Freeman Mbowe alia ubaguzi katika mfumo wa elimu Tanzania

Freeman Mbowe alia ubaguzi katika mfumo wa elimu Tanzania

Nitakupa mfano mdogo sana, tena usiohitaji jasho kabisa kuwa mahili ndani ya fani hiyo. Uandishi wa habari.

Ukitaka mfano wa masomo ya sayansi, pia nitakupa mifano mingi tu. Angalia watu tunaotazamiwa kuwategemea na kuwapa heshima zote kwa kusimamia elimu yetu, wao ndio wakitoa mifano mibovu kabisa.
Sijasoma Ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha uharibifu wa mazingira kilichosababisha samaki kufa ziwani na mto mara. Lakini kama yanayosemwa kwamba ndiyo yaliyomo kwenye ripoti hiyo, ninasikitika sana.
Kwenye issue ya ubovu wa elimu ningependa zaidi uzungumzie kule mwanafunzi anakopata maarifa yatakayomuwezesha kushindana na ulimwengu kwenye soko la ajira, usizungumzie matokeo yake yule anayepewa hayo maarifa anayatumiaje baada ya kupewa.

Kuhusu mfano wa ripoti uliyotoa hapa naona mfano wako hauko sahihi, nasema hivyo kwasababau huyo profesa inawezekana kabisa ana elimu nzuri na ya viwango hitajika, tatizo lake ni kuchanganya elimu yake na siasa, hapa ndipo alipofeli.

Lakini kama angekuwa anatakiwa aende kwenye inyerview kwa ajili ya kupata ajira, inawezekana kabisa angeiweka siasa pembeni abaki na elimu na maarifa yake ambayo yangemuewezssha kufanya vizuri kwenye interview hiyo.
 
Kwani mtoto unampeleka shule kwa lengo gani? ajue lugha na elimu na kukaa nayo nyumbani? au ajue lugha pamoja na elimu vitakavyo muwezesha kuyamudu mazingira atakayokabiliana nayo mbele ya safari yake ya kimaisha?
Nenda kule Zanzibar kwenye mahoteli ya kimataifa kama utawakuta hao unaowalazimisha wasome kwa kiswahili
 
Ok, kama unazungumzia wanaopelekwa kwa ajili ya mahitaji maalum hili nalo kwangu sio tatizo, mbona hata kwetu hufanya hivyo, lakini hawa tayari wanakuwa na guarantee ya ajira.

Vipi kuhusu wale ambao hawapelekwi huko ambao ndio kundi kubwa zaidi na ndio wanaozungumziwa kwenye mada hii, wao wasaidiwe vipi ili waondokane na tatizo la ajira kwa nchi hii yenye nafasi chache za ajira tena za kushindaniwa na watu toka nje?
Kuna dawa moja pekee.
Elimu yetu ifumuliwe moja kwa moja. Huko ndiko kwenye tatizo, siyo kwenye lugha.
 
Uko sahihi kuuliza maswali kama hayo lakini umekosa msingi wa unachokiita “elimu” na umeweka ufinyu katika namna ya kupata elimu na kuiona iko “shuleni”. Uzuri umetaja “kumudu mazingira”. Nitakukumbusha haya:
1. Hakuna mtu anayetumia elimu ya shule ya msingi kufanya chochote. Hata hajira rasmi hazina watu hao na ndio maana walifoji vyeti na wakafurushwa na JPM.
2. Mazingira ya sasa yanamtaka mtu akabiliane nayo sio kwa bidii tu, bali ufahamu. Tuna EAC na hivo mipaka ya ajira iko wazi. Ndio kusema hukusoma Mbowe anazungumzia watu wajuzi wa kiingereza wakichukua kazi kubwa kubwa? Ina msaada gani kama ajira za watanzania itakuwa ni kufagia ofisi, kumwagilia maua eti kwa sababu hawaajiriki kwa hawa wajuzi wa kiingereza???
3. Amezungumzia ubaguzi. Wewe unadhani wazazi wanaowapeleka watoto kwenye shule za mchepuo wa kiingereza hawajaamua kuwatofautisha watoto wao na wa shule za serikali??

