Mkuu najua na ninaamini unaelewa kuwa vitabu vingi vya Forex concepts zao ni kuhusu Resistance, Trendline, Zones, Support n.k.
Nakuomba utafute vitabu vinavyozungumzia Forex kwa utofauti na hizo takataka nimezotaja. Kama Forex ingekuwa ni support na resistance mbona Kuna watu wanachora vizuri hizo S&R na waishia kupigwa kama kawa.
Hivi Pesa imekuwa rahisi kihivyo uchore resistance tu na Pesa ije!! Wake up guys Find knowledge. Eti uchore trendline Pesa ije. Huu ni ukweli ambao nitapingwa humu na kila mtu kwasababu tumelishwa hii sumu kuanzia vitabu na wanaotufundisha.
Mbaya zaidi Mtu akijua kuchora S&R au Trend Line anakuwa Mwalimu. Ni mwendo wa kulishana sumu sumu sumu.
Siri kubwa ninayokupa hakuna successful trader anaefanikiwa kwa kuchora S&R au TL. Huo ni uchuro tu (Samahani kwa kusema lugha mbovu ). Na wengi hawawezi kukupa njia ya mafanikio yao. Ukiwa mdadisi na kuweka akili yako iwe huru kufikiri nje ya box utaelewa na kujua ninachomaanisha.