Formula 1® Grand Prix special thread

Formula 1® Grand Prix special thread

Swali

Kama Bugatti Chiron ina top speed ya 489 km/h na 0-100 km/h in 2.2 sec, je inaweza ingia ligi kwenye race track na F1 car?
 
F1 Beginner Class

1. Race za Formula 1 ni siku tatu (3), Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

2. Ijumaa ni siku ya practice. Unatest gari na kuijua track. Inaitwa Free Practice Sessions.

3. Jumamosi ni siku ya Qualifying. Hii ndio tunatafuta nani akae mbele, nani afuate, nani awe wa mwisho siku ya race. Qualifying imegawanywa sehemu tatu (3), Q1, Q2 na Q3.

Kinachofanyika una dereva una race Q1 tuna count muda, then watano wa mwisho wanatolewa. Yaani nafasi ya 16 hadi ya 20.

Tunakuja Q2 tena tuna watoa watano kuanzia wa 11 hadi wa 15.

Hafu tunakuja Q3 ambapo tunapata position ya 1 hadi ya 10.

Kwahiyo tunakua tumepata grid ambayo tutaitumia siku ya jumapili, kwamba namba moja hadi namba 20 tunavoanza race wanakaaje.

4. Jumapili ni race day. Hapa ndio tunapata point. Nafasi ya 1 hadi ya 3 ndio wanapanda podium mwisho wa race. Ila nafasi ya 1 hadi ya 10 ndio wanapata point, wengine kuanzia 11 hadi 20 hawapati kitu.

5. Kuna point za dereva na Manufacturer. Ila wengi humu ni fans wa madereva sio manufacturer. Mfano unakuta mtu fan wa Max ila anawakubali Ferrari, so kibishi anabaki kwa Max.
 
Endelea kwa kuelezea mgawanyo points... Toka mshindi hadi nafasi ya kumi.,
 
Ukiondoa thread ya Arsenal, threads nyingine kongwe hapa JF ukumbi wa michezo ni

  1. MotoGP ,WRC, Superbikes and other Motorsports. Ilianza 2008.
  2. Dakar Rally. Ilianza 2008
 
Endelea kwa kuelezea mgawanyo points... Toka mshindi hadi nafasi ya kumi.,
Mshindi wa kwanza anapata 25 points, wa pili 18, wa tatu 15, kisha wa nne hadi wa kumi wanapata 12, 10, 8, 6, 4, 2, 1 na 1.

Point 1 ya ziada atapewa dereva mwenye fastest lap (yaani aliekimbiza mzunguko mmoja fast kuliko yote). Lakini lazima uyo dereva awe alimaliza top tena. Wazee wa MB na Ferrari mambo yenu aya.

Kwahiyo point mnazikusanya kwenye kila GP na mwishoni mwenye point nyingi ndio mshindi, hapa kama kwenye Premier League za Football.
 
1. Tyre za gari za F1 sio tu zinapata joto, ila zinakua za moto hadi kufikia boiling point of water (100°C), wakati brake zenyewe uwa zinafika joto la 900°C.
 
Nadhani haiwezi ingia sababu ya safety. Chiron ikipinduka hata mara moja paa lake linakugandamiza wakati teknolojia ya Halo inayotumika F1 racing car inaweza binuka mara kumi na mtu akatoka bila mkwaruzo
Swali

Kama Bugatti Chiron ina top speed ya 489 km/h na 0-100 km/h in 2.2 sec, je inaweza ingia ligi kwenye race track na F1 car?
 
Hivi Kenya na Zanzibar iliishia wapi kuja kuhost F1?

1000129690.jpg
 
Back
Top Bottom