Freeman Mbowe akiachia Uenyekiti CHADEMA itakufa na kusambaratika ndani ya miezi michache

Jibu swali, kwann CCM ikae muda wote pekeake, huoni inatakiwa kubadilishana na vyama vingine?
hakuna chama makini cha kuweza kuchukua nchi zaidi ya ccm chadema wenyewe hawaelewani wenyewe kwa wenyewe sasa muwape nchi ? nchi siyo ya kujaribishana uongzi unatakiwa uwe umeiva kama wana ccm
 
Tusadie chama mbadala ni kipi kama CDM hakijakua Ili tukibadili na CCM?
 
hivi chadema wakipewa nchi si watakuja kulazimisha kukaa madarakani mpaka dunia iishe ?kama mwenyekiti tu hataki kutoka kuwapisha wengine unakiitaje kuwa chama cha democrasia yaani democrasia inabakwa hadharani na mhuni mmoja tu mbowe ambaye hana dira wala mwelekeo hajulikani kama kaunga juhudi au la?
Wewe hata hujui unajadili nini, CCM ndiyo iko madarakani tangu tupate Uhuru na ndiyo hii inatumia mabavu ya vyombo vya dola kubaki madarakani. Watu kibao wameshauliwa katika chaguzi mbali mbali ili CCM iendelee kutawala kibabe.
 
hakuna chama makini cha kuweza kuchukua nchi zaidi ya ccm chadema wenyewe hawaelewani wenyewe kwa wenyewe sasa muwape nchi ? nchi siyo ya kujaribishana uongzi unatakiwa uwe umeiva kama wana ccm
Kama Kweli unaona hakuna mbadala wa CCM huoni ni UDIKTETA huo!!!

Unapata wapi nguvu ya kuunyooshea kidole UENYEKITI wa MBOWE?

Kaa Kwa kutulia!!!

Pia ujue CDM ni MOJA.
 
Ni Kweli IKULU ni Mahali PATAKATIFU, mbona yule Askofu mwingira alimuona SHETANI kwenye nyumba hiyo na CCM ndo chama tawala???
Siyo kila mwenye macho huona kwa hiyo inategemeana ulionaje,Ndio maana Kuna wenye macho lakini hawaoni na Kuna wanao ona lakini hawaelewi.
 
Wewe hata hujui unajadili nini, CCM ndiyo iko madarakani tangu tupate Uhuru na ndiyo hii inatumia mabavu ya vyombo vya dola kubaki madarakani. Watu kibao wameshauliwa katika chaguzi mbali mbali ili CCM iendelee kutawala kibabe.
Watu gani walio uwawa,una ushahidi huo, Mbona wewe huja uwawa wakati kila Siku unafanya kazi ya kutukana mimatusi humu utafikiri umekosa malezi Bora ya wazazi?
 
Wewe unabishana kishabiki oya oya naamua kukupuuza. Wale waliuliwa kule Pemba hadi kwa mara ya kwanza tukazalalisha wakimbizi siyo watu au ulikuwa bado uko kijijini kwenu unakunya porini huko?
 
Jibu swali, kwann CCM ikae muda wote pekeake, huoni inatakiwa kubadilishana na vyama vingine?
CCM ipo madarakani na itaendeleaa kuwepo hapa kwa maelfu ya miaka kwa kuwa Ina Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania wanyonge,kwa kuwa Ina uchungu na maisha ya watanzania,kwa kuwa inawajari na kuwa sikiliza watanzania,kwa kuwa Ina Dira na muelekeo unaoeleweka,kwa kuwa Ina safu ya uongozi inayoeleweka,kwa kuwa CCM imefanya kazi kubwa Sana ya kuleta maendeleo katika Taifa letu katika kila nyanja Tangia tujipatie Uhuru wetu
 
Unajua maana ya DEMOKRASIA?

Marekani Kuna vyama viwili vikuu, DEMOCRATIC party na REPUBLICAN,

Vyama hivi vyote vinawatumikia vizuri wananchi Kila vinapopewa nafasi ya Kutoa RAIS wa kuongoza Nchi.

