Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

jooohs

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
2,524
Reaction score
10,287
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi ni kijana umri miaka 23 nimehitimu chuo mwaka huu .lakini kutokana na changamoto za ajira vijana wengi tumekuwa tukitafuta njia tofauti tofauti za kutokea ilimradi tupunguze ukali wa njaa iliyoko mtaani.

Kifupi wakati nilikuwa nasoma nilikuwa na hofu sana kuwa nikimaliza masomo yangu nitafanya nini nisipopata Ajira kitu ambacho kilinifanya niwe nachukua muda mwingi hapa jamii forum kusoma mada mbalimbali za baishara kilimo na ujasiliamali.

Mwaka 2017 wakati niko likizo nimemaliza mwaka wa kwanza nilipata kusoma mada inayohusu forex humu jukwaan kwakweli nilihamasika sana japo nilikuwa sina uwezo wa kuhudhuria mafunzo nilisema nitakomaa mwenyewe mpaka nielewe ,nilitumia muda mwingi youtube kudownload vitabu na kusoma mpaka nikapata mwanga kidogo.

Wakati tunaenda Kuanza mwaka wa pili kumbe kunajamaa yangu alihudhuria mafunzo kabisa akaanza kutupa muongozo namna soko linavyofanya kazi ukweli kutokana na tamaa ya kupata pesa tuliunda kikundi kila mmoja akafungua acc baada ya boom kutoka tukadeposite nakuanza kutrade.

Tulitumia muda mwingi kujadili forex mimi na wenzangu kuliko kituchochote kusoma ilikuwa kama part time muda wote unakuta tumekodolea macho kwenye simu nakufanya analysis kuhusiana na currencies tofauti.

Mbali na hapo tulikuwa tukijadili jinsi tutakavyo nunua magari makali siku ya graduation tuendenayo mlimani city .Halafu tukimaliza tukodishe ofisi kwenye lile jengo refu pembeni ya mawasiliano tower tuwe tunafundisha watu kuhusu foreign exchange.

Lakini kadri ya siku zilivyokuwa zinazidi ndio soko lilivyokuwa linazidi kuwa gumu maana Leo umepata faida dola 100 kesho umepigwa dola 150 ,kesho umeingiza 50 kesho kutwa umepigwa 100 maisha yalienda hivyo performance kwenye masomo ikashuka lakini hatukujali kwani tulijua kwa usawa wa magu ajira hakuna ,bora tukomae na forex ipo siku tutatoka.

Kifupi mpaka kufika mwaka wa tatu jamaa zangu walikuwa na madeni makubwa maana walianza kuchukua pesa kwa wanafunzi wengine wanatrade kwa riba na pesa zinaungua tu walianza kuuza vitu vya ndani laptop freezer subwoofer ili waongezee pesa za mtaji na wafidie madeni, wakati huo mimi bado nilikuwa nimebebana na jamaa yangu mabibo hostel wote 3rd year.

Nilikaa nikafikiri maisha ya nyumbani sio mazuri na forex ndio nilijua itanitoa kimaisha japokuwa inachangamoto ndogondogo nikiangalia acc ya benki sina hata shilingi zaidi ya pesa ya kula maboom nimebaki nayo mawili nikasema nijibane hiyopesa niichanganye ifike milioni moja nitrade kwa uangalifu labda itanitoa maana niliamini million 1 inakaribia kwenye dola 500 .

Asee sijui ilikuwa ni bahati maana nilichanganya zote nikatrade nikapata kama dola 2600 ndani ya kama wiki 3 maana nilikuwa nafungua tu order na risk management nilikuwa sifanyi vizuri ,nilitoa dola 1300 kama million 3 hivi nikaenda riverside nikapanga chumba self 100000 per month ndio napoka mpaka sasa ,kwa miezi sita nikanunua kitanda godoro, nikanunua TV 500k, feni, gesi, meza na viti, subwoofer,Friji getto likajaaa .

Kwenye Trading acc nilibaki na dola 1300 nikasema hii siwezi poteza nitakuwa na trade natoa pesa kidogo kidogo hata dola 50 per day ambayo ni zaidi ya 100k nikaona maisha nimeyapatia sisumbuki kutafuta kazi nikutrade full time .nikawa nikiingia humu jamii forum natafuta ule uzi wa magari mazuri naangalia nikijua anytime navuta mkoko.

Daa baada ya kumaliza chuo nikawa mimi na soko ,soko na mimi nilijitahidi nikapandisha acc mpaka dola 1600

Asee siku ya mkosi ilivyofika ilikuwa ni kwenye muda wa saa 1 1 jion kulikuwa na newz ya gbp nimeingia na kama lotsize ya 1 forex trader mnanielewa vizuri soko lilienda agaist na mimi nikajikuta naongeza tena lot ya 1 huwezi amini pesa yote ilichomeka sikubaki hata na Mia kwenye acc

Nilihisi kuchanganyikiwa na ukubwa wote nilionao nililia kama mtoto mdogo siku pata usingizi siku nzima huku lawama zote nikimtupia mungu kwa nini ameruhusu pesa yote zaidi ya 3.7m kupotea ndani ya masaa machache.

