Fred Ngajiro vs Sheria Ngowi?

Fred Ngajiro vs Sheria Ngowi?

My future generations are busy discussing nonsense staff rather than discussing the current economic status of their country we have a long way to go
Ukisema unaambiwa nenda jukwaa la siasa.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
Sio lazima wala haina afya kujadili mda wote hayo unayodhani ni mambo ya msingi, elewa unashauriwa na matabibu kufanya mazoezi ili kujenga afya nzuri ila sio ndio ufanye mda wote, waache watu warefresh mbongo zao baada ya mikikimikiki ya kutafuta ugali wa familia zao

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ni watanzania wangap wanaweza kununua nguo kwa elfu 50?
Acha nguo zipatikane katika bei ambayo majority wana afford ili kupunguza zile copy mtaani. Maana vita dhidi ya maharamia si ndogo. Ila miongon mwa namna ya kupunguza hao maharamia ni nguo kupatikana katka bei amayo wengi wanaweza ifikia
 
Nakumbuka ushindani WA Jersey alieanzisha ni Simba,
Sa nashangaa saiv hawataki midahalo ya jersey.
Umesema jambo la msingi sana nimetaka kulisema mda mrefu mno kwenye mijadala hii ya jezi. Ni vizuri umewakumbusha wenzio kuwa pioneer wa kuthaminisha jezi ni nani. Hawa waliokuja baadae au tunaweza kuwaita "wakuja" eti ndiyo wanataka kuifundisha Simba kuhusu masuala ya jezi.

Simba siku zote anaonyesha njia halafu wengine wanafuata. Aliyekuzidi amekuzidi tu.
 
Ifike mahali Watanzania tusitake kufananisha utam wa sukari na chumvi wala bei zake

Namaanisha nini?

SHERIA NGOWI anafahamika Kwa kila mtu kuwa ni mbunifu wa mavazi, Yes SHERIA kubuni mavazi ndio maisha yake, hivyo anachokifanya pale Yanga ni kuyaishi maisha yake na kuendeleza kipaji chake.

Wakati huohuo hakuna asiyemjua Fred Ngajiro (Vunjabei), Fred ni mfanyabiashara maarufu wa nguo za bei rahisi. Fred si mbunifu wa mavazi (Hana kipaji hicho ) Fred ni mfanyabiashara anayelenga kupata FAIDA Kwa kuuza nguo za quality ndogo Kwa bei ndogo pia (Kuvunja bei).

MADUKA mengi ya Fred suruali zinapatikana kwa elfu 18 za kitanzania, ni nguo ambazo quality yake ni ndogo na Fred havai hizo.

Haitatokea Abadan Sheria NGOWI akanunua nguo kwenye Maduka ya Fred lakin Fred bila shaka ashavaa sana nguo zilizopita mikonon mwa SHERIA NGOWI (Hii si kwa sababu za kibiashara Bali Ubora).

Imani yangu ni kwamba tegemea kuona Yanga wakiwa na jezi zenye ubora wa juu na bei ya juu ilihali tutegemee kuona Simba wakiwa na jezi zenye ubora mdogo na bei ndogo.

Si sahihi kumshindanisha SHERIA NGOWI na Fred Ngajiro kwenye mambo ya mavazi. SHERIA NGOWI anabuni yeye wakati Fred yupo pale Kama dalali Tu na Hana ajualo kuhusu ubunifu labda UGANGA.
Akitokea wa kukupinga, basi wewe mlete tu kwangu nimcharaze viboko.
 
Umesema jambo la msingi sana nimetaka kulisema mda mrefu mno kwenye mijadala hii ya jezi. Ni vizuri umewakumbusha wenzio kuwa pioneer wa kuthaminisha jezi ni nani. Hawa waliokuja baadae au tunaweza kuwaita "wakuja" eti ndiyo wanataka kuifundisha Simba kuhusu masuala ya jezi.

Simba siku zote anaonyesha njia halafu wengine wanafuata. Aliyekuzidi amekuzidi tu.
Umekurupuka read between the lines
 
Majezi yote ya timu zote mbili, ni makorija yslioshonwa hovyo kienyeji na kubuniwa hobela. Material dhaifu, na maandishi ya maandishi ya wadhamini ambayo ukifua yanafutika. Watu wanaingia mkenge tuu kwa mahaba ya timu kudanganywa jezi ni nzuri. Mbunifu Bora wa jezi za mpira Tanzania ni DISMAS TEN tuu.
 
Back
Top Bottom