Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Hongera ONTARIO kwa moyo wa dhati kabisa,,naamini una nia njema kabisa,Mungu akutie nguvu
Ila mnaotaka kufanya hii kitu mnahitaji utulivu wa akili na dhamira sababu hakuna kitu rahisi ,,hakuna!
 
Swali la kwanza, leverage inakupa uwezo wewe mwenye account ndogo kufanya trade kubwa. Sio kwamba unakopeshwa hizo hela.
Swali la pili, lot size inategemea na portfolio yako. Ukiwa na portifolio ndogo unashauriwa kutumia lot size ndogo.
Kaka, kama hutajali, naomba urudie kuelezea ni namna gani leverage inafanya kazi. Yes broker anakupa uwezo wewe retail trader kufanya trade kubwa, how? Je leverage ni just a mathematical ratio au ni real money? Na kama ni real money jamaa kauliza ikitokea umeunguza akaunti yako (assume unaenda negative), nini kinatokea?
 

Swala la msingi sana hapo kwenye red, kila la kheyr!
 

Wewe unaona magari ndiyo mafanikio? I'm not looking to be inspired, nadadisi!
 

Mkuu USD ikishuka dhidi ya Euro kwenye hiyo pair thamani ya euro itakuwa kubwa hivyo hipati hasara. Rudi kwenye moja ya comment zangu nyuma nimeelezea kwa mfano rahisi zaidi. Hautopata hasara, utanunua USD kwa kuuza euro then ukiwa na dola zangu mkononi USD ikishuka zaidi utauza Dola zako ununue euro kwa rate ya mwisho ambayo USD ilishuka na sio rate ya awali
 
Kwa hapa mkuu umeeleweka na mm nimeelewa hivyo pia. Wasiwasi wangu ulikuwa kwa mdau anayesema kuwa going short ni kununua currency inayotaka kushuka
 
To some, risking 100$ is a hell of money but others are willing to risk up to 10,000$ and they find its very okay with that.
Hebu naomba tupe na mwanga wa binary options hii imekaaje? (samahani nipo nje kidogo ya mada)
 
Mkuu Ontario Ahsante kwa Uzi Mzuri Usiache kuzidi kututoa tongo tongo c Unajua Wa Tz Ni wabishi Kama Wewe First Time Kuckia About FoRex. Salute
 
Wabongo tunapenda sana kuzungumza vitu tusivyovijua, ukisha google na kusoma website 2-3 unajiona unajua na kuchangia mada kama mjuzi. Hii yote ni wivu, tukidhani Antorio atapata sana kwa hizo ada. Hatuangalii manufaa ambayo yataweza kupatikana kwa hayo madarasa.

Ngoja nikuambie bro, hizi sessions zinajumuisha na live trading, mwanafunzi anaona jinsi unavyo order na kupata au kukosa. Na itakuwa wehu wa hali ya juu watu wahitimu kisha washindwe kutrade, maana yake zile kodi unazolipa Jangid Plaza zitakuwa ni bure maana baada ya first graduation hakuna mwanafunza atakaye mrecommend mwingine.

Pili watabe wa trading hifanya vitu viwili au vitatu: kutrade, train na/au ku-sell signal. Analysis anazozifanya kabla haja trade ndizo anazotumia kufundishia. Akishajua aweke order vipi ana-sell signal na bongolala wananunua na kupiga hela kama kawaida.
 
Suala la risk kalizungumzia kwenye huu uzi mpaka akajitolea na mfano labda kama ukifanya skimming
 
Hii kitu nilishawahi kujisajilj kwenye makampuni ya nje through online wakawa wananipigia sana simu kwamba nianze kufanya trading inafaida kubwa, ilikuwa haipiti siku bila kunipigia simu lakini waliponiambia kuna amount natakiwa kudeposit ili nianze hiyo biashara nilisita nikadhani ni wale matapeli, hivyo sikutaka kuifuatilia tena , na hii ilikuwa kutokana na kutojua biashara yenyewe ilivyo ingawa nina knowledge na mambo ya finance lkn sikuweza kufikiri au kujua km inafanyika online pia,
Hivyo basi mkuu Ontario unaweza kuni invite na mm pia niweze kujifunza hiyo biashara, maana nipo tayari kufanya trading endapo nitajua security yake ya deposit
 
Kuna watu ni Kama vile roho zina wauma kuona kijana kawaza mbali. Tunajua wengi wenu mna muda mrefu kwenye FX lakini hamkuwahi kufikiria kuanzisha your own FX trading firm mkawa na training center pamoja na broker services. Kijana Hana muda mrefu kaiona fursa

Wivu wenu ni Kama wa Ali kiba kwa Diamond, Ali kiba alikuwa kwenye game kitambo lkn hakuwa na mtazamo wa kimataifa Kama Diamond

Ontario haibii mtu na ameweka wazi kila kitu hadi hizo risk. Target yake kubwa ni kusaidia vijana watoke kwa hicho kidogo walicho nacho sasa in the process lazima na yeye afaidike na sidhani Kama ni dhambi yeye kufaidika.

Binafsi nitajiunga na training akishaanza kutoza ada, hii ya bure watu 300 nawaachia nafasi wengine Wasio na uwezo wa kulipia fee. By the way sina mpango wa kufanya trade sooner Bali nataka kujifunza nijiongezee maarifa

Tuache maneno tuweke muziki, acheni watu wajifunze wajaribu wakishndwa basi lkn at least wajaribu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…