Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Pole Sana mkuu, FOREX ni biashara ya ukweli Sana, tatizo Ontario aliwaonyesha Dalali tapeli (fake Broker) wapo madalali wazuri mno wa FOREX, Ontario pumbavu sana akashawishi watu wajiunge na JP markets kumbe ana kamisheni kila watu wakiunguziwa akaunt, FOREX ni lazima uijue vizuri kwanza inahitaji ujisomee sana kuijua FOREX na uwe na smart mind, na siyo kukurupuka tu hapo lazima uichukie FOREX, ukiijua vyema, hakuna biashara yenye pesa Duniani kama FOREX, yaani Hakuna.
 
Hivi "Double Entry" system ya Forex imekaaje?
Niki-Debit kwangu, wapi kunakua Credited?
Yaani niki-gain, nani ana loose?, na niki-loose nani ana-gain?
uki gain ume gain Hakuna anaye loose, ni pesa yako imezaa, na Broker naye ana gain 12% ya pesa yako uliyotumia ku trade, mfano $5 per single trade wewe unapata $4 na Broker $1,uki loose Broker anakula yote $5,FOREX tamu Sana hakyanani.
 
Nadhani sasa amekuelewa, Hakuna biashara tamu na yenye pesa Kama FOREX Duniani, mimi kwa mtaji wa $100 tu kila siku nakuja $45 faida sawa na sh 110,000 Kwa siku, niliteseka Sana kujifunza na wakati naanza nilikula loss zaidi ya mara tatu lakini sikukata tamaa, Leo nakula bata tu.
 
Forex iko na faida kama utakubali kufuata taratibu zake.

Ila ukiingia kwa pupa, umeliwa
 
Kujaribu hutaki inaishia kusikiliza wanayosema watu. Watu mwataka mlishwe kilichotafutwa na wengine, shughuli gani duniani hapa isiyohitaji kutumia akili, fedha na muda kuifanikisha?
 
Forex iko na faida kama utakubali kufuata taratibu zake.

Ila ukiingia kwa pupa, umeliwa
Ukiwa na akili kama za jiwe utaichukia mno FOREX, lakini ukiwa na bongo iliyotulia Kama ya Obama au Clinton ,aisee FOREX ni tamu mno, "you should treat FOREX just like any other business that has Profit and Loss".Ukijua hiyo slogan, FOREX inakutajirisha asubuhi tu.
 
Kuna mwenzako humu jf anaitwa anaitwa CCNP ENGINEER alikua anasema anapiga sio chini ya ma million kila wiki huko FOREX mara paap kafungua thread anaomba ushauri anataka kukopa mil 5 aache kazi akafanye ujasiriamali,hahah
 
Mitaa niliyokulia mimi hakuna mtu anatapeliwa kizembe kuanzia mtoto mdogo hadi wazee,maana matapeli nguli wametokea huko.
Kuna kanuni za maisha ambazo ukizifuata hutakaa utapeliwe.
1.hakuna mtu atakaye kuunganisha kwenye fursa zaidi ya watu wako wa karibu,baba,mama,dada etc.sio mtu baki,we hujiulizi mtu akute mfereji wa hela saa ngapi anapata muda kuwatangazia humu jf?,binaadamu yuko radhi akuonyeshe matumizi yake na sio anapopatia hela.

2.If its sounds too good to be true,its definately not true.Ukiona/kukutana na 'fursa' ambayo inasisimua na kuonekana iko perfect sana basi weka alama ya kiulizo,jamani hakuna namna utaweza kupata mihela kirahisirahisi,ize touch,yaani upakuwa tu mshiko kama una nawa,hela kuipata lazima uminyike one way or another.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…