F1 Beginner Class
1. Race za Formula 1 ni siku tatu (3), Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
2. Ijumaa ni siku ya practice. Unatest gari na kuijua track. Inaitwa Free Practice Sessions.
3. Jumamosi ni siku ya Qualifying. Hii ndio tunatafuta nani akae mbele, nani afuate, nani awe wa mwisho siku ya race. Qualifying imegawanywa sehemu tatu (3), Q1, Q2 na Q3.
Kinachofanyika una dereva una race Q1 tuna count muda, then watano wa mwisho wanatolewa. Yaani nafasi ya 16 hadi ya 20.
Tunakuja Q2 tena tuna watoa watano kuanzia wa 11 hadi wa 15.
Hafu tunakuja Q3 ambapo tunapata position ya 1 hadi ya 10.
Kwahiyo tunakua tumepata grid ambayo tutaitumia siku ya jumapili, kwamba namba moja hadi namba 20 tunavoanza race wanakaaje.
4. Jumapili ni race day. Hapa ndio tunapata point. Nafasi ya 1 hadi ya 3 ndio wanapanda podium mwisho wa race. Ila nafasi ya 1 hadi ya 10 ndio wanapata point, wengine kuanzia 11 hadi 20 hawapati kitu.
5. Kuna point za dereva na Manufacturer. Ila wengi humu ni fans wa madereva sio manufacturer. Mfano unakuta mtu fan wa Max ila anawakubali Ferrari, so kibishi anabaki kwa Max.