Freeman Mbowe akiachia Uenyekiti CHADEMA itakufa na kusambaratika ndani ya miezi michache

Freeman Mbowe akiachia Uenyekiti CHADEMA itakufa na kusambaratika ndani ya miezi michache

Leo saa mbovu imesema Kweli.

Mbowe ahakikishe CDM inashika DOLA ndo ang'atuke .

Bt kumbuka pia Uenyekiti CDM Si vita, CHADEMA ni Moja.

Aamen
Chadema na chama chochote kile Cha upinzani hakiwezi kupewa nafasi ya kuongoza nchi hii,Jua liwake mvua inyeshe Hakuna mpinzani wakwenda ikulu. Ikulu no mahali patakatifu siyo mahali ambapo kila mtu anaweza kwenda na kukaa,
 
Siyo kweli Mbowe katengeneza backup mzuri sn, Heche, Mnyika, Sugu, Msigwa, MMM n.k
Awaangalie Sana akina Lema na Lisu ,wale Ni vibaraka wa mabeberu,wapo tayari kuleta na kuchochea hata machafuko maana hawana uchungu na nchi yetu,Namtetea mh Mbowe kwa kuwa yupo Tayari kwa maridhiano
 
Utahangaika sana lakini kamwe hutateuliwa Samia hatoi teuzi za kishamba na hataki kushobokewa
Naona unahangaika Sana na Mimi kuhusu neno Hilo la uteuzi kana kwamba hii Ni barua ya kuomba uteuzi,ungekuwa wewe Ni mgawaa pumzi bila Shaka ungeninyima oksijeni ili nife maana unachuki kubwa Sana na Mimi. Hata hivyo Mimi Sina hasira Wala kinyongo na wewe,Nakuombea Hekima na busara ili upunguze chuki na hasira juu yangu
 
Naona unahangaika Sana na Mimi kuhusu neno Hilo la uteuzi kana kwamba hii Ni barua ya kuomba uteuzi,ungekuwa wewe Ni mgawaa pumzi bila Shaka ungeninyima oksijeni ili nife maana unachuki kubwa Sana na Mimi. Hata hivyo Mimi Sina hasira Wala kinyongo na wewe,Nakuombea Hekima na busara ili upunguze chuki na hasira juu yangu
Safari hii hakuna teuzi za kindezindezi.
 
Mimi Ni CCM na nitaendelea kuwa mwana ccm mwaminifu,Nipo ccm kwa sababu ndio chama chenye Sera na ajenda za kueleweka,Ndio chama chenye Dira na muelekeo unaoeleweka,Ndio chama chenye itikadi inayoeleweka,Ndio chama chenye mfumo imara na madhubuti,Ndio chama chenye safu ya kiuongozi imara na shupavu Hadi ngazi ya mashina,Ndio chama chenye uchungu na maisha ya watanzania,Ndio chama kisicho na ubaguzi,CCM ndio chama ambacho kinatoa nafasi kwa yoyote kutimiza Ndoto zake. Hakika CCM ndio chama kiongozi na Bora kabisa barani Afrika
Ndiyo mnavyokaririshwa huko CCM?
 
Ndugu zangu sote Tunaona na kusikia yanayoendelea huko Chadema ambapo Baadhi ya wafuasi na viongozi wa chadema wakimuona Mwenyekiti wao Kama Msaliti na anayepaswa kuwapisha, leo Baadhi ya viongozi wanamuona Mbowe Kama muda wake umekwisha,amapitwa na wakati ,Anawachelewesha mambo yao, Anawakwamisha.

Leo Kuna wafuasi wa chadema wanajifanya ni makamanda na majasiri kuliko Mbowe,Leo Kuna wafuasi na viongozi wanajionaa kuwa wanapaswa kupewa funguo za chama kuongoza jahazi.

Leo akina Lema na Lissu waliokaribishwa na Mbowe chamani, wakafundishwa siasa halisi za upinzani, wakapewa majukwaa na Mbowe, wakapewa nafasi za kugombea ubunge hadi chamani, wakatambulishwa mbele ya wazee wa chama Sasa wanamuona Mbowe ni msaliti? Kwamba Hawa akina Lema na Lisu Ni wazalendo na wenye uchungu na chama kuliko Mbowe?

Hawa wote wamemkuta Mbowe akihangaika na CHADEMA, akipita huku na kule kusaka vijana wa kujiunga na chama chake. Eamemkuta Mbowe akitumia jasho lake kuijenga CHADEMA, wamemkuta Mbowe akilala nje ya nyumbani kwake kuijenga CHADEMA. ,wamemkuta mbowe akihutubia Hadi Miti lakini hakati Tamaa ya kusonga mbele kukijenga chama chake.

