Je kwanini ubuni?
Unapaswa kujua post code yako, Tembelea ukurasa wa TCRA kupata postcode yako
Sahihi, initial registartion haina tatizo, ni kuweka taarifa zako na account inakuwa tayari kupokea fedha.
Hapo umechanganya habari.
Yaonekana kuwa ulikuwa huna hakika ya nini hasa unatakiwa kufanya, bali ulikuwa ukijaribu kubahatisha. Kitu ambacho sio sahihi.
Skrill ni Moja ya kati ya site zenye mifumo salama zaidi, katika haya maswala ya fedha, site zingine salama ni paypal, alipay, amazon pay etl. Hivyo ondoa shaka katika hilo.
Ili ufanikishe kufanya verification kirahisi
1. Tumia PC
2. Tumia google chrome - itakuwa rahisi kwa sytem yao ku_capture geo location yako, na kufanya zoezi zima kuwa rahisi.
Ukisoma maelekezo kabla ya kuanza kufanya verification hakuna ugumu wowote.
Tatizo linakuja kwa wale wanaotaka kutumia simu kwa process zote ndio hupata tabu.
Kushindwa kuverify taarifa zako, ni uzembe wa mhusika sababu kila kitu kiko wazi stepwise.
Siri ni hiyo hapo juu TUMIA PC na TUMIA CHROME uone kama kuna mahala utakwama.
Skrill wana restriction kwa kadi za mastercard hasa katika kutoa fedha. Ni vyema akatumia au akawa na visa card.
Kwa upande wa usalama skrill wanafanya vizuri, na hii ndio inawaongezea watumiaji kila kukicha.
Nadhani hapa alikuwa anazungumzia kitu asichokijua kiungani.
Skrill wame invest sana katika mifumo ya usalama kuhakikisha watumiaji wanakuwa salama.