Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Msimamo wangu,na haujabadilika bado,kuwa ndani ya CCM hakuna wa kujilabu kuwa ni mpambanaji wa ufisadi,hauwezi kuwa katika kundi la shetani ukabakia kuwa malaika,vitu tofauti,mtu akijiona tu anataka kuwatetea Watanzania wanyonge,masikini,wanaoporwa mali zao na majizi ya chama tawala,hatokubali katu kubakia ndani ya kundi la watu(CCM),lililozaa,kulea na kukuza uhalifu huo.
Nikasema, kuwa hao akina Mwakyembe,Mama Kilango,S.Malecela,Ole Sendeka n.k wanaodaiwa kuwa ni makamanda wa vita zidi ya ufisadi,ni wapigaji zogo...mashetani katika kundi lao wakijifanya malaika....mpiganaji wa ufisadi hataweza kukaa CCM hata dakika moja...Mh.Fred Mpendazoe...ni mfano wao...na wangine wanaoumwa kweli,si bla bla bal...waige mfano wake.
 
Kidatu.. hata wakitoka wengine hakuna mtu ataamini watatafuta mambo mepesi mepesi ya kuelezea. Unadhani hata akitoka Kikwete CCM watu wataamini? HIvi akitoka Sitta unajua watu watasema nini? Katika hili hali imekuwa ni "damned if you do and damned if you don't"..

Mkuu,
Kila kitu kina mwanzo. Kumekuwa na tetesi kila kona za mwanzo wa mwisho wa CCM tokana na vitendo vyao vichafu wanavyovifanya na watanzania wameichoka CCM. Kuondoka CCM kwa Mbunge huyu ni ushindi kwa wananchi wanaopingana na ufisadi. Wakiondoka wabunge wengine ambao walikuwa wakipiga kelele pamoja na Mpendazoe utakuwa ni ushindi mkubwa sana kwa taifa na bila shaka utakuwa ndiyo mwanzo wa mwisho wa CCM.
 
Hii ni good move ndio maan leo nikabadili na avator yangu kabisa
niliona mambo mazuri kwenye ulimwengu wa roho
 
Nikasema, kuwa hao akina Mwakyembe,Mama Kilango,S.Malecela,Ole Sendeka n.k wanaodaiwa kuwa ni makamanda wa vita zidi ya ufisadi,ni wapigaji zogo...mashetani katika kundi lao wakijifanya malaika.....

- Kwa mantiki hii sisi wananchi wote wa hili taifa ni mashetani, maana viongozi mashetani hawachaguliwi na wananchi malaika, ni kweli Mpendazoe amekimbia uozo au amekimbia kabla ya kufukuzwa? Wapiganaji wakitoka CCM utakua ndio mwanzo na mwisho wa hili taifa, siliafiki hilo wazo wapiganaji ni lazima wabaki CCM unless otherwise!

- Ninaheshimu sana maneno mazito sana aliyoyasema kwenye mkutano wake na waandishi leo, lakini kwamba ni mfano wa kuigwa hapo bado nina wasi wasi maana huku pembeni nimeshaanza kusikia mengi sana kuhusiana na kukimbia kwake mapema kabla ya NEC next week ingawa pia inaeleweka the desparation ambayo inatupeleka wengine kufikia kufurahia anything!

Respect.

FMEs!
 
Mkuu,inaposemwa kuwa kuna kundi ndani ya CCM "linalojipambanua kupinga ufisadi",hoja inakuja hapa,kwanini wabaki kuwa kundi wakati chama kina itikadi moja?
Kwanini wakati hawaridhiki na hali inayoendelea ndani ya chama wasitoke huko wakajitenga nacho badala yake wamejifanya kuwa kundi ambalo haliishi kuwekewa vikao visivyo na ajenda za maana na tume za kutukanana matusi?
Ndiyo maana jungu alilopika katibu Makamba na wenzake kutaka kujenga uadui na hilo kundi linaloitwa "wapambanaji",linaleta athari zake sasa kwa maana ya ile hoja ya kuwa "mpambanaji" hutafuta kundi sahihi la kupambana,habaki katika kundi la maadui analopambana nalo, kwahiyo hapa ni sahihi kabisa kwa Mpendazoe kuwa mfano halisi wa hali niliyoielezea, natamani watu wanaoonekana majasiri kama ,Dr.Mwakyembe, Ole Sendeka, Selelii,Mama Kilango n.k kesho nao tukawasikia wanajiunga na wananchi masikini,wanyonge wa Tanzania,kwa kutoka huko walikojiweka katika "kundi la wapambani" ambalo halitakiwi kuwapo kabisa.
On hearsay,au za pembeni ulizosikia, mimi sizi entertain kwa kuwa CCM majungu na umbeya ndo kazi yao,kila anayesema ukweli na kuusimamia anakuwa adui...anatengezewa vikao vya kufukuzwa...Mkuu, ukweli ukidhihiri tukubali kuwa uongo hauna cha kusubiri tena...CCM wamekanyaga sipo...kazi kwao,wache waendekeze utabiri,nyumba inaungua..!
 