Sababu ya kutaka kiingereza ni kupanua uwigo wa ushindani!! Sio kwamba Kiswahili hakina maana. Kwa kiswahili tu, maana yake uwigo unakuwa finyu. Kiingereza kina wigo mpana wa maarifa kwa sababu ndio lugha inayoongewa (hata kama si kwa ufasaha) na watu wengi kuliko lugha nyingine yoyote!!
Narudia kukusoma lakini sikuelewi.

- Hakuna mahali niliposema elimu ya msingi inaweza kumpa mtu ajira.

- Ushindani nimeuzungumzia kwa kuwataja wakenya kwenye interview kwenye soko letu la ajira, ili kuonesha vile ujuzi wao wa lugha pamoja na maarifa wanayopata kwenye vyuo vyao unavyowasaidia.

- Suala la ubaguzi, nakubaliana nalo ndio maana Mbowe ameamua kulizungumzia ili kuondoa dhana ya "aliyenacho" na "asiyenacho" kwenye elimu yetu, sasa hapa napo sijaona pointi yako.

Hicho kiswahili kama unaona kina maana, niambie kitakusaidia wapi kwenye kushindana kwenye soko la ajira kama sio kuishia kuwa mfagizi? hapa tuwe realistic, kama kweli mnataka kukibeba kiswahili, basi kibebeni kama pambo tu kwa wakati huu, lakini sio kiwasaidie kushindana kaenye soko la ajira hasa EAC.
 
Kwenye issue ya ubovu wa elimu ningependa zaidi uzungumzie kule mwanafunzi anakopata maarifa yatakayomuwezesha kushindana na ulimwengu kwenye soko la ajira, usizungumzie matokeo yake yule anayepewa hayo maarifa anayatumiaje baada ya kupewa.

Kuhusu mfano wa ripoti uliyotoa hapa naona mfano wako hauko sahihi, nasema hivyo kwasababau huyo profesa inawezekana kabisa ana elimu nzuri na ya viwango hitajika, tatizo lake ni kuchanganya elimu yake na siasa, hapa ndipo alipofeli.

Lakini kama angekuwa anatakiwa aende kwenye inyerview kwa ajili ya kupata ajira, inawezekana kabisa angeiweka siasa pembeni abaki na elimu na maarifa yake ambayo yangemuewezssha kufanya vizuri kwenye interview hiyo.
"Kushindana na ulimwengu kwenye soko la ajira", hitaji ni moja tu, na siyo lugha. Ni kuwa na uelewa wa fani unayoitumikia (unayoombea kazi). Hakuna zaidi ya hapo.

Ponda ponda lugha, si hoja, mradi ujuwe unachokifanya.

'Surgeon' mzuri hahitaji kujua kiingereza safi sana ili aweze kufanya kazi yake ipasavyo.

Kwa bahati nzuri au mbaya umetumbukiza sababu nyingine inayoharibu elimu yetu..., SIASA.
 
Kuna dawa moja pekee.
Elimu yetu ifumuliwe moja kwa moja. Huko ndiko kwenye tatizo, siyo kwenye lugha.
Huko "kufumua" hakutahusisha na kubadilisha lugha? nionavyo kama "utaifumua" lakini bado lugha itumikayo ikabaki kiswahili naona tutaendelea kuzunguka pale pale.
 
Nae atuonyeshe mfano, anaongea kiingereza kilichonyooka? Au ni sawa na yule jamaa yangu aliyehojiwa na radio fulani ya Kenya, tulihesabu neno "actually" mara mia. Ni kweli lugha inatuendesha ila tukiweka Nia tutaweza.
Kwa kweli Lughba ya Kiingereza inatuangusha sana Watanzania.

Nilishangaa sana wakati fulani nikiwa West Afrika kikazi. Sikuona Mtanzania hata mmoja kwenye kundi lile nililokutana nalo. Jioni nilikuwa nikikutana nao, wao walikuwa wakipenda sana kunisikia mimi nikiongea Kiswahili cha Kitanzania. Lilikuwa ni kundi la Wakenya 12 wakifanyia UN., Wakiwa na jukumu maalum kwa nchi ya Ivory Coast na Liberia. Mimi nilikuwa huko kikazi kwa kupitia makampuni ya kimataifa.