Wananchi wanavibadili vyama hivi watakavyo.

KWANN CCM isiwe na mbadala?

CCM ni mama etu asiwe na mbadala?
 
Ndugu zangu sote Tunaona na kusikia yanayoendelea huko Chadema ambapo Baadhi ya wafuasi na viongozi wa chadema wakimuona Mwenyekiti wao Kama Msaliti na anayepaswa kuwapisha, leo Baadhi ya viongozi wanamuona Mbowe Kama muda wake umekwisha,amapitwa na wakati ,Anawachelewesha mambo yao, Anawakwamisha.

Leo Kuna wafuasi wa chadema wanajifanya ni makamanda na majasiri kuliko Mbowe,Leo Kuna wafuasi na viongozi wanajionaa kuwa wanapaswa kupewa funguo za chama kuongoza jahazi.

Leo akina Lema na Lissu waliokaribishwa na Mbowe chamani, wakafundishwa siasa halisi za upinzani, wakapewa majukwaa na Mbowe, wakapewa nafasi za kugombea ubunge hadi chamani, wakatambulishwa mbele ya wazee wa chama Sasa wanamuona Mbowe ni msaliti? Kwamba Hawa akina Lema na Lisu Ni wazalendo na wenye uchungu na chama kuliko Mbowe?

Hawa wote wamemkuta Mbowe akihangaika na CHADEMA, akipita huku na kule kusaka vijana wa kujiunga na chama chake. Eamemkuta Mbowe akitumia jasho lake kuijenga CHADEMA, wamemkuta Mbowe akilala nje ya nyumbani kwake kuijenga CHADEMA. ,wamemkuta mbowe akihutubia Hadi Miti lakini hakati Tamaa ya kusonga mbele kukijenga chama chake.

Wamemkuta Mbowe akihangaika kutafuta wafadhiri wakumsaidia chochote ili asafiri hadi vijijini kutafuta wanachama wapya. Hawa akina Lema wameikuta CHADEMA imekua, imeimarika, imekuwa na mtandao wa kiuongozi.

Mbowe ndani ya CHADEMA kuna jasho, damu na machozi yake. Kuna nguvu yake, kuna mikono na alama zake ambazo huwezi kuzifuta. Ndio CHADEMA mwenyewe na CHADEMA ndio yeye. Amelala maporini na kila sehemu ambayo huwezi kujua kama kiongozi mkubwa wa aina yake anaweza kulala. Amekuwa alama ya mabadiliko ndani ya CHADEMA kimfumo na kiutendaji.

Leo Lema ni kama anataka kuongoza kundi la kumuasi na kumpindua Mbowe ndani ya CHADEMA. Anasema hataki maridhiano, anataka chama chake kijitoe ndani ya meza ya mazungumzo. Swali ni kuwa kama hataki maridhiano anataka nini wakati huu ambao Rais wetu mpendwa na kipenzi cha Watanzania Mama Samia smefungua milango ya maridhiano?

Hivi Lema anaweza kushindana na CCM? Anaweza kushindana na serikali ya CCM? Anaweza kushindana na dola? Anaweza kuvuruga amani yetu? Anaweza kuwashawishi Watanzania ujinga wake wakamkubalia? Hakuona Lissu alishindwa kuwashawishi Watanzania waandamane?

Kama ni mwanaume kwa nini anaongelea ugenini? Si srudi na kukaa hapa kama ilivyo kwa Mbowe? Kwanini asije kuongoza mapambano anayoyataka? Anataka wakina nani wapambane kwa niaba yake? Kwanini asije na familia yake huku ndio aongoze na kuwa mstari wa mbele kufanya hayo anayoyataka kimabavu?

Watanzania chini ya mama yetu shupavu Mama Samia tunahitaji amani, tunahitaji umoja wa kitaifa, mshikamano, upendo na kusonga mbele kwa pamoja kama taifa.

