Danpol
JF-Expert Member
- Aug 15, 2013
- 5,727
- 8,918
Mkuu, swala la elimu juu ya kitu fulani ni swala pana sana, na kuna njia nyingi mno za kupata elimu yenyewe, njia kuu mbili zilizo zoeleka ni ELIMU kwa maana ya kusoma na nyingne ni real life experience
Eneo la kwanza ambalo ni elimu umesha lipitia yaani kusoma, njia ya pili sasa na ambayo ndio ya muhimu kuliko vyoote ni real life experience naona umeizuia kabisa kwako, huitaki kabisa..
Ni kwanini nasema haya
Ukiangalia trade zako, mara nyingi kama sio zote umekua MVIZIAJI, hau trade kulingana na elimu uliyo pata na pia hautaki kulipa fursa soko likufunze yaani likupe real life experience ya forex ilivyo, unakosea sana mkuu,
Ukiendelea kuvia once trade ziki turn blue unaamua ku close position kwa hakika utakua hakuna unachofanya, pili, hakuna elimu wala experience ya soko unayopata, liache soko lipumue, fanya analysis yako vizuri, ingia sokon ukiwa na sababu ni kwanini nimeamua ku trade hivi, kua na target yako unataka ku archive nini kwenye hiyo trade, ukiweza hifadhi hata screenshot before and after trade, endapo soko likienda vizuri ama vibaya rudi kwenye analysis uongeze ujuzi ama upate funzo n kwann nilioa A ikatokea O... usivizie vizie hvyo mkuu
ipo siku utapiga hasara ya maana.. at the same time unakuta ukirudi kwenye kumbukumbu una winning trade karibu 50 mfululizo... hasara moja tu inakomba kila kitu, wakati ungetembea na risk vs reward ratio nzuri hiyo hasara wala isingekutikisa, Risk vs reward ratio ni vitu ambavyo hupaswi vitenga, pitia pita Astroforex
Mengine nikupongeze, you are doing good, ila tu acha kunyelea nyemela, lete hata screenshot hapa yenye Faid ndefu ndefu kidgo sio 1.09 kwa position moja...