Huu Uzi ni mzuri sana katika kuwafundisha watu juu ya biashara ya FOREX
Binafsi Nina uzoefu wa hii biashara, kwa hiyo napenda kushare machache humu ili watu watambue faida na risk zake..
Kwanza kifupi ni kwamba hii biashara sio rahisi kama wengi wanavyodhani, ina hitaji umakini wa hali ya juu maana unakuwa umekubaliana na mambo mawili. Profit au loss.
Hatua ya kwanza kabisa inabidi uchague broker (hapa pia panahitaji umakini).. Baada ya kuchagua broker inabidi umstudy kwa kina maana kumbuka kwamba wewe unahitaji profit na broker nae anahitaji profit kupitia ku-loose kwako au kuwin (hapa ni brokers wachache)
Kifupi ni kwamba unahitaji kupata uzoefu kidogo kwa kuangalia trend ya biashara kwenye FOREX lakini pia kupitia mtu ambaye ana uzoefu wa kutosha kwenye hii biashara FOREX (hapa itabidi upate mkweli)
Jambo lingine LA msingi ni kufahamu risk ambazo utakumbana nazo katika hii biashara, tambua kwamba kila mtu anahitaji faida kupitia hii biashara, kwa hiyo kupata kwako loss ndio faida kwa mwingine (kwa lugha nyingine naweza kusema ni struggle for the fittest)
Nirudi kwa mtoa mada, kwanza nimpongeze kwa kujaribu kuelezea kwa ufupi uhalisia wa biashara hii lakini kuna Vitu ametazamia kwa lengo la yeye kujiongezea kipato (japokua kihalali) kutoka wa watu watakao kuwa tayari kuianza biashara hii..
Nafafanua kidogo:-
1. Mtoa mada amesema ana mpango wa kufungua office na kutoa train kwa watu 300 bure kwa kushirikiana na brokers alioingia nao ubia (ni wazo zuri)
Naamini train hiyo itakuwa inamzungumia broker (aliyeingia nae ubia) jinsi anavyofanya kazi, offer zake na faida kwa mtu atakayejiunga kupitia huyo broker...
Kwahiyo baada ya train hao watu 300 watajiunga na kuwaambia wengine kujiunga kupitia broker aliyewapa train (na hapa ndipo anapopata faida kupitia watu wanaomtumia broker aliyeingia nae ubia.. Kwahiyo hapo wewe pamoja na broker your fighting for profit... kwahiyo mmoja aki-lose ndio faida ya Mwingine).. Ndio maana nasema hapa inahitaji umakini mkubwa sana.
2. Kama lengo LA mtoa mada ni kugain profit kupitia ubia wake na broker na watu watakaojiunga. Basi naamini katika training atajikita zaidi kuelezea benefits zaid kuliko risks maana target yake ni kuku-win wewe, kwa mantiki hiyo hawezi kujikita zaidi katika risk maana anajua utaogopa atakukosa.
Ndio maana Jambo la msingi unapaswa kujiuliza ni kwanini mtoa mada amekubali kuingia gharama zote hizo kuleta mentors?? (Usifikiri in positive ways pekee yake, check on both side +ve & -ve)
Pili kwanini sahivi anataka kufungua office?? Kwanini asingetengeneza Whatsapp group akatoa elimu bila kusubiri apate office ili atoe fursa kwa watu wa mikoani??
Maana me naamini kumpatia mtu juu ya hii elimu haihitaji uwe na ofisi wala uwe nae ana kwa ana (me niliipata hii elimu kupitia internet pamoja na kusoma vitabu, lakini sahivi nafanya vizuri)
Mwisho nawashauri ni vizuri mkawa makini sana na kujiridhisha kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.
NB: hayo ni mawazo yangu kulingana na uelewa wangu na uzoefu wangu juu ya biashara ya FOREX, sijatoa kwa lengo LA kum-criticise mtu bali kwa lengo la kuelimisha zaid.