Kama ni kweli, basi wapo wengi vigogo wa CCM wenye hisa huko CCJ. Na huyu ameanza tu. Ila siamini kama kweli ameamua kuukacha ubunge, na kukimbilia CCJ. Sidhani kama ameamua kwa dhati akose haya marupurupu ya miezi hii michache iliyobaki. Kwanini asingehama baada ya bunge kuvunjwa?
Everything need preparation and clear focused arrangements, siyo kukurupuka tu kama unavyo dhani wewe. Angehama tu Bunge lilipovunjwa ulikuwa unaujua ni nini mustakabali wa CCJ kwa wakati huo? Je Ulikuwa unajua majukumu yake ya Kichama kwa wakati huo? Nadhani huu kwake ameona ndio wakati muafaka, mengine let us wait and see.
 
Mkuu,inaposemwa kuwa kuna kundi ndani ya CCM "linalojipambanua kupinga ufisadi",hoja inakuja hapa,kwanini wabaki kuwa kundi wakati chama kina itikadi moja?
Kwanini wakati hawaridhiki na hali inayoendelea ndani ya chama wasitoke huko wakajitenga nacho badala yake wamejifanya kuwa kundi ambalo haliishi kuwekewa vikao visivyo na ajenda za maana na tume za kutukanana matusi?

- Siasa sometimes ni kama sheria inajali sana historia, tumejionea siasa za mataifa mengi duniani ambayo tunajaribu sana kuwaiga demokrasia wakiwa na makundi makubwa ndani ya chama, na infact pamoja na maana zingine nyingi demokraisa ni kupingana two advesarial sides na kuishia kupata msimamo mmoja hoja kwamba wapambanaji ni lazima wajitoe CCM ili kuwa for real ni hoja finyu sana kwa maendeleo ya taifa ingawa inaweza kua hoja njema kwa a small picture, it takes a lot kujitoa na kuendelea kuwa effective hasa kwa mazingara ya siasa za taifa letu ambapo Rais ni almost a king, wapiganaji kujitoa it not the right time sasa hivi unless katiba imebadilishwa na kumpunguzi madaraka Rais.

Ndiyo maana jungu alilopika katibu Makamba na wenzake kutaka kujenga uadui na hilo kundi linaloitwa "wapambanaji",linaleta athari zake sasa kwa maana ya ile hoja ya kuwa "mpambanaji" hutafuta kundi sahihi la kupambana,habaki katika kundi la maadui analopambana nalo, kwahiyo hapa ni sahihi kabisa kwa Mpendazoe kuwa mfano halisi wa hali niliyoielezea, natamani watu wanaoonekana majasiri kama ,Dr.Mwakyembe, Ole Sendeka, Selelii,Mama Kilango n.k kesho nao tukawasikia wanajiunga na wananchi masikini,wanyonge wa Tanzania,kwa kutoka huko walikojiweka katika "kundi la wapambani" ambalo halitakiwi kuwapo kabisa.
On hearsay,au za pembeni ulizosikia, mimi sizi entertain kwa kuwa CCM majungu na umbeya ndo kazi yao,kila anayesema ukweli na kuusimamia anakuwa adui...anatengezewa vikao vya kufukuzwa...Mkuu, ukweli ukidhihiri tukubali kuwa uongo hauna cha kusubiri tena...CCM wamekanyaga sipo...kazi kwao,wache waendekeze utabiri,nyumba inaungua..!

- Hapo kuna siasa za JF na hali halisi nyumbani, maneno mengi unayoyasema ni good for JF lakini wananchi nyumbani wanaelewa nguvu ya wapiganaji, Mpendazoe amesema maneno mazito sana, lakini kwamba he is a hero tayari hapana siasa does not work that way, bado all the facts kutoka as of why ametoka, ingawa bado alichokifanya ni good thing lakini siwezi ku-support viongozi kujitoa tu bila mpango, at this point and time mafisadi watakwua na furaha sana kuona wapiganaji wakijitoa CCM, maana sasa watakua na everything on their hands!

