Fredrick Sumaye: Samia ataongoza nchi mpaka 2030

Fredrick Sumaye: Samia ataongoza nchi mpaka 2030

Hua naogopa sana juu ya mambo yanayo endelea dhidi ya ccm, kuna siku watu watabadilika wataingiwa na roho mbaya ya kutaka kujua hatma ya maisha yao.

Hawa polisi hawatafua dafu, jeshi halitaweza kuwazuia raia walio chafukwa roho.

Haya majamaa ya ccm yatakikana chama chao hadharani. Siku inakuja na itafika tu
Mkuu, amka Sasa, daladala litakupitiliza kituo, naona ndoto imekukolea
 
Kitendawiliii!
Waziri mkuu duni aliyedumu muda mrefuuu...
Tuache kulamba watawala visigino!!!
 
Yote hii ni baada ya Bashiru kuunguruma?
 
Mr ZERO Hadi anamalizia uongozi wake kama MP, hakujua Hasa kwann Tanzania ni maskini.

Yaani hajui chanzo Cha umaskini wa Watanzania.

Ye nani aseme Hadi 2030, huo Si ndo udikteta?

What if Watanzania wakimchagua Rais Kutoka UPINZANI 😠😠😠?
 
Hizi ni salamu kutoka kwa gwiji la Siasa za Tanzania. Ametumikia chama tawala na aliongoza Chadema. Amezitoa salamu wakati Rais Samia Leo hii, akiwa ziara Mkoa wa Manyara.

Anasema kwa tathmini yake, hakuna wa kumuondoa SSH katika nafasi ya urais mpaka 2030.

Huyu ni mtu aliyekaa na akina pipoz, lazima anawajua undani wao, kwamba ni tabula rasa, wanaojenga nyumba kwa tofali za barafu.

Pia anaijua vizuri CCM. Nani wa kumbishia?
Kwani nani kakataa,mbona wanakimbiza vivuli vyao wenyewe??Sisi wananchi hatuna shida na urais hata akiamua kuwa malikia,sisi tunataka matokeo chanya ya urais sio sifa na mapambio wakati wanachi hatuna maji ya kuoga tunanuka vikwapa na tunashinda bila umeme tunalala giza.Kama mtu ni kiongozi lazima ataona aibu hata kuchukua hiyo formu ya urais ila kama mtu ni mtawala au mlamba asali mshipa wa aibu nakuwa hana kuchukua fomu ya urais zaidi atakuwa rais wa masifa basi.
 
Hizi ni salamu kutoka kwa gwiji la Siasa za Tanzania. Ametumikia chama tawala na aliongoza Chadema. Amezitoa salamu wakati Rais Samia Leo hii, akiwa ziara Mkoa wa Manyara.

Anasema kwa tathmini yake, hakuna wa kumuondoa SSH katika nafasi ya urais mpaka 2030.

Huyu ni mtu aliyekaa na akina pipoz, lazima anawajua undani wao, kwamba ni tabula rasa, wanaojenga nyumba kwa tofali za barafu.

Pia anaijua vizuri CCM. Nani wa kumbishia?
Ila pia tukumbuke kuna watu waliwahi kuitwa marofa na mzee Mkapa.R.I.P Mzee wa Rupaso.
 
Ana haki ya kutoa maoni kama Bashiru.

Kampumzike sasa maana hii ni thread ya 40 kwa leo.
 
Back
Top Bottom