Hatutaki majitu ya mioyo ya mavurugu vurugu na mihemuko kama akina Lema, hatutaki ghasia katika taifa letu wala wakutuletea mipasuko. Hatuwezi kumkubalia mtu wa namna hiyo, tutamkabila kama taifa na tutamshinda kama taifa kwa umoja wetu.

Napenda kuwashauri CHADEMA kuwa kama alivyofanya na kutamka Mwenyekiti wenu kuwa hamtajitoa katika maridhiano fanyeni hivyo kwa kuwa CCM ipo tayari na dhamira njema. Muungeni mkono Mwenyekiti wenu kama ambavyo sisi wana CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti wetu.

Nje ya hapo napenda kuwaambieni ukweli kuwa hakuna njia yoyote mtakayoitumia itakayo wasaidieni, maana hamtaambulia kitu, hamtapata kitu, hamtaungwa mkono na Watanzania wala hamtasikilizwa na yoyote mwenye akili timamu.

Kama mkiikimbia meza ya mazungumzo, mliikimbia Bunge la Katiba na bado kama taifa tukasonga na bado tunasonga kwa kasi ya ajabu, hata hapa mkikimbia hamtatutetelesha CCM na wana CCM, maana tunaungwa mkono na Watanzania ambao wameshatambua dhamira njema ya Rais wetu mpendwa Mama Samia.

Narudia Tena mkiikimbia meza ya mazungumzo hakuna wa kuwabembeleza na wala hamtafanya chochote kile kuitikisa serikali yetu na Rais wetu. Nchi yetu na serikali yetu chini ya uongozi wa Mama Samia ni imara sana na ambayo haiwezi kutishiwa na yeyote kwa maneno na hata kwa matendo.

Ambaye haamini maneno haya basi ajaribu kuichezea amani ya nchi yetu hii inayolindwa kwa jasho na damu ili sisi Watanzania tuishi kwa amani na upendo na kufanya shughuli zetu bila wasiwasi wala bughudha.

Polee Sana Mbowe, uliowaamini na kuwakaribisha na kuwakuza sasa wanakuona hufai, sasa wanakuona muoga, sasa wanakuona huna uchungu na chama chako, sasa wanakuona umepitwa na wakati, sasa bila ushahidi wanasema unalamba asali, sasa wanataka kukupindua, wanataka kukutoa kinguvu, sasa wanakuzunguka, sasa wanajiandaa kukuasi na wameshakuasi kimsimamo.

Sasa hakuna uongozi wa kutoa dira na muelekeo, hakuna nidhamu ndani ya chama ndio maana kila mtu anakuja hadharani na kujiropokea anavyojuwa mwenyewe.

Hakika wapinzani mna mengi sana ya kujifunza kutoka CCM, maana mnayoyafanya huko huwezi kuyakuta wala kuyasikia, wala kutokea ndani ya CCM, sisi huku tunaheshimia na kupendana, tunawasikiliza viongozi wetu na kuwaheshimu, tunajuwa msimamo wa chama inatolewa na vikao maalumu baada ya vikao vya kihalali na siyo kwa mtu mmoja kuja kujiropokea hadharani au mitandaoni.

Ikikupendeza karibu sana CCM, mimi nikiwa kama mwanachama mtiifu wa CCm na ninayeendelea kukiunga mkono chama changu na kuipenda serikali yangu ya CCM nakukaribisha sana kwenye chama hiki kisicho na ubaguzi.

Kazi Iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627

Ulikuwepo wakati kaburu ana hama CHADEMA?

Ulikuwepo wakati Zitto anahama CHADEMA?

Ulikuwepo kipindi Dr Slaa anahama CHADEMA?

Nini kilitokea baada ya hao watatu kuhama chama?. Chama kimebaki imara.

CHADEMA Ina watu wengi wakuongoza. Mbowe kaacha vifaa vingi.
1. Lissu
2. Heche
3. Mwalimu
4. Amani Golugwa
5. Dr Albano
6. Msigwa.
7. Lema
8. Mnyika
9. Susan Kiwanga
10. Ruge Catherine, etc

CHADEMA Ni imara Sana hakuna wa kuiangusha zaidi ya Mungu mwenyewe.
 