- Saisa sometimes inaweza kuwa speculations na hearsays pia, especially kwa taifa kama letu ambalo kila habari ni siri, habari za Mpendazoe na CCJ zilikuwepo huko pembeni sio kwamba ni mpya, ndio maana ninasema mimi binafsi ninajaribu kuwa careful na hukumu yoyote kuhusiana na kutoka kwake, ingawa bado ninaheshimu sana maneno aliyoyasema kwenye mkutano wake, yes CCM wanahitaji kusikia that kind of maneno, otherwise inanishngaza sana kuwashupalia wapiganaji 11 katika taifa la wananchi Millioni 45 kwamba ndio respeonsible na misery ya hili taifa kiuongozi, binafsi ninawa-support wapiganaji kwa sababu wamekua more effective kuliko hata wapinzani combined no wonder tunawalaumu sana maana tumesahau hata kama tunao wapinzani, ambao ndio hasa responsibility yao kuleta upinzani kwa CCM.

- Tufike mahalai wananchi wote wa hili taifa tubebe responsibility ya kujinasua badala ya kufikiria kwamba ni tatizo la wapiganaji 11 tu, they are doing their best, siamini kwamba wananchi wengi sana waliojitokeza kumpokea Sendekea majuzi na kumchangia Shillingi Millioni 13 within some few hours ni wajinga wasioelewa kinachoendelea na taifa letuna wapiganaji, ingawa sisi the so called Great Thinkers inaonekana bado hatuelewi hali halisi ya ground zero, lakini hawa Wamasai wanaelewa kilichomfanya Sendeka kushitakiwa kuliko sisi the so called the over-exposed! you wonder who is really exposed kati yetu na hawa Wamasai huko kijijini!

Respect.

FMEs!
 
kweli ukipenda hata chongo utaita kengeza............... the same mrema (or a number of mremas) is (are) back.................. mi nadhani hata mrema alikuwa na hekima kidogo, alijiunga na chama ambacho kiko hai, saasa huyu anajiunga na mimba ya chama!!!!!!!!!!! chama kisipozaliwa? au kiizaliwa njiti?.......... mbona mmeirahisishia kazi CCM, ikiona tishio lolote inacheza na wakunga tu, wakati wa ku-deliver wananjyonga katoto kwisha kazi............ hahah..... hizi domokrasia very funy................
hahahahaha Mkuu you made my night kweli kweli.
Ila bado nasisitiza kwamba yeyote aliyepitia malezi ya CCM hawezi kwa dhati kabisa tena kwa nadhiri moyoni kuwa mpinzani wa kweli. Unajua kwa nini?? Muulize Mwanakijiji
- Kwa mantiki hii sisi wananchi wote wa hili taifa ni mashetani, maana viongozi mashetani hawachaguliwi na wananchi malaika, ni kweli Mpendazoe amekimbia uozo au amekimbia kabla ya kufukuzwa? Wapiganaji wakitoka CCM utakua ndio mwanzo na mwisho wa hili taifa, siliafiki hilo wazo wapiganaji ni lazima wabaki CCM unless otherwise!

- Ninaheshimu sana maneno mazito sana aliyoyasema kwenye mkutano wake na waandishi leo, lakini kwamba ni mfano wa kuigwa hapo bado nina wasi wasi maana huku pembeni nimeshaanza kusikia mengi sana kuhusiana na kukimbia kwake mapema kabla ya NEC next week ingawa pia inaeleweka the desparation ambayo inatupeleka wengine kufikia kufurahia anything!

Respect.

FMEs!
Mheshimiwa sana FMEs!
Heshima mbele Kaasisi wetu, ukisoma hapo kwenye bold ninadhani kuna siri fulani unaifehemu kuhusu mwenendo wa hivi karibuni wa chama chetu. Je kile kikao cha dharura kilikuwa ni maksudically kuwaNAIL some pipo? and there is more victims on track ambao halmashauri kuu itawaweka ktk kikaango au kuwatimua? Nitoe kizani maana sentesi zako zaonesha lipo ujualo
 
Waungwana kama mlivyosikia jana Mbunge Mpendazole kajiunga na CCJ. Sasa ndo kusema mlolongo wa wana CCM kujitoa ndo umeanza au vipi????? Japo Msekwa katika mahojiano yake na BBC alisema eti ni kama kuchota maji bombani na kumwaga kwenye Mto Ruvu. Ni kweli haya au mwasemaje????
 
Wote waliojaribu kupambana na uozo wakiwa ndani ya CCM walishindwa. Njia iliyobaki ni hii ya kuipasua CCM. Vyombo vya DOLA na hasa TISS wakikaa pembeni wakaangalia masuala ya usalama wa TAIFA na sio wa CCM, tunaweza kupiga hatua.
 
