Mkuu 'denooJ' nilikusoma kule juu ulipomjibu mmoja wa wachangiaji, nami nikashawishika kukujibu, lakini nikajizuia. Sasa umekuja na kunijibu hapa, kwa hiyo unanipa nafasi ya kukujibu pia.
Lugha ya Kiingereza ni lugha tu, kama lugha nyingine, pamoja na kwamba inazungumzwa na kutumika kila mahali duniani.
Kama lugha nyingine yoyote, mtu yeyote hata asiyekwenda shule anaweza kabisa kujifunza hii lugha na kuijua na kuitumia kwa mawasiliano, kama zilivyo lugha nyingine zozote, hata za kikabila zetu.
Ninakuomba unielewe: tatizo letu hapa Tanzania siyo kutojua lugha ya kiingereza. Tatizo ni elimu yetu kuwa mbovu, mbovu kabisa, kiasi kwamba wahitimu wake wanatoka bila kuiva kimasomo, bila kujali lugha waliyotumia katika kujifunza. Tatizo ni hilo.
Nimetumia mfano wa waChina hapo juu uliponijibu kwa maksudi kabisa, kwa sababu ya kuwa na uzoefu nao watu hao. Vijana wao wengi walitapakaa sana katika vyuo vya nchi za magharibi kwenye miaka ya 80, 90 hadi leo hii 2022. Wengi wa hawa wanafunzi walikuwa wakiingia kwenye vyuo hivyo vya magharibi,(soma hapa, kama Uingereza na Marekani nilikokutana nao) wakiwa hawajui kabisaaaaa, lugha ya Kiinereza. Hawa watu walikuwa wanawekwa kwenye 'program' ya kujifunza kiingereza kwa miezi mitatu, ndiyo, miezi mitatu, tena wakiendelea na kozi zao za masomo darasani.
Kwa vile hawa vijana walikuwa na msingi mzuri wa elimu, waliokuwa wamejifunzia nyumbani kwao kwa kichina, darasani hawakuathirika vyovyote kwa kutojua lugha ya kiingereza. Na baada ya hiyo miezi mitatu, pamoja na kwamba bado hawakuwa wamenyoosha lugha ya kiingereza vizuri sana, lakini waliweza kuendelea na masomo yao yote bila ya shida yoyote
Na hadi walipofikia mwisho wa masomo yao kabla ya kuhitimu, mtu usingeweza kutambua kabisa kwamba mwanzo hawakuwa na ufahamu wa lugha hiyo ya Kiingereza walipoanza.
Na sisemi wachina tu, Waarabu wengi pia hili lilikuwa linawahusu, hasa kutoka Iraq na kwingine. Huu ni uzoefu nilioupata, siyo kwa kuambiwa, bali kwa kushuhudia mwenyewe kwa muda mrefu sana.
Lugha yetu ya Kiswahili inatosha kabisa kuwafundisha watoto wetu tukiwa na mfumo wa elimu unaomfanya mwanafunzi kuelewa na kujua alichojifunza, na kuweza kutumia elimu hiyo katika maisha yake, bila kujali mazingira ya lugha nyingine itakayopaswa kutumiwa; mradi tu awe na basis (basic) ya matumizi ya lugha hiyo.
Kwenye jibu langu kwako hapo juu nimeweka factors kama mbili zinazotulazimu sisi kukimbilia kiingereza, (1) utegemezi wetu kiuchumi (kuvutia wawekezaji) (2) ushindani.
Nakusoma vizuri sana ulipozungumzia hao jamaa hususan wachina waliotoka kwao wakaenda nje Marekani na kwingineko kujifunza lugha za kule kwa miezi mitatu, then after wakaendelea na masomo yao mapaka vyuo vikuu na kupata elimu bora.iliyowasaidia kurudi kwao na kupata ajira.
Hapa ni sawa na umetolea mfano wa kikundi kidogo cha wazazi wenye uwezo kiuchumi hapa kwetu wanaopeleka watoto wao nje wakapate elimu bora then wakirudi nyumbani wapate ajira, na hawa wengi wao huzipata kwasababu hukidhi viwango vya ushindani.
Lakini vipi kuhusu hawa watoto wa shule za kata? wangapi huwa na uwezo aa kuahindana na hao wanaosoma nje au wageni waliotoka nje kuja kutafuta ajira Tanzania? simply hakuna.
Nimeona unazungumzia ubovu wa elimu yetu kwa ujumla sana, hujawa specific, hapa ningependa zaidi uwe specific ubovu kwenye eneo gani hasa?
Kwasababu mimi binafsi kwa uzoefu wangu, kesi nyingi zinazokuja toka kwa waajiri kwanini wanafunzi wa kayumba hawapati ajira, wengi husema wanakosa uwezo wa kujieleza kwa lugha ya kiingereza, hili kwangu ndio tatizo kuu ambalo hawa jamaa hukutana nalo.
Na nikiangalia kwa undani, naona kweli, mitaala yetu kwa shule za primary huwa mostly ni kiswahili, mtoto hujifunza kiingereza kwa somo moja tu English itself.
Huyu mpak aende secondary ndio akakutane na kiingereza, kumbuka ametoka primary school na kiswahili kwa miaka 7, then aende secondary aka adopt kiingereza kwa miaka 4.
Then A level 2 yrs tena asome arts, akienda masomo ya science ndio balaa kabisa, then chuo nako akienda kusoma hizo fani za ufundi ndio balaa, wengi hushindwa interview pale wanapokutanishwa na hao waliotoka nje.
Hapo bado hata walimu wanaowafundisha hao watoto ni wabovu kwenye kiingereza, nakumbuka kama miak miwili au mitatu nyuma, wanafunzi wengi walifeli somo la kiingereza kwenye mitihani yao ya form four waliyofanya, sasa huyu mwanafunzi atapata lini uwezo wa kuijua lugha hiyo?
Hao uliowataja wanaoenda kusoma Marekani na kwingineko wao hawakutani na matatizo haya, ndio maana nakubaliana na hoja ya Mbowe kwa maana kwamba tuwekeze kwenye kiingereza, kuanzia vitabu, walimu, na vyote watoto waanze kupata elimu bora ya kiingereza wakashindane na hao wanaotoka nje, lkn sio tupoteze muda na kiswahili chetu.