shadownet
Senior Member
- Aug 4, 2015
- 133
- 677
Kwa swali hili nina imani nitakua sijavunja misingi ya jamii forums
Hivi hakuna shuhuda za upande wa pili? Kula hasara? Nimesoma sana posts za forex humu ndani lakini naona watu wanakula tu🙂🙂, Najiuliza sana maana naona sample za kula tu watu wakivuta tu pesa, je kati ya watu 300 waliokula training na wanatrade hakuna aliyepoteza, Kuna post imeanzishwa ya ushuhuda wa mafanikio ya wiki chache tangu walipoanza kufundishwa forex na nimegundua shuhuda ni za wale waliopiga pesa tu, Je hakuna waliopunwa , kwanini zisiwekwe picha za ushuhuda kula hasara ili tujifunze kwamba forex sio kula tu.
- Kama wapo kwanini tusitumie mifano yao pia kama lessons ili tumfukuze pepo kuliwa katika injili hii ya Forex?☺
KILA KITU UNACHOWEKEZA PESA KINA HASARA IWE BIASHARA, KUBETI HATA FOREX