Binafsi sioni mantiki ya Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia masomo shule za msingi, halafu gjafla mwanafunzi akiingia Secondary lugja ya kufundishia masomo inageuka na kuwa Kiingereza.

Tuamue kukiweka Kiswahili kuwa somo maalum la Lugha lakini Kiingereza kiwe lugha ya kufundishia.

Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa hatuwezi kukiacha Kiingereza kwa sababu ndiyo Kiswahili cha Dunia.
 
Mtoto anaenda shule ili ajue kusoma na kuandika, lakini pia kupata maarifa ya kuja kumsaidia katika maisha yake.

Lugha ni njia tu inayo tumika kumhamishia mtoto maarifa. Hivyo lugha mama humrahisishia zaidi kuelewa hayo maarifa kuliko ile lugha ya pili. (Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali!)
Atayapataje hayo maarifa wakati yote yameandikwa kwa Lugha ambayo haimudu?¡
 
Siungi mkono hoja. Lugha nzuri ya kufundishia mtoto ni ile Lugha Mama! Na kwa bahati zuri kwa Tanzania ni Kiswahili.
Hicho kigezo cha kusema Kingereza ni Lugha ya Kimataifa, hakina mashiko. Tunaweza kukisoma kama Lugha nyingine mfano Kichina, Kifaransa, nk. Kwa ajili ya hayo matumizi ya Kimataifa.

Kuhusu ubaguzi wa kielimu nchini, yuko sahihi kabisa! Elimu yetu inawabagua watoto kwa misingi ya mwenye nacho na asiye nacho! Elimu Bure kwa Tanzania ni kichaka cha watawala kuwapumbaza Watanzania masikini! Maana watoto wao hawasomi huko! Badala yake wanawapeleka shule binafsi za mchepuo wa kiingereza, na zenye gharama kubwa.


Na hata watoto wake Mh. Mbowe bila shaka wamesoma/wanasoma shule za gharama kubwa, kama ilivyo kwa wanasiasa wenzake wengi! badala ya zile za kata.
Huyu Mbowe anatakiwa awe na washauri wazuri.Naona anakurupuka tu.
 
"Kushindana na ulimwengu kwenye soko la ajira", hitaji ni moja tu, na siyo lugha. Ni kuwa na uelewa wa fani unayoitumikia (unayoombea kazi). Hakuna zaidi ya hapo.

Ponda ponda lugha, si hoja, mradi ujuwe unachokifanya.

'Surgeon' mzuri hahitaji kujua kiingereza safi sana ili aweze kufanya kazi yake ipasavyo.

Kwa bahati nzuri au mbaya umetumbukiza sababu nyingine inayoharibu elimu yetu..., SIASA.
Kama unazungumzia specialist ndio maana hupelekwa nje kujifunza, especially madaktari, na huko hukutana na walimu wazuri wa lugha wanaoweza kuwapa elimu yenye viwango.

Lakini usidharau umuhimu wa lugha kwa "kuponda ponda" hasa kwenye fani sensitive kama ya utabibu, bila daktari kumsikiliza mgonjwa na kumuelewa vizuri ni sawa na kutengeneza tatizo kubwa zaidi mbele ya safari.
 
Mbowe hataki kukuza lugha ya Kiswahili ili iwe lugha ya kitaaluma?
Mbona wachina, Wajapan, Warusi, Waswede, Wajerumani, wafaransa wanatumia lugha zao kufundishia watoto wao kwa nini kiswahili kisiweze?
Lugha yako ili iwe na nguvu, na kuwa nyenzo muhimu ya kupatia maarifa, ni lazima kuwa na maarifa makubwa katika jamii husika.

Kama hutengenezi dawa za kuwatibu watu na mifugo, hutengenezi vifaa tiba, hufanyi ugunduzi wowote wa kisayansi, hutengenezi machine yoyote, n.k; lugha yako haiwezi kuwa na nguvu ya kuhamisha maarifa kwenda kwa wanafunzi.

