Forex sio mafanikio ya haraka kama watu wanavyodanganywa

Forex sio mafanikio ya haraka kama watu wanavyodanganywa

nilijaribu kusoma kwalengo lakuingia uko nikaacha
nikajaribu tena nikaacha
bado nilijaribu tena nikaacha na nimeacha kabisa

majaribio mawili ya mwisho ni kutokana na ushawishi wa jamaa zangu
Mimi bado naendelea kufanya hii "Probability Business" ya kuwindana na Broker. Vita ni kubwa sana almost 7 years ya kutumia Common Forex books, Signals, Indicators, Robots, Sjui Supply and demand na kujifunza kwa You tube videos za abroad na bra bra zoooote bado hii Vita nimekimbia kwa muda. Nimerud nyuma kidogo sija surrender hii Vita bado Mbichi😀

Nimeingia mafichoni kutathmini shida iko wapi. Mbinu gani sasa iliyo sahihi?? Strategy gan nitumie kuspeculate the movement of Price??

Well, Mapema mwaka huu nikakaa chimbo mwenyewe nikajitoa kwenye telegram groups, WhatsApp groups, Un-Following most common Forex mentors na influencers... .e.t.c

Nikafanya uchambuzi wangu binafsi nimefuatilia kwa kina baadhi ya Pairs, Economic data, Geopolitical data dhidi ya Movement of Charts kwa kutumia akili yangu ya kuzaliwa, binafsi kuna vitu vingi nimevigundua vina work vzr 80% kama sio 100% in long run ambavyo sijawah kusoma wala kuona mahala popote.

" If you want something you never had, You have to do something you never done"

So narud vitani tena 2025 mpaka mwezi kama huu panapo majaaliwa Mungu akitupatia uzima nitakuja kutoa feedback ya maendeleo yangu.
 
Trading ni biashara kama biashara zingine ila upekee wa Forex ni psychology based business ila kila kitu ni the same. Ukiingia kichwa kichwa lazima uje kuwaambia watu ni scam ila kumbe scammer ni wewe mwenyewe.

Binafsi sijajenga Wala gari ninayotumia sijanunua kwa hela ya forec ila home familia inaishi kwa forex no stress kabisa it's just about time kufanya makubwa zaidi. Kama wewe ni trader unaeanza usikatishwe tamaa na yeyote pambania unachoamini.
 
Mimi na miaka 14 kwenye soko la forex ila sio mafanikio ya haraka watu wanavofikilia.nimeona malalamiko mengi hapa JF bora kueleza ukweli.

Asilimia kubwa forex ni High risk na inaweza kukuweka maskini kwa sekunde tu. Sababu kubwa kinacho changia ni watu kutokuelewa na kuwa na haraka ya mafanikio wakiona ushawishi wa mitandao ya kijamii yale mafanikio wanayo onyeshwa bila kujua uhalisia wa watu.

Ogopa sana mtu anayekwambia kafanikiwa kwenye forex alafu huyo hyo anataka kuwafundisha au kuwa tradia mkiipa pesa zenu. Watu hawa asilimia kubwa wametrade na kupoteza pesa nyingi na kuanza kutafuta kwa njia nyengine ili kupata kipato.

wanaongia kwenye forex wengi ni betting jackpot bila kujua risk management. Ili jambo linawakuta sana wanaoingia kwenye forex sababu ya kuaminishwa na matamanio wanayoelezwa kuwa utatoboa haraka.

Ukweli forex ni utapeli uliochangamka kwa wasiojua biashara hii ilivyo sababu imebebwa na tamaa za watu kutaka mafanikio. Kwa nini forex ni utapeli uliochangamka? Biashara ya forex imegeuka kuwa utapeli sababu hakuna mwenye uhakika na soko kama neno lake lilivyo Foreign exchange.

Sababu ni hipi kuonekana kuwa ni utapeli?
  • Wengi wetu sio wasomaji wa vitabu vinavyo husiana na elimu hii wanataka kufundishwa leo kesho yupo sokoni.
  • Waaminishaji na wahamasishaji ni wengi pale wanapokuonesha mafanikio yao ila hasara kuoneshwa ni ngumu.
  • Usiri wa mafanikio ya forex ni mkubwa sana kwa wachache ila ni wengi waliofeli kwenye mafanikio.
  • Mabroker wengi wamekuwa matapeli sababu hawa wapeleki sokoni hapa unatakiwa kujua ni broker gani kwako.
  • Kujiona muelewa ndani ya mda mfupi bila kutambua soko sio lako na kufeli hapo hapo.
TAHADHARI:
Hakuna chochote duniani utakacho fanya bila kukidadisi mwenyewe usitegemee mtu yoyote kukupa mafanikio sio changamoto utafeli.

Most people lose money in Forex trading, why is this? Actually numbers are following: 70% -75% of people lose money in their first year of trading!

Other 20–25 % lose money in next 5 years! (hapa srJEff ina muhusu)

And only 3–5% of all traders are profitable or not losing money.

Reason why people lose money:
  • Not following money management;
  • Do not know how position sizing works;
  • Do not have trading system;
  • Over trading!
Reason why people lose money:
  • Not following money management;
  • Do not know how position sizing works;
  • Do not have trading system;
  • Over trading!

    sio kwel, ivi vyote ulivotaja vinajulikana na hata ukivifanya you can never be profitable, you may ask why, because you are a retail trader upo chini kwenye rank za traders na kila elimu unaoijua kuhusu trading ni bullshit, have u ever asked yourself wanaopata pesa wanatumia njia gan kutrade na kwann wako tafauti?
 
Reason why people lose money:
  • Not following money management;
  • Do not know how position sizing works;
  • Do not have trading system;
  • Over trading!

    sio kwel, ivi vyote ulivotaja vinajulikana na hata ukivifanya you can never be profitable, you may ask why, because you are a retail trader upo chini kwenye rank za traders na kila elimu unaoijua kuhusu trading ni bullshit, have u ever asked yourself wanaopata pesa wanatumia njia gan kutrade na kwann wako tafauti?
Mkuu unainanga sana forex trading, wakati huo unajiita stakehigh unabet?
 
Mkuu unainanga sana forex trading, wakati huo unajiita stakehigh unabet?
issue ni forex ipo ila ya mt4 sio forex, i am trying kusaidia watu waelewe izo tafauti kwa sababu kuna gap kubwa sana katii ya mt4 forex na forex yenyewe na hilo gap watu hawalielewi
 
issue ni forex ipo ila ya mt4 sio forex, i am trying kusaidia watu waelewe izo tafauti kwa sababu kuna gap kubwa sana katii ya mt4 forex na forex yenyewe na hilo gap watu hawalielewi
Bro nimekua nikiona kwenye "threads" watu wakipost kupata hela kupitia forex trading je ni uongo? Na je hamna namna mtu wa kawaida akapata pesa kupitia forex trading ikiwa Wamefanya training na kujua baadhi ya training skills?
 
Back
Top Bottom