Wamemkuta Mbowe akihangaika kutafuta wafadhiri wakumsaidia chochote ili asafiri hadi vijijini kutafuta wanachama wapya. Hawa akina Lema wameikuta CHADEMA imekua, imeimarika, imekuwa na mtandao wa kiuongozi.

Mbowe ndani ya CHADEMA kuna jasho, damu na machozi yake. Kuna nguvu yake, kuna mikono na alama zake ambazo huwezi kuzifuta. Ndio CHADEMA mwenyewe na CHADEMA ndio yeye. Amelala maporini na kila sehemu ambayo huwezi kujua kama kiongozi mkubwa wa aina yake anaweza kulala. Amekuwa alama ya mabadiliko ndani ya CHADEMA kimfumo na kiutendaji.

Leo Lema ni kama anataka kuongoza kundi la kumuasi na kumpindua Mbowe ndani ya CHADEMA. Anasema hataki maridhiano, anataka chama chake kijitoe ndani ya meza ya mazungumzo. Swali ni kuwa kama hataki maridhiano anataka nini wakati huu ambao Rais wetu mpendwa na kipenzi cha Watanzania Mama Samia smefungua milango ya maridhiano?

Hivi Lema anaweza kushindana na CCM? Anaweza kushindana na serikali ya CCM? Anaweza kushindana na dola? Anaweza kuvuruga amani yetu? Anaweza kuwashawishi Watanzania ujinga wake wakamkubalia? Hakuona Lissu alishindwa kuwashawishi Watanzania waandamane?

Kama ni mwanaume kwa nini anaongelea ugenini? Si srudi na kukaa hapa kama ilivyo kwa Mbowe? Kwanini asije kuongoza mapambano anayoyataka? Anataka wakina nani wapambane kwa niaba yake? Kwanini asije na familia yake huku ndio aongoze na kuwa mstari wa mbele kufanya hayo anayoyataka kimabavu?

Watanzania chini ya mama yetu shupavu Mama Samia tunahitaji amani, tunahitaji umoja wa kitaifa, mshikamano, upendo na kusonga mbele kwa pamoja kama taifa.

Hatutaki majitu ya mioyo ya mavurugu vurugu na mihemuko kama akina Lema, hatutaki ghasia katika taifa letu wala wakutuletea mipasuko. Hatuwezi kumkubalia mtu wa namna hiyo, tutamkabila kama taifa na tutamshinda kama taifa kwa umoja wetu.

Napenda kuwashauri CHADEMA kuwa kama alivyofanya na kutamka Mwenyekiti wenu kuwa hamtajitoa katika maridhiano fanyeni hivyo kwa kuwa CCM ipo tayari na dhamira njema. Muungeni mkono Mwenyekiti wenu kama ambavyo sisi wana CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti wetu.

Nje ya hapo napenda kuwaambieni ukweli kuwa hakuna njia yoyote mtakayoitumia itakayo wasaidieni, maana hamtaambulia kitu, hamtapata kitu, hamtaungwa mkono na Watanzania wala hamtasikilizwa na yoyote mwenye akili timamu.

Kama mkiikimbia meza ya mazungumzo, mliikimbia Bunge la Katiba na bado kama taifa tukasonga na bado tunasonga kwa kasi ya ajabu, hata hapa mkikimbia hamtatutetelesha CCM na wana CCM, maana tunaungwa mkono na Watanzania ambao wameshatambua dhamira njema ya Rais wetu mpendwa Mama Samia.

Narudia Tena mkiikimbia meza ya mazungumzo hakuna wa kuwabembeleza na wala hamtafanya chochote kile kuitikisa serikali yetu na Rais wetu. Nchi yetu na serikali yetu chini ya uongozi wa Mama Samia ni imara sana na ambayo haiwezi kutishiwa na yeyote kwa maneno na hata kwa matendo.

Ambaye haamini maneno haya basi ajaribu kuichezea amani ya nchi yetu hii inayolindwa kwa jasho na damu ili sisi Watanzania tuishi kwa amani na upendo na kufanya shughuli zetu bila wasiwasi wala bughudha.

Polee Sana Mbowe, uliowaamini na kuwakaribisha na kuwakuza sasa wanakuona hufai, sasa wanakuona muoga, sasa wanakuona huna uchungu na chama chako, sasa wanakuona umepitwa na wakati, sasa bila ushahidi wanasema unalamba asali, sasa wanataka kukupindua, wanataka kukutoa kinguvu, sasa wanakuzunguka, sasa wanajiandaa kukuasi na wameshakuasi kimsimamo.