Pesa niliokuwa nimebakinayo mpesa ilikuwa laki 4 kwa kile kipigo niliogopa kurudisha hiyo pesa kwenye forex kwani ilikuwa haifika hata dola 200 nikaanza kujiuliza nitaishi vipi hapa town na sina mtu hata wakuomba sh 100 . Nikaanza kuona simu za mama nazikwepa kwani nilikuwa nimezoea kumtumia pesa nashindwa akiniomba nitafanyaje.

Baasi nikatafuta rafiki yangu alikuwa anauza karoti ilala boma kwenye meza najua wenyeji wapale wanaelewa vizuri nikwamwabia anitafutie eneo kweli akaniambia per day meza unalipia 1000 na ushuru sasa mwenye meza anataka 60k ya miezi miwili nikasema poah ,nikampatia jamaa yangu pesa .

Akaniambia mwenye eneo amesema mkataba wa mtu anaetakiwa kuondoka unaisha baada ya siku 3. zikifika nikaanze biashara nikaenda kununua mzani kkoo wa kupimia 80k daa nilisubiria eneo jamaa aliekuwa anatakiwa kunipisha haondoki nikawa nimetapeliwa hivyo. Jamaa yangu kwa kuona hivyo akaniambia twende tukashitaki polisi turudishiwe pesa yetu.

Nikafikiria pesa niliyopoteza 3.7m kwa 60k nikaamua nipotezeee ,yule jamaa yangu akahisi labda anamakosa akaniambia kwenye meza yake niwe nachukua mzigo tunachanganya nikakubali lakini profit perday ilikuwa tunapata kama 15k nikaona namzibia jamaa riziki yake nikamwabia nimepata kazi mahali nikaondoka na mzani nikamuachia.

Nikarudi kukaa geto mpesa nikawa nimebaki na 170000 nikasema nizunguke hata kwenye karakana za furniture labda naweza kupata kazi huku nikijifunza wapi ,viwanda vya matofali unakutana na vibarua tu wanapiga kazi.

Nikahisi kukata tamaa nikatafuta kila njia ikashindikana nikasema nifanyeje nikapata wazo nijaribu kufanya betting kwani kipindi cha nyuma nilikuwa nafanya ndani ya wiki moja nikawa nimepoteza pesa yote hata pesa ya kula nikakosa ikabidi nimfate yule jamaa wa ilala nikamwabia kazi imebuma anipatie 30k nimuachie ule mzani akanipatia nikanunua msosi geto.

Huwa sina tabia ya kuuza vitu hovyo lakini nilitafuta mteja nikauza friji kwa bei ya hasara kama 300k hata miezi mitatu ilikuwa haija maliza, nikaendelea kubet .kila nilipikuwa naendelea kubet ndio pesa ilivyokuwa inazidi kupotea kila siku kuliwa tu asee asikwambie mtu betting sio kazi ya kutegemea inaweza kukuaibisha muda wowote.

Mwezi uliopita kwenye tarehe 20s nikafuma mikeka mitatu siku moja yote nikala zaidi ya 8m siku hiyo siku lala kwa furaha nikiwithdraw kama 7m nikawa nazo getto nimetunza nilibakiza 1m nikabet tena yote nikala 1.5m .wiki ikiyopita nikabet 500k nikala 2.6m jumla nikawa na kwenye acc na 3.6m .
Juzi na Jana nimebet nikapoteza 1m nimeona nitoe 2.6m nichanganye na ile 7m iwe 9.6m.

Nimeona kwa hiki kiasi cha 9.6m najua humu kunawataalam wa biashara wanaweza kunisaidia kunipatia wazo ama ushauri nifanye biashara ipi maana mimi nilikuwa na wazo nifungue kaduka niwe nauza vinywaji vinywaji vikali nichanganyanye na soft drink. Ama nitafute sehemu niuze hata nafaka ila mtaji ndio sijui unahitajika shilingi ngapi.

Note biashara ambayo nimewahi kufanya tofauti na hizo kamali hapo juu ni ufugaki kuku tena zamani sana huko j4.

Nitashukuru sana kwa mchango wako wowote ule utakao utoa maana umri unasogea na majukumu yanazidi kuongezeka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu hii thread yako imekaa kichonganishi sana. Sijaona forex ilipo kufirisi kama heading yako inavyojieleza, zaidi naona imekupa maisha ya kupanga chumba na kukijaza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu unajua pesa ya mtaji niliokuwa nimebakinayo ndio ilikuwa kila kitu kwangu sikutegemea kama itapotea kirahisi hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua $3000 deposit anza kufanya biashara ya forex, fuata RM vizuri baada ya mwaka ww utakua ni mtu mwingine kabisa. Maana forex inaonekana una uzoefu nayo kiaina. Na kubet usiache

Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja ila ajiwekee sheria na kanuni zake na ahakikishe anazifuata. Betting & forex asiache.

Ila afanye biashara mbadala.
 
Naunga mkono hoja ila ajiwekee sheria na kanuni zake na ahakikishe anazifuata. Betting & forex asiache.

Ila afanye biashara mbadala.
Tatizo fx unaweza jiwekea kanunu lakin ukishaanza kutrade unajikuta umeshachapa 0.5 kwenye mtaji wa 100. Ila ushauri wako nitaufanyia kazi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom