Ni kweli kusoma vitabu sio suruhisho la kujua Forex Trading, inakubidi utengeneze strategy yako ukiwa ktk demo kisha ndio uitumie ktk live trading, ujitume na ujue kila session ina tabia zipi na pair ipi ina tabia gani mda wa trading hivyo itakurahisishia kujua trading vizuri na sio kutanga tanga. Walio wengi watapenda wakufundishe zile mbinu zao zao ilaukijituma ukawa mzuri wa kudadisi utaelewa wapi uanzie ili kusudi ukikutana na mtu wa kukupa mbinu zake utaunga na zile zako ili ufike mbali. Vitabu ni vingi, kila mtu kaandika lake na ana mbinu zake, binafsi nimekusanya vitabu vipatavyo 180. Ila ktk kuongea na mtu m1 alinambia inabidi ujueprice action ndio msingi wa forex, alinidai nimlipe kiasi kadhaaambacho kwa mda huu sio rahisi mie kukipata. Nilishukuru kwa kunitajia neno "PRICE ACTION" wengi watapenda kukwambia Forex ni hivi na vile ila vitabu vyenye madini husika hawataki kusema. Baada ya hilo nilitafuta kitabu vitabu vya PRICE action vikatimia 18, niliona kazi itakuwa ngumu japokuwa napenda kusoma vitabu ili khali mpaka mda huo kabla ya kufatilia story behind price action nilikuwa nimemaliza kusoma Forex Bible, nikaongezea vitabu vingine 3 ambavyo vyote vinaelezea mbinu.
Mwisho wa siku graph yangu ilijaa uchafu mwingi, nilichokuja kugunduakila mwandisi alikuwa akisema nakupa mbinu zangu ili uzijaribu kama zitakufaa uziongeze kwako pia. Ndipo nikajua hapa inatakiwa mtu uwe na system yako tayari.
With no fear nilisema nitaanza kuhumu kitabu kwa kava yake japo ni kosa, Mungu si mchoyo alinijaalia kukipata kitabu ambacho ndicho kimekuwa mwanga wa Forex ili hata nikiamua kukutana na mentor yeyote yule sitakuwa gizani ama hatonitoa from zero to hero.
KABLA YA HAYO YOTE: Ni kuwa niliweza kuzifahamu candlesticks karibia zote, nilfanya uamuzi wa kutoa uchafu wote indicators nikaanza demo kwa $25 ambazo nili-blow account 3 kwa kuzijaribu candlestick kama ni kweli zinasema ukweli
😀😀😀
Baadae niliamua kuacha kuzijaribu nimeamini hazidanganyi, japo kuna watu nyuma ya uwepo wa hizo candlestick nikafungua demo nyingine na kuanzia $25 ambazo niliweka malengo ya kupata $5 kila siku, niliweza kufanya hivyo na kufanikiwa kupata faida
Day 1: $11.88
Day 2: $15.04
Day 3: $26
Hapo mtaji wangu ulikuwa na kuamua kuongeza dau la lot size kwa kanuni niliyojitungia mwenyewe, usiku wa siku ya 4 yaani saa 7 za ki
TZ nilifanya trading za currency pair 1 tu kwa position 2 tofauti na kuweka TP (take profit) nilipitiwa na usingizi ki-ukweli nikashtuka saa 11 nikakuta zimeingia $64 hiyo ni siku ya 4 alfajiri hapo ndipo nilipata kuongeza tena lot size yangu kwa kanuni yangu mwenyewe sio ya kwenye vitabu, nilisaka currency pair inayochangamka nikazisoma candlestick zisizodanganya mara nyingi kiukweli kama ni live akaunti nilifanya overtrading na kupata $200 jumla nikawa na faida ya jumla ya $286, nikabaki na currency pair hiyo hiyo ikaleta viashiria vya soko kubadili kuelekeo nikaingia mzigoni nikaingia muamala zikasoma mpaka $212 faida ikiwa ningefunga faida ningekuwa na jumla ya $498 kama faida ya siku ya 4 na ilikuwa ni Asia session tu kabla ya London, zilionekana candles za reversal kwa kuwa ni demo candles zikaanza kubadilika taratibu mapa faida ikaja kwenye $150 kwa position ile, nikawa makini kuziangalia zile candlesticks nikaziona kuwa ni ishara ya trend kubadili uelekeo ila nilipuuza tena mwisho akaunti ikaenda na maji, kumbuka mtaji wangu ulikuwa tayari umefikia $365 kabla ya ile 212, nilifunguademo nyingine ambayo niliikuza hadi $989, mwisho niliamua kurudi ktk zoezi langu la mtaji naotegemea kuanza nao ila mwisho wa siku nikawa na uchu, ulafi na upuuzi ambao umezungumziwa ktk vitabu mara nyingi, ila kiujumla akaunti nazikuza zote.
Baada ya historia hiyo fupi ni kwamba nilijiona nimejua ninao uwezo wa kufungua live iwapo ningepata hela, rafiki yangu alienishawishi kusoma forex alinikatalia, nikameshimu na kuanza kusoma ila sikupata kitabu gani nisome maana nina vitabu vingi, mwisho ndipo nikapata kitabu kama nilivyosema awali nilihukumu kwa kava, nikavutiwa na The Candlestick Trading Bible ambacho unaweza kukipakua hapa
THE CANDLESTICK TRADING BIBLE.pdf kinaelezea Price action, nimeona ndi msaada wangu hicho kitabu hivyo nimeona wengi wetu tunakwamishwa na kipato japo sijaanza live ila nafsi inanisuta kwa kutoshare kile nilichogundua.
Nia yangu:- Tusiwe wavivu kusoma, tusiwe wachoyo kuelekezana wapi tuanzie ili mtu ajihukumu badala ya kutanguliza hela mbele, mpe mtu materials wapi aanzie kusudi yeye aamue 1 kujisomea alone ama alipe ada. Mentor atabaki pale pale usije jidanganya, game la forex alone hutoboi.
Nyongeza ni hii telegram channel yenye vitabu vingi kuhusu masuala ya hela n.k
Traders Library huenda mtu alishai-share nami naikazia. Nitaleta mrejesho mafanikio yangu nitakapoanza live, kwa sasa naendlea na demo niive vizuri
😎😎😎