FOREX: Hivi hakuna shuhuda za upande wa pili? Kula hasara

Mod msitoe wala kuunganisha uzi huu,hii ni taarifa huru.

Kwa wote mnaendelea kuifuatilia Biashara ya Forex Trading kama ilivyotambulishwa na ndugu [HASHTAG]#Ontario[/HASHTAG] humu JF na sasa kuonekana inashika kasi nimeoona si vibaya tukashirikishana hili.

Nimejaribu kutembelea Website ya moja kwa moja ya FXTM na kufanya usajali wa awali, katika hatua hizo nilibahatika kupata number ya simu na kuchart nao ,bad luck majibu waliyonipa yalikua negative. Kwa kifupi niliwauliza kama wanajua kinachoendelea TZ , direct walisema hawajua lolote na hawana taarifa zaidi juu ya biashara yao nchini TZ .

Sina lengo la kurudisha biashara hii nyuma ila pia ni vyema tukawa wachunguzi wa mambo katika hatua za awali.

Kwa muda wako unaweza kutembelea site link hii hapo chini na kama hutotaka kufika huko Number waliyonayo kwenye Site hiyoo ni +447593612469.

Wapo verry active katika kureply lolote utakalowauliza kuhusu Biashara yao.
(Majibu mtakayopata yatatusaidia kukusanya dots na kujua hiki kinachofanyika kwetu kipo katika status ipi ya uhalisia wa biashara husika).





Forex Trading with FXTM
 
Hiyo forex kutwa munaitangaza na ukisearch rissk zake ni kubwa nenda youtube mtafute huyu jamaa
 
sijui kama umesoma nilichokiandika . Ila its Okay Binafsi nimekuelewa . Ahasnte .
Brother sorry sana sikusoma vzr hope umenisamehe mana huwa naona watu humu kila kukicha na forex kitu ambacho kwa tz bado kuwa chakuaminika nimefurahi naae kuwa mpingaji wa huu utaoeli mpya mjini
 
[Forex trading is not for everyone]
Mimi kujipima kwangu kote na kusoma majibu ya watu mbalimbali walioshiriki, wanaoshiriki 4rex trading mitandaoni zikiwemo reddit na quora, nikaona kabisa this thing doesn't match my risk tolerance level.
Ila watu wanapiga ela, japo changamoto hazikosekani.
Kama umeelewa ingia jaribu bahati yako, ukishindwa angalia utaratibu mwingine.
 
Brother sorry sana sikusoma vzr hope umenisamehe mana huwa naona watu humu kila kukicha na forex kitu ambacho kwa tz bado kuwa chakuaminika nimefurahi naae kuwa mpingaji wa huu utaoeli mpya mjini
Hakuna Shida Mkuu.
Japo pia mm sio mpiganaji wa kupinga , ila nimpiganaji wa kufanya research & Critical analysis.
 
Hiyo zali bora uende na hiyo oesa casino
 
Issue ya wao kujua kinachoendelea kenya, uganda au congo sio rahisi kujua kwasababu nadhani wapo brokers sehemu mbali mbali duniani ambako watu ndo hujiunga humo na kufanya michakato yao, kwa hiyo ukiwauliza ya Tanzania watakuwa hawana cha kukujibu. Sidhani kama hiyo point ina mashiko.
 
Mkuu huyo broker watu weng hawamtumii eg.... Watu wanaopita TMT wanatumia jpmarkets
 
Nadhani hutapata mwenye kuzungumzia hasara!
Na kampuni imekuwa na ushawishi Mkubwa Kwa kutoa positives tu! Nadhani sababu kubwa itakuwa ni kutokana na kutosajiliwa na chombo chochote cha serikali kinacho wa regulate hawa jamaa.
Mbali na kuwa na usajili Wa BRELA, leseni ya manispaa na TIN number sidhani kama wanapata leseni ingine Kwa mamlaka kama vile Benki kuu, cmsa, wizara ya viwanda na biashara etc
Mamlaka nilizotaja halo kuu zingewataka waweke warning statements kwenye matangazo yao. Kwa mfano kampuni mpya zinazota kujiunga na soko LA mitaji (DSE) ni lazima zitengeneze waraka Wa matarajio ( prospectus) ambayo itakuwa na tahadhari ndani yake Kwa wawekezaji. Mara nyingi ile cautionary statement hueleza Kwa uwazi kabisa kwamba ununuzi Wa hisa unaweza kukusababishia hasara kutokana na fluctuation ya bei sokoni, Kwa hivyo wekeza kile kiasi ambacho itakuwa tayari kupoteza endapo soko litayumba.
Vivyo hivyo forex trading ni risk, kupoteza fedha zako ni possibility mojawapo. Kwa hivyo hawa mentors na trainers nashauri waliweke swala hili Kwa uwazi zaidi kabla ya kuchukua fedha za watu (training fees).
 

Umeongea vyema, ila naomba nikuulize swali kwa akili ya kawaida tuu ubongo wa mwanadamu una uwezo wa kuchekecha na kupima jambo kabla haujaamua kulifanya, kinachofanya watu wafanye forex sio TMT ni watu wenyewe baada ya kupata anamweleza na jirani/rafiki/mjomba/shangazi

Kuhusu risk jamaa alishaeleza sana SANA SANA SANA kwenye yzi wake wa kwanza na pia darasni watu huelezwa pia

Hayo mengine yapo kwenye michakato
 
Ukiona biashara ambayo mnatafutwa watu wengi namna hiyo jua kuna walakini, a real business haiko hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…