Mpendazoe- Safi
CCJ- Safi
Upinzani- Safi

CCM hawawezi kuzuia nguvu ya mabadiliko, kwa vile ni wao wenyewe waliotuonyesha ni jinsi gani wamechafuka, kinachofuatia ni kuwaepuka. Kutowaunga mkono hao wachafu, waozo, wenye harufu ya kila kisonoko CCM. Vikao watakavyofanya, kamati watakazounda ni kupoteza muda, ngoma ishafika kwetu watanzania halisi na tunajua namna ya kuicheza, kuwapiga bao hawa waganga njaa kwa kutumia chama na serikali.

Je CCM, wanafikiri wananchi hawawezi kuwabaini? Ni kweli CCM imekuwa ni mradi, siyo chama tena, bali mradi unaotumiwa na mabepari wanyama wanaoitafuna Tanzania, mabepari wachafu wanaweka na kuwaunga mkono wanasiasa mchwara, vibaraka, ili wakacheze wimbo unaopigwa na mafisadi , wenye ajenda ya kuwaangamiza watanzania kwa kupora haki ya utajiri asili wa Tanzania.

CCM imepoteza dhamana, sifa, haiwezi kuaminiwa kusimamia utawala wa nchi, kwani uaminifu wa viongozi wa CCM upo kwa mabwana zao mafisadi na si kwa wananchi waliowachagua. Inawezekanaje, jambo lililo wazi mf. mafisadi wakubwa, wala rushwa wanaundiwa kamati ili kuwanusuru na kuwajengea hatma mpya ya kisiasa na kuwaadhibu, kuwatisha wanasiasa wenye muelekeo wa kukemea, kupinga uozo ndani ya serikali na CCM?????

Hatua ya kubadilisha uozo wa Tanzania, inategemea maamuzi tunayofanya mimi na wewe na upande upi tunaouunga mkono na wala siyo CCM

Mimi na mwili, nafsi na roho yangu ninaunga upande wa Mungu, Mungu anasema na watanzania wakatae uozo na kugeuzwa si chochote ndani ya nchi yao wenyewe.

Tuwaunge mkono viongozi na watu wanaosaidia katika harakati za kukomboa utu wa mtanzania, Mpendazoe ni mmojawapo.
 
871288 said:
Hamisi Mgeja, mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga ambako anatokea Mpendazoe, alisema: "Mimi kama mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga, sijastushwa kwa sababu tulitegemea hili jambo mimi na wana-CCM wenzangu kutokana na viashiria vingi.

"Kwa muda mrefu amekuwa mtovu wa nidhamu kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa. Chama kipo imara mkoani Shinyanga na kina hazina kubwa. Nawaonea huruma wananchi wa jimbo la Kishapu kwa kukosa mbunge hasa katika kipindi hiki cha Bunge la bajeti."

Mwenyekiti huyo alisema kuwa anaona uamuzi wa Mpendazoe kama safari ya mamba ambayo hujumuisha kenge na kwamba moto aliouanzisha mbunge huyo wa Kishapu ni wa mabua.

Mbunge wa Maswa, John Shibuda, ambaye ametangaza kuwa atapambana na Rais Jakaya Kikwete kuwania urais kwa tiketi ya CCM, alimpongeza Mpendazo kwa uamuzi wake, akisema kuwa kuhama chama si kukofishana na serikali.

"Kuhama msikiti au kanisa la eneo moja kwenda kwenda kwenye msikiti au kanisa la eneo jingine si kuhama Uislamu au Ukristo," alisema Shibuda katika ujumbe mfupi alioutuma kwa Mwananchi.

"Kwa kuchukua uamuzi huo, hajadhulumu utiifu wake kwa serikali na wala hajaasi uzalendo wake kwa taifa. Muumini kukosana na askofu au sheikh si kukosana na Bikira Maria au Mtume Muhammad. Njiwa mwerevu huficha bawa lake."

Mhhhhhhhh...Kazi kweli kweli
 
Wanaodhani Mpendazoe kaondoka peke yake naomba waangalie behind the scene wafikirie upya na CCM isipoangalia inaweza kulipoteza jimbo la Kishapu, kwa mwanaCCM makini atasikitika kumpoteza Mpendazoe wasio makini ndio wanaosema bora kaondoka yaani wale wa type ya sizitaki mbichi hizi

Matokeo ya Ubunge Jimbo la Kishapu 2005
CCM
FRED MPENDAZOE TUNGU kura 64,109 sawa na 81.9%
CUF
JUMA MUSSA SHAMTE kura 6,783 sawa na 8.7%
CHADEMA
MAGEMBE KANOGU PAULO kura 6,689 sawa na 8.5%
TLP
SEIF HAMOUD MASELE kura 659 sawa na 0.8%
Una uhakika gani kuwa hizi zilikuwa kura za Mpendazoe na si za CCM? Unadhani akiwa nje ya CCM bado atazipata hizi kura? Toa sababu.
 
