Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Sawa nimekusoma

Lakini let be honest for a minute

Foreign Exchange Market ni speculative process.

Kwa maana hii naona nafasi ya traders wadogo kupiga chapaa inakuwa minimized na upatikanaji wa taarifa kwao.

Pia ni ukweli traders wadogo hawana control yoyote dhidi ya brokers wanaowatumia

Hii business haina regulations, only demand and supply ndiyo inasimamia kila kitu. Hapa maana yake broker ndiyo "King" anaweza amua kufanya manipulation

Pia kwa sababu ya high volume of liquidity traders wadogo ni rahisi sana ku-over trade na mambo yakiwa tofauti ni kilio.

Wangapi hapa wapo tayari ku-risk $1000?

Je hizo $1000 zikipukutishwa wataongeza nyingine kufidia losses?

Binafsi naona forex unahitaji kwanza kuwa na vijisenti kwasababu kuna msemo Failure is the mother of success.

Na hii ipo ki mkakati maana kupigwa kwenye forex week chache za mwanzo ni rahisi kama vile mtoto anayefijunza kutembea anavyoanguka mara kwa mara

Binafsi naona ili upate profit lazima muda mrefu wa kujifunza uhusike na kama ulivyosema usiingize emotions. Yaani uwe professional kabisa.

Boss!! Twende pole pole. Kwa kiasi fulani nakubaliana na hoja zako, kwa kiasi fulani napingana na hoja zako pia.

Yes! Fx ni speculation. How does that minimizes retail trader's profitability. Hebu nambie vizuri.

Pili, unasema retail trader hawezi kumRegulate broker... sijui umeandika kwa bahati mbaya ama vipi? Yani unamaanisha Trader amregulate vipi broker, forex is about you and the market. Broker hana chochote zaidi ya kukupa platform inayokulink na global market. Sasa unataka trader aRegulate nini, specifically??

Pia unasema broker is the 'king' - king wa nini?! Hapa kuna soko, hapa kuna wewe trader, general principle iliyopo kama ulivyosema ni demand and supply ya currencies ktk soko, sasa hapa Broker anakuaje king?! How can a broker manipulate a $5 trillion market?! Nakubali market makers wana nguvu yao, but that doesn't mean wanaweza kukusababisha kila trade iwe losing trade. Hiyo haipo.

Swala la kuover trade ni discipline na psychology ya mtu, haziendani kutokana na liquidity iliyopo sokoni. Mtu akiamua kuover trade ni kwa mapenzi yake.

Hakuna haga principle 1 ya trading inayosema unahitaji vijisenti - traders need right information, right knowledge, skills and strategies pamoja na emotions control. Mtu anaweza kuraise $100 hadi kuwa $1000 ndani ya less than a month. Na vile vile kutokana na leverage pesa hiyo hiyo unaweza kuipoteza kama haujui nini unafanya.

Zaidi ya yote ninakubaliana na wewe kuwa forex si get rich quick scheme, inabidi ufahamu ndani nje, inabidi uwe na knowledge, inabidi ugharamie muda mwingi kujifunza. Na zaidi ya yote huwezi kuwa Pro trader bila kuwa newbie - lazima utoke from 1 point to another. Kwasababu mtu si Pro hakumfanyi asijifunze forex na kuwa Pro, we all started from somewhere. It takes time, but it's worth it.
 
Asante kwa uzi mzuri wa kujenga. Ni kweli wapo watu wengi wanafanya trade hasa wahindi kwa hapa Tanzania. Mimi nilisikia mwaka 2012, nikajifunza mwaka mzima. Nitaweka screen shot ya kile ninachoweza kutengeneza ndani ya miezi mitatu. Kikubwa kuliko yote kwa anayetaka kujiunga kama alivyosema mtaalam ni lazma akubali kukaa chini ajifunze kwanza. Pamoja na kwamba amejaribu ku-simplfy lugha ya trade ili kwa mtu ambaye haifahamu aweze kuelewa nini alichosema, ila mkianza kujifunza mtaelewa vizuri nini anachomaanisha. Nawatakia mafanikio wote mtakaomua kuanza kujifunza
 
mkuu ni wapi / mtandao gan naeza fungua hyo account ya forex nkaeza kuanza na demo accnt
 
brother ontario, nimekupata poa sana sema me ni science case kuhusu trading niko empty lakini kwa habari ya hiyo thread ya forex nimekupata fresh kabisa and nimekuwa impressed nayo me nipo tayari ku settle chini na kujifunza please naomba unisaidie jinsi ya kupata data za forex trading utakuwa umenisave sana mkubwa.
 
