Mara zote naitamani Kiss Fm ya 2010 kurudi nyuma
Asubuhi unaanza na John Karani JK na mwanadada fulani simkumbuki. Baada ya hapo ni Kiss Prime Time
The Big Fuse na Captain JML Joachim Munga Luguru (alikua anasema "keep on your inner ear and get terrifying"). Alikua na DJ Jeff Jerry...noma sana
Baadaye hii show alirithiwa na Ezden The Rocker,akaibadili jina na ikaitwa Bongo Collabo Mix Show. Hakuiharibu sana
Saa tano kamili tunapata News from the BBC na show inaendelea mpaka saa sita. Hapo tunapata show ya afternoon mpaka saa nane
Kuanzia saa nane ni Kiss Hot Wire na Dj Chriss...we acha kabisa
Saa kumi ni Kiss Drive. Ilikua na mtangazaji bonge moja la vocalist Dunia nzima Tobby The Splash! Huyu jamaa sijaona mfano wake mpaka sasa.
Show ya Tobby iliisha saa kumi na mbili jioni. Hapo aliingia Dee Seven na African Beat...mitamboni alikuwepo DJ Maliz..kulikua na jingle ya miluzo...fyuu fyuuuuuu...! acha kabisa Mangi. Hii ilikua ndio show pekee ya kiswahili kwa hii redio. Ilisimamisha mitaa yote na daladala zote Dodoma enzi hizo. Mji mzima iliskika sauti moja tu ya Kiss FM
Saa mbili kamili show iliisha. Aliingia mwanamama Sharbano Aboubakar "Sherry" na Kiss Comfort Zone. Ilikua hatari nyingine
Kuazia saa tatu kulikua na habari za BBC na sports kama sikosei. Saa nne kamili alichukua usukani jamaa mmoja mlavidavi aliitwa Gody B The Pilot na show iliitwa Love Zone! Acha kabisa arif...
Weekends waliungana na redio za marekani. Show ya Ryan Seacrest ya American Top 40 ilirushwa Mubashara. Kulikua pia na Weekend Top 30. Jumamosi kulikua na sebene mix za kufa mtu kuanzia saa tisa mchana
Walikua na best DJ's...Dj Maliz,DJ Devi,DJ Jeff Jerry,DJ Chriss na wengine
Kiss FM ilivyoharibika na watangazaji wote kutimkia kusikojulikana basi nilipatwa na msongo wa mawazo!
Aliyeiloga Kiss FM alaaniwe sana! Sasa hivi redio zote zinatengeneza programu sawa tu na Clouds. Hakuna ubunifu wowote utakaomfanya msikilizaji awe na choice ya program za redio tofauti. Program za asubuhi,mchana,jioni na usiku ni zilezile kwa redio zote. Ovyo kabisa!
Fredwaa pale RFA alikua na show ya tofauti sana na ubunifu wa kipekee nje ya huu mfumo wa ki-clouds. Sasa alipoenda clouds pale alikosa kabisa emotional freedom ya kufanya makeke yake! Natamani kumwona jamaa akiwa na show yake mwenyewe kwenye redio kubwa. Energy Man is very talented! Mashabiki wake tutakua naye mpaka mwisho!
Sent using
Jamii Forums mobile app