Awaangalie Sana akina Lema na Lisu ,wale Ni vibaraka wa mabeberu,wapo tayari kuleta na kuchochea hata machafuko maana hawana uchungu na nchi yetu,Namtetea mh Mbowe kwa kuwa yupo Tayari kwa maridhiano
Maridhiano ya kijinga hayana time frame na ni faida kwa CCM
 
Ndugu zangu sote Tunaona na kusikia yanayoendelea huko Chadema ambapo Baadhi ya wafuasi na viongozi wa chadema wakimuona Mwenyekiti wao Kama Msaliti na anayepaswa kuwapisha, leo Baadhi ya viongozi wanamuona Mbowe Kama muda wake umekwisha,amapitwa na wakati ,Anawachelewesha mambo yao, Anawakwamisha.

Leo Kuna wafuasi wa chadema wanajifanya ni makamanda na majasiri kuliko Mbowe,Leo Kuna wafuasi na viongozi wanajionaa kuwa wanapaswa kupewa funguo za chama kuongoza jahazi.

Leo akina Lema na Lissu waliokaribishwa na Mbowe chamani, wakafundishwa siasa halisi za upinzani, wakapewa majukwaa na Mbowe, wakapewa nafasi za kugombea ubunge hadi chamani, wakatambulishwa mbele ya wazee wa chama Sasa wanamuona Mbowe ni msaliti? Kwamba Hawa akina Lema na Lisu Ni wazalendo na wenye uchungu na chama kuliko Mbowe?

Hawa wote wamemkuta Mbowe akihangaika na CHADEMA, akipita huku na kule kusaka vijana wa kujiunga na chama chake. Eamemkuta Mbowe akitumia jasho lake kuijenga CHADEMA, wamemkuta Mbowe akilala nje ya nyumbani kwake kuijenga CHADEMA. ,wamemkuta mbowe akihutubia Hadi Miti lakini hakati Tamaa ya kusonga mbele kukijenga chama chake.

Wamemkuta Mbowe akihangaika kutafuta wafadhiri wakumsaidia chochote ili asafiri hadi vijijini kutafuta wanachama wapya. Hawa akina Lema wameikuta CHADEMA imekua, imeimarika, imekuwa na mtandao wa kiuongozi.

Mbowe ndani ya CHADEMA kuna jasho, damu na machozi yake. Kuna nguvu yake, kuna mikono na alama zake ambazo huwezi kuzifuta. Ndio CHADEMA mwenyewe na CHADEMA ndio yeye. Amelala maporini na kila sehemu ambayo huwezi kujua kama kiongozi mkubwa wa aina yake anaweza kulala. Amekuwa alama ya mabadiliko ndani ya CHADEMA kimfumo na kiutendaji.

Leo Lema ni kama anataka kuongoza kundi la kumuasi na kumpindua Mbowe ndani ya CHADEMA. Anasema hataki maridhiano, anataka chama chake kijitoe ndani ya meza ya mazungumzo. Swali ni kuwa kama hataki maridhiano anataka nini wakati huu ambao Rais wetu mpendwa na kipenzi cha Watanzania Mama Samia smefungua milango ya maridhiano?

Hivi Lema anaweza kushindana na CCM? Anaweza kushindana na serikali ya CCM? Anaweza kushindana na dola? Anaweza kuvuruga amani yetu? Anaweza kuwashawishi Watanzania ujinga wake wakamkubalia? Hakuona Lissu alishindwa kuwashawishi Watanzania waandamane?

Kama ni mwanaume kwa nini anaongelea ugenini? Si srudi na kukaa hapa kama ilivyo kwa Mbowe? Kwanini asije kuongoza mapambano anayoyataka? Anataka wakina nani wapambane kwa niaba yake? Kwanini asije na familia yake huku ndio aongoze na kuwa mstari wa mbele kufanya hayo anayoyataka kimabavu?