Asante kwa uzi mzuri wa kujenga. Ni kweli wapo watu wengi wanafanya trade hasa wahindi kwa hapa Tanzania. Mimi nilisikia mwaka 2012, nikajifunza mwaka mzima. Nitaweka screen shot ya kile ninachoweza kutengeneza ndani ya miezi mitatu. Kikubwa kuliko yote kwa anayetaka kujiunga kama alivyosema mtaalam ni lazma akubali kukaa chini ajifunze kwanza. Pamoja na kwamba amejaribu ku-simplfy lugha ya trade ili kwa mtu ambaye haifahamu aweze kuelewa nini alichosema, ila mkianza kujifunza mtaelewa vizuri nini anachomaanisha. Nawatakia mafanikio wote mtakaomua kuanza kujifunza
mkuu weka haraka
 
Wale ambao wamekitafuta kitabu kilichokuwa recomended "Currency Trading for dummies by Brian Dolan, 2nd edition" bila mafanikio ama wamepata ambacho hakijakamilika na chenye pages pungufu, hii hapa copy ya kitabu full nimewaatachia. Kina pages 384. Hope mkisoma zote, mtapata mwangaza wa mahala pa kuanzia.
Asante sanaa ubarikiwe mkuu
 
Hata mimi ninahitaji kuwepo kwenye hiyo list ya watu 300. Sisi watu tuliokula chumvi kiasi tuliwahi ifuatilia miaka kama 10 na ushei iliyopita but kwakuwa kipindi hicho hakukuwa na sources za kutosha na access ya information tukaacha. So I believe ni good business la msingi ni kuwa knowledgeable kadri inavyotakiwa.

hii biashara nilivutiwa nayo sana those days ila sikujua pa kuanzia.
 
Mkuu Nadhani unapenda kujulikana.Kama umeusoma uzi huu Na kuelewa usinge andika pumba.Au wewe ndio hao wasio taka jamii kufahamu Forex?

Samahani kama nimekukwaza, lakini nakuonea huruma kama huwezi kusoma kwa umakini na kuona mlindimo wa koments zangu. Sijasema elimu iliyotolewa ni mbovu, la hasha, ila imetolewa kabla ya ktengeneza mazingira ya kuwa na mzunguko wa hizo pesa za nje. Ni ndoto kufikiria unaweza kufanya biashara hii ukiwa hapa pasipokuwa na mzunguko kabisa wa pesa za kigeni. Nimesema ni somo zuri sana kwa mjukuu wangu. Ugumu wa somo hili ambao naadhani kwako ni kama uatandu wa buibui kuelewa unatengenezwaje jiulize kwa nini hawa wawekezaji wakubwa kwa mfano wa mahoteli na majumba ya kupangisha wanafanya bei zao kwa dola (unalipa kwa rate ya siku hiyo).
Kwa hiyo, na hapo chambua mchele na ubaki na PUMBA zako.
 
Thread nzuri sana
Hongera sana kwa kuendelea kumotivate vijana tangu kule kwenye kilimo na ufugaji mpaka huku forex Mungu akubariki Ontario.
 
Ni vizuri ametukumbusha kuhusu Forex Trading ingawa baadhi yetu tulisha isikia bila kuchunguza zaidi. Lakini pia nimemuelewa kwamba Ontario lengo lake ni kuanzisha u broker ili atengeneze pesa kwa commission. Wabongo wanatakiwa wawe waangalifu amasivyo watapoteza pesa kwa pupa. Kwanza hiyo training atakayo toa ni bure au ndiyo njia ya kujipatia pesa?

Very good! Wewe uko makini mno, and in that way umeelewa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom