bubbs
JF-Expert Member
- Feb 2, 2013
- 361
- 178
sasa "bwana mdogo" halafu ni bint tena?
me mwenyewe nilifikiri anaongelea mvulana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa "bwana mdogo" halafu ni bint tena?
mh. My heart was racing reading all this.
Sasa hii story ya uhuru na mwenge imebaki tu kuwa oral tradition? Au kuna sehemu tunaweza kwenda kusoma?
Kunamtu kasema tukiuliza historians wa bagamoyo we can get the info. Sasa hii iko written kama other events ama yenyewe imebaki vinywani tu?
Twambieni nasi tujue kumbe nchi inashikiliwa na mashetani/miungu!! Nasikiaga hawa wazee wa Dar wanaomshauri rais, nilikuwa najiuliza kwanini wote waislamu! And i was wondering 'wazee wa Dar? Seriously? Badala yakutafuta educated people huko juu. Lol. Au ndo wana ''hekima''
sina amani!! Najuta kufungua thread.
Ngoja na mimi nitohoe thiridi hapa hapa " NINI HASA MAANA YA YA MWENGE WA HURU NA HISTORIA YAKE INI IPI HASA KWA USHAHIDI ULIJITOSHELEZA?"
SAMAHANI, I DONT MEAN TO CAUSE HARM, naombeni kuuliza, waarabu walipokuja watakuwa walikuja na mashetani yao eh?
Au uchawi in these lands of ours have always been there hata kabla ya waarabu?
Watu wakiongelea a 'typical african', anaongelea mtu anayeabudu miti, mawe,milima, jua. Sijawahi kusikia habari ya mapepo, wala ufanyaji miujiza.
ENLIGHTEN MEE, OOHH U ENLIGHTENED ONES
Hii mienge hii ni ya kutilia shaka sana, huwa sipati ina maana gani! Maana hata huku Netherlands kuna jengo la chuo linaitwa Aula(Wageningen University) wanalitumia kwa ajili ya mahafali ya PhD na mbele ya hili jengo kuna mwenge unawaka kila siku na wakati wa kuingia wanabeba kitu kama siwa lile la bungeni... Yaani ni full of mysteries tunaishi na kufanya vitu tusivyovijua wala kuhoji mwanzo wake. Hatari sana
Samahani kwa kwenda off topic kidogo. Ila mimi huwa nina amini kuwa kukosa "mawendeleo" kwetu wa Afrika kunatokana sana na kukana Mungu/miungu wetu na kupapatikia ya wenzetu.
Nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea kwa kasi zina Miungu yao. Angalia, Americans, Europeans, Arabs, Chinese and Indians wote wana Miungu yao na wameendelea kuliko Wa Africa na wa Latino ambao kwa aslimia kubwa wameiga Miungu ya wenzao!
Turudi kwenye topic ya Mwenge! Japo sijawahi shiriki maandamano pia sijawahi tafakari sana undani wake. Hoja humu za leo zimenifanya nipate hamu ya kujua zaidi! JF 4 life. Ndio mana niko since 2006!
Mkuu Kuberwa,
Baba Monaa nakusalimia !
Huyu kweli bwana Forojo amesahaulika maana ukiingia google unaikuta hii habariDaa! Amazing! Kwanini mwananthropolojia na NSWECKY Msikae chini na kutunga/kuandika kitabu ambacho mnaweza kukipa jina la HISTORIA ILIYO SAHAULIKA au jina jingine lolote lile? Binafsi nimependa masimulizi yenu ingawaje yanahitaji ushahidi kidogo. Nawasilisha
yeah..lol
like call yourself boobs lol
we umeliona hilo la stress tu mkuu!!ni zaidi ya hilo!jf ni pahala pa kupunguza stress..
unavyosema ni kweli haya matukio yapo orally hayajaandikwa bado,na mtu ambaye angekua ametufanyia haki kuiandika hii historia ni mwl .Nyerere kwan alishiriki katika mambo yote na alikua pia ni mwandishi wa vitabu sasa sielewi kwa nini hakutaka kuandika historia iliyotokea na hakuwahi kuandika harakati zake hata mpaka anakufa?
na alikua mwazi kuyasema hadharani,jaribu kufuatilia hotuba zake anasimulia kuhusu mambo aliyofanya wakati wa kuusaka uhuru
kuhusu wazee wa dar kumshauri raisi ni kitu cha kawaida tu kama wazee wenye busara na wanaoijua hii nchi kwani dar ndio kitovu cha harakat zote za uhuru ulipoanzia na kusambazwa mikoani halaf ukarudi tena dar na wanachomshauri siomambo ya economics of country kwani raisi ana washauri wake kwa mambo hayo
tafsiri unavyotaka kama nchi imekabidhiwa mashetan au mungu, ila kwa wazawa wa kweli na wenye kuujua utanzania na uafrika na watanzania wakweli kutoka rohoni na wanaoheshimu mababu zetu waliotuleta hapa dunian,wakatulisha,wakatuvisha wakatulinda na hatari zote kupitia kumuomba huyo mungu ambae watu wanasema ni shetani na kufanikiwa kuhimili maisha kwa kuomba kwa mungu ambaye alikua anatuletea mvua,anatuonesha siri zilizofichika machon,anatufunulia tiba za magonjwa mbalimbali kupitia njozi au njia zingine mpaka ukawepo leo hii. tunasema nchi imekabidhiwa kwa mungu wetu na sio mungu wa kigeni ambae babu zetu hata hawakumjua na aliyekuja akatupeleka utumwani,akatugeuza makoloni yake, huyo kwetu sio mungu ni shetani
na kuna maeneo matakatifu ndani ya hii nchi ambamo tunaenda kusali na tunafanikiwa
hujawahi kujiuliza kwanini viongozi wanakimbilia mlingotin
tafakari na uikimbie mental slavery
hivi huu mwenge huwa unaenda na zanzibar au wao wanao wao!!
suala la wao kuja na mambo yao ni kama wazungu walivyokuja na mambo yao
na sio kweli kwamba waafrika tulikua tunaabudu jiwe au miti bali tunaamini kuna maeneo ambapo nguvu za mungu ni kubwa zaidi kuliko maeneo mengine ni sawasawa na kusema
waislamu wanaabudu jiwe lile la makka?
jews wanaamin mlima wa sinai au hekalu la sulemani ndio mungu ?
wakristo wanaamin ule msalaba wa yesu ambao upo makanisani ndio mungu?
je wao wanaamini ndio mungu yao?
sasa mkuu kama ulianzishwa kabla ya Muungano huko zanzibar unaenda kufanya nini!!mwenge upo moja tu Tanzania! na unatembea ndani ya mipaka ya Tanzania nzima
sasa mkuu kama ulianzishwa kabla ya Muungano huko zanzibar unaenda kufanya nini!!
mwananthropolojia amesema una kimbizwa ndani ya mipaka ya tanzania!Hivi unakimbizwaga hadi zenji?