Watanzania chini ya mama yetu shupavu Mama Samia tunahitaji amani, tunahitaji umoja wa kitaifa, mshikamano, upendo na kusonga mbele kwa pamoja kama taifa.

Hatutaki majitu ya mioyo ya mavurugu vurugu na mihemuko kama akina Lema, hatutaki ghasia katika taifa letu wala wakutuletea mipasuko. Hatuwezi kumkubalia mtu wa namna hiyo, tutamkabila kama taifa na tutamshinda kama taifa kwa umoja wetu.

Napenda kuwashauri CHADEMA kuwa kama alivyofanya na kutamka Mwenyekiti wenu kuwa hamtajitoa katika maridhiano fanyeni hivyo kwa kuwa CCM ipo tayari na dhamira njema. Muungeni mkono Mwenyekiti wenu kama ambavyo sisi wana CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti wetu.

Nje ya hapo napenda kuwaambieni ukweli kuwa hakuna njia yoyote mtakayoitumia itakayo wasaidieni, maana hamtaambulia kitu, hamtapata kitu, hamtaungwa mkono na Watanzania wala hamtasikilizwa na yoyote mwenye akili timamu.

Kama mkiikimbia meza ya mazungumzo, mliikimbia Bunge la Katiba na bado kama taifa tukasonga na bado tunasonga kwa kasi ya ajabu, hata hapa mkikimbia hamtatutetelesha CCM na wana CCM, maana tunaungwa mkono na Watanzania ambao wameshatambua dhamira njema ya Rais wetu mpendwa Mama Samia.

Narudia Tena mkiikimbia meza ya mazungumzo hakuna wa kuwabembeleza na wala hamtafanya chochote kile kuitikisa serikali yetu na Rais wetu. Nchi yetu na serikali yetu chini ya uongozi wa Mama Samia ni imara sana na ambayo haiwezi kutishiwa na yeyote kwa maneno na hata kwa matendo.

Ambaye haamini maneno haya basi ajaribu kuichezea amani ya nchi yetu hii inayolindwa kwa jasho na damu ili sisi Watanzania tuishi kwa amani na upendo na kufanya shughuli zetu bila wasiwasi wala bughudha.

Polee Sana Mbowe, uliowaamini na kuwakaribisha na kuwakuza sasa wanakuona hufai, sasa wanakuona muoga, sasa wanakuona huna uchungu na chama chako, sasa wanakuona umepitwa na wakati, sasa bila ushahidi wanasema unalamba asali, sasa wanataka kukupindua, wanataka kukutoa kinguvu, sasa wanakuzunguka, sasa wanajiandaa kukuasi na wameshakuasi kimsimamo.

Sasa hakuna uongozi wa kutoa dira na muelekeo, hakuna nidhamu ndani ya chama ndio maana kila mtu anakuja hadharani na kujiropokea anavyojuwa mwenyewe.

Hakika wapinzani mna mengi sana ya kujifunza kutoka CCM, maana mnayoyafanya huko huwezi kuyakuta wala kuyasikia, wala kutokea ndani ya CCM, sisi huku tunaheshimia na kupendana, tunawasikiliza viongozi wetu na kuwaheshimu, tunajuwa msimamo wa chama inatolewa na vikao maalumu baada ya vikao vya kihalali na siyo kwa mtu mmoja kuja kujiropokea hadharani au mitandaoni.

Ikikupendeza karibu sana CCM, mimi nikiwa kama mwanachama mtiifu wa CCm na ninayeendelea kukiunga mkono chama changu na kuipenda serikali yangu ya CCM nakukaribisha sana kwenye chama hiki kisicho na ubaguzi.

Kazi Iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Ungekuwepo enzi ya mkoloni ungejiunga na chama cha mkoloni na kuwaacha waafrika wenzako kwani unapenda vilivyokwishakuwa tayari. Waache wapiganaji CDM waunde chama.
 
Back
Top Bottom