1+1==2 basic maths

2+2 =4 basic maths

2+2 = 5 synergy

1+1 = 1 Christian Marriage.

1+ 1million = 4 million politics

Msekwa upo?
 
Jamani Mpendanzole Kishapu anahali mbaya pia alijua sana.
Hana jipya mpeni moyo tu
 
Una uhakika gani kuwa hizi zilikuwa kura za Mpendazoe na si za CCM? Unadhani akiwa nje ya CCM bado atazipata hizi kura? Toa sababu.
Matokeo ya Ubunge Jimbo la Kishapu 2005
CCM
FRED MPENDAZOE TUNGU kura 64,109 sawa na 81.9%
CUF
JUMA MUSSA SHAMTE kura 6,783 sawa na 8.7%
CHADEMA
MAGEMBE KANOGU PAULO kura 6,689 sawa na 8.5%
TLP
SEIF HAMOUD MASELE kura 659 sawa na 0.8%

Mtu B usianze kuchekesha watu wewe unafikiri kura zilikuwa za nani za Juma Shamte wa CUF
 
Jamani Mpendanzole Kishapu anahali mbaya pia alijua sana.
Hana jipya mpeni moyo tu
...nani alikuambia kuwatumikia watu lazima uwe mbunge tu??? zipo kazi nyingine nzuri atafanya kwa dhamira safi bila unafiki!!
 
otherwise inanishngaza sana kuwashupalia wapiganaji 11 katika taifa la wananchi Millioni 45 kwamba ndio respeonsible na misery ya hili taifa kiuongozi, binafsi ninawa-support wapiganaji kwa sababu wamekua more effective kuliko hata wapinzani combined no wonder tunawalaumu sana maana tumesahau hata kama tunao wapinzani, ambao ndio hasa responsibility yao kuleta upinzani kwa CCM
....wamekuwa more effective wapi?? kwenye ccm yao au wapi? acha uongo na cheap spinning, camp ya upinzani(Dk Slaa na wenzake) ndio wamebadilisha siasa za nchi hii kwa sasa hata udhaifu wa serikali kuonekana dhahiri kwenye mambo mengi, au eleza kwa mifano hayo unayodhani na kuamini ndio hali halisi!
 
Msimamo wangu,na haujabadilika bado,kuwa ndani ya CCM hakuna wa kujilabu kuwa ni mpambanaji wa ufisadi,hauwezi kuwa katika kundi la shetani ukabakia kuwa malaika,vitu tofauti,mtu akijiona tu anataka kuwatetea Watanzania wanyonge,masikini,wanaoporwa mali zao na majizi ya chama tawala,hatokubali katu kubakia ndani ya kundi la watu(CCM),lililozaa,kulea na kukuza uhalifu huo.
Nikasema, kuwa hao akina Mwakyembe,Mama Kilango,S.Malecela,Ole Sendeka n.k wanaodaiwa kuwa ni makamanda wa vita zidi ya ufisadi,ni wapigaji zogo...mashetani katika kundi lao wakijifanya malaika....mpiganaji wa ufisadi hataweza kukaa CCM hata dakika moja...Mh.Fred Mpendazoe...ni mfano wao...na wangine wanaoumwa kweli,si bla bla bal...waige mfano wake.

Niulize swali! Kipi kilitangulia kwanza ni CCM yenye alama ya jembe na nyundo (nina uhakika unafahamu maudhui ya hizo alama)
au hili kundi la mafisadi majizi na maporaji (kama ulivyoyaita). The way I understand akina Mwakyembe, Six, Ole, Mama Kilango they are standing for the value of the party! The founding fathers of the party and party's policy stood and as of today stands for saving nation's interest. Although they dress like CCM, walk nad talk likewise, this prooves the old saying "Kwenye msafara wa mamba kenge huwa hawakosi" They are the ones who should leave, because the original CCM wasn't for msafara of Kenges it was for Mambas.
They might not be willing to leave, but with this dwindling public approval and this growing public anger and frustration well, CCM has no choice, they have to ask them out!! It won’t be long before CCM will be history like KANU of baba Moi

REV 13:9 "Aliye na masikio, na asikie

Back
Top Bottom