Freeman Mbowe alia ubaguzi katika mfumo wa elimu Tanzania

Hata kidogo.
Lugha ya kufundishia siyo tatizo kabisa. Kiswahili kimekua na kujitosheleza kabisa kuwa lugha ya kufundishia elimu iliyo bora kabisa.
Kiswahili kimejitosheleza vipi wakati bado hatuna vitabu vya kutosha kufundishia kwenye fani mbalimbali zilizopo vyuoni?
 
Nimekusoma nikaishia kucheka tu; kimsingi umekubali hoja za Mbowe ila shida yako ni "uenyekiti" tu, tulia next year ataondoka wewe na wenzako mpumue tuone na hilo chaguo lenu mtakalotuletea.
 
Chadema imepwaya sana
 
Naomba nikupinge katika elimu bure, elimu bure imesaisia sana watanzania,shule za kata zinatoa elimu bora kabisa kulingana na mitaala yetu,labda shule iwe haina walimu.

Ukienda vyuo vikuu watoto kutoka shule za kata na hizo private wamejaa,labda tuendelee kuishauri serikali namna ya kuboresha zaidi mazingira ya ujifunzaji ya watoto wetu
 



 
Tulitakiwa tusome kwa Kiswahili toka chekechea mpaka phd
 
Tuachane nao tu! Aliyewaroga ni Nyerere na kashakufa!
 
Kwa Mara ya kwanza najitokeza NAYAPINGA MAWAZO YA MBOWE[emoji848][emoji848]
Mkuu Una shule binafsi?
Maana serikali ikiamua kubadilisha mitaala kwa lugha ya kingereza kuanzia std 1 to sec schools,

Soko la shule binafsi linapunguwa au kufa kifo cha Mende .
Shule binafsi ndy muuaji wa shule za government Tanzania.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Haya ndo Watanzania tunahitaji kuyasikia yakitugusa moja kwa moja siyo kila kukicha oooh Katiba mpyaa
 
Hebu nikumbushe hilo swali lako, mambo yalikuwa mengi wakati mwingine ni rahisi kusahau jambo.

Bado kwangu nakushauri usidharau umuhu wa lugha kwenye fani yoyote kama chombo cha mawasiliano, hicho ndio kiunganishi kikuu.
Ni wapi nimedharau lugha. Kiswahili siyo lugha?
 
Kiswahili kimejitosheleza vipi wakati bado hatuna vitabu vya kutosha kufundishia kwenye fani mbalimbali zilizopo vyuoni?
Kuwa na vitabu vya kutosha ni swala tofauti, ambalo ufumbuzi wake ni rahisi.
 
Ni wapi nimedharau lugha. Kiswahili siyo lugha?
"Ponda ponda lugha si hoja mradi ujue unachofanya"

Sijui kama ulijua maana ya hayo maneno uliyotumia "ponda ponda" maana yake ni kama kulipua, ...fanya bora liende, sasa kama kwako huku sio kudharau lugha sijui ni nini.

Huwezi "ponda ponda" halafu ukawasiliana na mlengwa, lugha ni chombo cha mawasiliano, ukiponda ponda unapoteza maana ya mawasiliano.
 
Kuwa na vitabu vya kutosha ni swala tofauti, ambalo ufumbuzi wake ni rahisi.
Mpaka huo ufumbuzi wake utakapopatikana ndio hilo jambo litakuwa rahisi, kwasasa sioni urahisi wowote, sisi bado ni tegemezi, kiswahili kitaendelea kutumika mitaani pekee, sio kwenye uwanja wa soko la ajira.
 
Mpaka huo ufumbuzi wake utakapopatikana ndio hilo jambo litakuwa rahisi, kwasasa sioni urahisi wowote, sisi bado ni tegemezi, kiswahili kitaendelea kutumika mitaani pekee, sio kwenye uwanja wa soko la ajira.
Basi tuseme upo sawa!
 
Huu ni ubishi. Sina la zaidi.
 
Kiswahili kama ilivyo kiarabu lugha hizi ni inversely proportional na elimu. Zikikuingia za kwanza kwenye ubongo wako maarifa sahau kuingia kwako zaidi utakuwa ni mtu wa kukariri kariri kulimeza kama lilivyo bila hata kujali linamaanisha nini na ukiwa mkubwa unakuwa ni mtu mwenye kulalamika lalamikankuwa unaonewa , unanyimwa haki
 
Elimu Bora katika Karne ya 21 inatakiwa imwezeshe mhitimu mambo makuu matatu;​

Kwanza, elimu imwezeshe mhitimu kuwa na tabia ya udadisi na kuyatafakari kwa kina mazingira/mambo/matukio yanayomzunguka kwa nia ya kubaini changamoto zinazomkabili katika kufikia anayoyatamani ili hatimaye kuweza kuainisha fursa na rasilimali zitakazotumika kutatua changamoto zinazomkabili.

Pili, elimu bora imwezeshe kufanya kazi na wengine kama timu moja. Hapa kwa kifupi ni uwezo wa kujenga mahusiano chanya kazini na nje ya kazi.

Tatu, elimu imwezeshe mhitimu kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuthubutu.

Kama mhitimu hana sifa hizi basi elimu aliyoipata haitamkomboa bali itakuwa kitanzi au minyororo ya utumwa kwa maana atashindwa kujitegemea isipokuwa atatumikia wengine.
Sasa tunataka elimu ya aina gani inategemea na jinsi tunavyoamini. Kama tupate elimu ya kwenda kufanya kazi nchi nyingine ama tupate elimu Ili tuweze kubadilisha maisha yetu kwa kutumia rasilimali zetu.
Kama mtazamo ni kwenda kuajiriwa nje ya nchi wanaopigia chapuo kiingereza wako sawa. Lakini kama mtazamo ni kujielimisha kwa ajili ya kujitawala basi lugha ya kiswahili ndio lugha sahihi itakayotuunganisha kati ya nadharia za kielimu na mazingira yanayotuzunguka ili kuibua udadisi.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…