Bottas kachukuliwa awe namba 2 pale tu ikitokea Hamilton ana tatizo yeye anatakiwa azibe pengo.F1 ukiwa na jogoo wawili kwenye tundu moja inakuwa ngumu kuwadhibiti angalia 2014 na 2016 Nico Rosberg na Lewis Hamilton walikuwa wao magari yao yapo fiti zaidi ya wengine ila walikuwa wanatupana nje kama kule hispania round ya 1 waligongana wenyewe wakatoka nje haikuishia hapo kule austria na uhasama ulianzia kule Spa Francorchamps,Rosberg alimgonga mwenzake.na ndivyo ilivyo F1 toka kina Ayrton Senna na Alan Prost.Ferrari hili hawalitaki ndiyo maana wana dereva namba 1 na 2 dereva namba 2 kazi yake ni kumlinda namba 1 tu anatakiwa achukue kazi ya dereva namba 1 pale likimtokea tatizo dereva mwenzake namba 1. Kama hawa madereva wawili yaani 1 na 2 wote wawe huru lazima ugomvi utakuwepo sana.kama mwaka jana ukiangalia Force India kati ya sergio Perese na Esteban Ocon walikuwa wanapambana wenyewe kwa wenyewe mpaka walikuwa wanagongana.mpaka team principal anashindwa kuwapa muongozo nani ampishe mwenzake ndiyo huwa inatokea lile munapambana ndugu kwa ndugu.