TANZIA Fr. Privatus Karugendo amefariki dunia

Nimesoma makala zako kwenye magazeti mbalimbali tangu ningali kijana mdogo. Sehemu ya uandishi wangu leo ni yale niliyojifunza kwa kusoma maandiko yako. Kudadavua hoja, kutafuta ushahidi (facts &evidence), kufafanua takwimu, kupangilia lugha etc.

Maandiko yako yalinijenga kifikra. Japo kuna baadhi ya mitizamo yako sikukubaliana nayo lakini niliiheshimu. Nakumbuka mgogoro wako na Kanisa mwanzoni mwa miaka ya 2000. Nakumbuka uliposimamishwa kufanya huduma za kitume. Nakumbuka kitabu chako kiitwacho "Wito wangu, Imani yangu" ambacho ulielezea kiini cha mgogoro huo.

Nakumbuka mwaka 2008 ulivuliwa rasmi daraja la upadri baada ya miaka 8 ya kusimamishwa na ukaondoa neno "Padri" mwanzoni mwa jina lako. Nakumbuka miaka 9 baadae (mwaka 2017), Vatican ilikubali ombi lako la kuoa na ukafunga ndoa na mama Rose Birusya. Nakumbuka namna mlivyokua mkipishana mara kwa mara na mdogo wako Prudence Karugendo ambaye amefariki majuzi.

Nakumbuka misimamo yako ya kisiasa na jinsi ulivyosimamia hoja bila kujalisha ni wangapi wanakuunga mkono. Yote kwa yote umepigana vita njema na umeimaliza safari. Kwaheri Padri Privatus Karugendo. Maisha yako ni hadithi yenye kufunza mengi. Until we meet again. Pole nyingi kwa kanisa na familia.!

Malisa GJ
 
RIP big man 🙏 mwendo umeukamilisha, hakika mavumbini sote tutarudi.
 

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampokee katika ufalme!
 
Ni miongoni mwa viongozi wa chache wa dini waliochagua kuendelea kusema kweli na kuikosoa mamlaka wakati Tanzania inapitia kipindi kigumu cha uminywaji wa haki za kiraia, uhuru wa habari na demokrasia.

Pumzika kwa amani Father Karugendo 😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…