Unaniuliza swali au unajishangaa?Maana nakumbuka ni wewe uliyekuwa unatetea makande kuliwa na matajiri.
Anyway tusidanganyane lakini mwenye utajiri hawezi kuwaza kula makande bwana eti kwa ajili ya kujibana.
Sikushangai maana ndivyo waswahili tulivyo.
Kama hupendii makande ni wewe na hauko peke yako, na hicho chakula unachoona kwako ni bora sana kuna wengine wanaona ni TAKATAKA.
Nenda Upanga ukaone mboga wanazokula wahindi, check wachina vyakula wanavyokula. Hiyo hakumaanishi hawana pesa.
Chakula ni suala la utamaduni. Mfano; Mjaluo huwezi kumtenganisha na Uji hata kama ni tajiri kama Bakhresa.
Vyakula vingine ni vya kiafrika pure. Huvikuti sehemu nyingine, mfano Ugali, lakini nilienda Bukoba nikakuta mpaka wabibi kwenye maisha yao hawajawahi kula Ugali, wao chakula cha heshima ni ndizi.
Wengi wa wahaya shule za boarding ziliwashinda Kwasababu ya Ugali. Baadaye migomba ilipoanza kupata magonjwa na ndizi kuadimika wakaanza kujifunza kula wali. Lakini kuna watu huwaambii kitu kuhusu wali, hadi wengine wako tayari kufanywa chochote ilimradi wapewe wali.
Sasa hivi bongo tuna hulka ya kuona vyakula kama Biryani ( Indian dishes, Sausages, Burger na Pizza ) kama vyakula bora just out of nowhere just Kwasababu ni vyakula vya wazungu.
Binafsi nimewahi kujaribu kula sausage zikanishinda.
Mimi hata chai ya rangi na majani asubuhi hunipi lakini huku Pwani hata mtu awe tajiri vipi ni kawaida kula chai na chapati usiku.
Kwetu Mara, mtu hata awe tajiri vipi lazima ake ugali wa mhogo nixer mtama ( wengine wanaona uchafu )
Kwahiyo usidharau chakula cha mtu yeyote Kwasababu chakula no completely suala la utamaduni, siyo hali ya kiuchumi.