeso , japo sikubaliani na wewe, lakini hoja yako ni ya msingi sana, na kati ya hao wapinzani wengine amteue yule Bidada Qeen Sendiga

P
 
Mkuu mwenge, japo sikubaliani na wewe, lakini hoja yako ni ya msingi sana, na kati ya hao wapinzani wengine amteue yule Bidada Qeen Sendiga

P

Kwa kuwa Urais ni Taasisi kubwa na ya kipekee katika kila nchi, una jinsi ya kutambua uwezo na uadilifu wa kila mwananchi. Hivyo uteuzi wa kujaza nafasi 10 naamini utazingatia taarifa za mtu binafsi. Kama ulivyompendekeza huyo Bidada, nami napendekeza uteuzi wa baadhi ya wagombea wa nafasi ya Urais kujaza nafasi. Kwa uteuzi kutoka kambi ya Upinzani, mbugeni wataweza kuunda Serikali Kivuli na hatimaye kuandaa bajeti mbadala.
 
Mkuu mirisho pm , thanks kwa objectivity yako kwenye bandiko hili.

P
 
Wamfutie kesi zote. Alitaka kuandamana, wampe na bendi ili afurahie maandamano. TL asiguswe kabisaa
 
Mmmh akifanya hivyo utakuwa mtego ili akamalizie kazi ambayo hakuifanya vizuri pale Area D makazi ya viongozi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…