Sasa hakuna uongozi wa kutoa dira na muelekeo, hakuna nidhamu ndani ya chama ndio maana kila mtu anakuja hadharani na kujiropokea anavyojuwa mwenyewe.

Hakika wapinzani mna mengi sana ya kujifunza kutoka CCM, maana mnayoyafanya huko huwezi kuyakuta wala kuyasikia, wala kutokea ndani ya CCM, sisi huku tunaheshimia na kupendana, tunawasikiliza viongozi wetu na kuwaheshimu, tunajuwa msimamo wa chama inatolewa na vikao maalumu baada ya vikao vya kihalali na siyo kwa mtu mmoja kuja kujiropokea hadharani au mitandaoni.

Ikikupendeza karibu sana CCM, mimi nikiwa kama mwanachama mtiifu wa CCm na ninayeendelea kukiunga mkono chama changu na kuipenda serikali yangu ya CCM nakukaribisha sana kwenye chama hiki kisicho na ubaguzi.

Kazi Iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Chama kama hakina mbadala wa tu mwingine kushika uenyekiti ni chama mfu yaani akiondoka mbowe kina kufa? sasa hicho siyo chama ni saccoss ya mbowe ndiyo jina unaweza kusema kwa maana chama ni taasisi siyo mali ya mtu binafsi kwanza ni matusi kusema hakuna mtu mwingine zaidi ya mbowe
 
Leo saa mbovu imesema Kweli.

Mbowe ahakikishe CDM inashika DOLA ndo ang'atuke .

Bt kumbuka pia Uenyekiti CDM Si vita, CHADEMA ni Moja.

Aamen
chama kama hakiwezi kubadirishana uenyekiti huwezi kuita chama ni kikundi tucha wahuni fulani
 
chama kama hakiwezi kubadirishana uenyekiti huwezi kuita chama ni kikundi tucha wahuni fulani
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani kihuni , rejea ushenzi uliofanyika 2019/20 kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani kihuni , rejea ushenzi uliofanyika 2019/20 kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
hivi chadema wakipewa nchi si watakuja kulazimisha kukaa madarakani mpaka dunia iishe ?kama mwenyekiti tu hataki kutoka kuwapisha wengine unakiitaje kuwa chama cha democrasia yaani democrasia inabakwa hadharani na mhuni mmoja tu mbowe ambaye hana dira wala mwelekeo hajulikani kama kaunga juhudi au la?
 
chama kama hakiwezi kubadirishana uenyekiti huwezi kuita chama ni kikundi tucha wahuni fulani
Tuanze kubadilishana DOLA,

Miaka 5 CCM, miaka 5 inayofuata tunakipa CDM au chama kingine Cha upinzani.

Utaratibu huo ni mzuri sana, chama Cha Democratic na Republican wamefanya sana na umeleta tija USA.

Kwann CCM inganganie tangu uhuru?

Huoni ni UHUNI huo ndugu???
 
Tuanze kubadilishana DOLA,

Miaka 5 CCM, miaka 5 inayofuata tunakipa CDM au chama kingine Cha upinzani.

Utaratibu huo ni mzuri sana, chama Cha Democratic na Republican wamefanya sana na umeleta tija USA.

Kwann CCM inganganie tangu uhuru?

Huoni ni UHUNI huo ndugu???
hatuoni jipya kwa chadema maana kama wameshindwa kuwa na democrasia ndani ya chama wataweza kubadirishana nchi? inaonekana hawana hazina ya watu wenye uwezo wa uongozi sasa mnawapa nchi ya nini
 
hatuoni jipya kwa chadema maana kama wameshindwa kuwa na democrasia ndani ya chama wataweza kubadirishana nchi? inaonekana hawana hazina ya watu wenye uwezo wa uongozi sasa mnawapa nchi ya nini
Jibu swali, kwann CCM ikae muda wote pekeake, huoni inatakiwa kubadilishana na vyama vingine?
 
Chadema na chama chochote kile Cha upinzani hakiwezi kupewa nafasi ya kuongoza nchi hii,Jua liwake mvua inyeshe Hakuna mpinzani wakwenda ikulu. Ikulu no mahali patakatifu siyo mahali ambapo kila mtu anaweza kwenda na kukaa,
Ni Kweli IKULU ni Mahali PATAKATIFU, mbona yule Askofu mwingira alimuona SHETANI kwenye nyumba hiyo na CCM ndo chama tawala???
 
Back
Top Bottom