Frateli ni nani katika Kanisa Katoliki?

Frateli ni nani katika Kanisa Katoliki?

Hapo kuna watu wawili kwenye nafasi mbili kuna ndugu kiroho na msaidizi wa kiroho.

Ila kwa tamaduni mlizo zoezwa huko makanisani kwa sasa huyo frateli hana nafasi ila utasikia baba, mama wa kiroho kama aliyekusimamia kwenye kipa bora ooh sorry kipaimara au ubatizo.

Shemasi kadharika hiyo mtu mmemfanya ndiye anasimamia wavaa nusu utupu, vibaka, kukusanya mapato ya kanisa nk na ameacha nafasi yake inayotakiwa ya usimamizo kiroho.

Note; hayo ni kwa jinsi nilivyofahamu.
Shwaini
 
Wakuu habari za muda!! Naomba kujua Frateli ni nani katika Kanisa Katoliki na Shemasi ni nani na wana ngazi gani za elimu?
Neno 'Frateli' linalotokana na neno la Kilatini 'Frater' ambalo maana yake ni 'Brother'. Huyu ni mwanafunzi katika Seminari Kuu anayesomea Upadri. 'Shemasi' ni Frateli aliyekaribia kumaliza masomo yake ya Upadri. Masomo ya Seminari Kuu huchukua si chini ya miaka saba. Wote wanaosoma hapo katika ngazi yo yote ile huitwa 'Frateli'. Wakimaliza mafunzo ya Philosophy na Theology wanapandishwa daraja na kuitwa 'Shemasi', ingawa wanabakia kuwa mafrateli. Katika ngazi hii wanaweza kufanya vitu kadhaa ambavyo frateli wa chini yao haruhusiwi; kwa mfano kubatiza, kukominisha, kusoma Injili wakati wa ibaada, kufungisha ndoa; n.k. Frateli anadumu katika daraja la ushemasi kwa kiasi cha miaka miwili, ikiwa ni pamoja na kupangiwa kuwa katika parokia kwa mwaka mzima. Huo mwaka tuufananishe na mwaka wa 'internship' kwa kazi za kiraia. Baada ya kufuzu majaribio hayo ndipo anapewa Upadri.
Huyo Shemasi niliyemuelezea hapo juu ni Shemasi wa muda tu kwani ni Padri mtarajiwa. Kuna mashemasi wa kudumu ambao hawatakuja kuwa Mapadri. Hawa ni raia wa kawaida , wanaweza kuwa na ndoa, wanapitia mafunzo yale yale ya Seminari Kuu na kupewa hilo daraja la Ushemasi. Wanaweza kutimiza yale yale anayofanya shemasi wa Seminari Kuu. Tofauti pekee ni kwamba Shemasi wa Kudumu hatapewa Upadri.
 
Usishadadie usivovijua
Nadhani utakuwa katekista wewe, maana ulivyoreply utadhani umefukuzwa kwenye kigango.

Nilichoandika mpaka mwisho kinajieleza sasa unajaza pumba wakati soya ipo bladfk!.
 
Back
Top Bottom