Mataifa uliyoyataja, yanajitegemea kwa kiasi kikubwa katika maarifa. Uswizi, zamani walikuwa wanatumia Kijerumani kama official language yao, japo wananchi wao walio wengi walikuwa wanaongea French. Baada ya maarifa kukua, sasa hivi official language yao ni Kifaransa.
 
Mjadala wa lugha gani itumike kufundishia katika mfumo wa elimu, mara nyingi umekuwa ukiibua hisia mbalimbali miongoni mwa wadau wa elimu nchini.

Aghalabu mitazamo huwa ni miwili, ama Kiingereza kiendelee kutumika kama ilivyo sasa katika ngazi za sekondari na vyuo vya elimu ya juu, au tugeukie Kiswahili ambacho kwa sasa kinatumika katika ngazi ya elimu ya msingi pekee.

Mitazamo hiyo imezaa kambi mbili kuu kubwa ambazo mara zote zimekuwa zikiparurana kwa hoja.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitoa msimamo wa chama chake, akisema kikifanikiwa kushika dola, lugha itakayotumika ni Kiingereza ili kuondoa alichokiita ubaguzi wa kiajira unaotokana na vijana wengi wa Kitanzania kutoijua lugha hiyo .

Alia ubaguzi

Akiwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro siku chache baada ya kutoka gerezani alipokuwa mahabusu, Mbowe alisema elimu ya Tanzania imejaa ubaguzi wa makundi kati ya wenye uwezo na masikini, huku akieleza kuwa ubaguzi huo unajidhihirisha hata katika ajira hususan kwenye taasisi na kampuni kubwa.

Akihutubia mamia ya wafuasi wake na wananchi waliojitokeza kumpokea katika viwanja vya Bomang’ombe, Mbowe alisema elimu inayotolewa kwa sasa haimjengi Mtanzania kuingia katika soko la ajira kutokana na mfumo wake ulivyo na kwamba inahitaji mabadiliko.

“Kumekuwa na ubaguzi katika elimu kwani viongozi wetu wamekuwa wakituhutubia tujifunze Kiswahili ni lugha yetu ya Taifa, lakini leo Kiswahili hicho kinazungumzwa kwenye shule zetu za kata, viongozi wote na watu wenye uwezo wanasomesha watoto katika shule za mfumo wa Kiingereza; huu ni ubaguzi,” alisema.

Kiongozi huyo anasema Chadema kikiingia madarakani, kitahakikisha watoto wote wanafundishwa kwa lugha ya Kiingereza, kwa kuwa ndiyo lugha ya kimataifa.

Anasema katika dunia inayokwenda kwa kasi huku ikichagizwa na mabadiliko ya teknolojia, maarifa ya lugha ya Kiingereza ni ya lazima na kwamba Kiswahili kitabaki kuwa kama somo la ziada.

Advertisement
Anatoa mfano wa namna Wakenya wanavyotamba katika soko la ajira, kwa sababu ya uwezo walionao katika kutumia Kiingereza.

‘’Vijana wa Kenya wamelikamata soko kubwa hata katika nchi zenye uchumi mzuri ndani ya Afrika tofauti na Watanzania, ambao licha ya kuwa na uwezo, wanakwamishwa na suala la lugha,’’ anaeleza.

Ilivyo sasa nchini, wanafunzi wa shule za awali hadi darasa la saba, wanafundishwa kwa lugha ya Kiswahili, huku Kingereza kikiwa kama somo.

Pia kuna shule za mchepuo wa Kingereza katika ngazi hiyo ya elimu, hata hivyo, nyingi zinamilikiwa na watu au taasisi binafsi. Wanafunzi hao wote wanapomaliza darasa la saba, wanalazimika kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia.

Wasomi wamjibu

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Aman Chipalo anapingana na mtazamo wa Mbowe, akisema lugha inayofaa kwa kufundishia nchini Tanzania ni Kiswahili, ambacho kinasaidia wanafunzi kuwa na uelewa mpana wa masomo.

Anasema wanaotaka Tanzania ifundishe kwa lugha ya Kiingereza, wanatakiwa kufanya utafiti kwanza ili wajenge hoja zao kwa mapana zaidi.

“Tafiti zilishafanyika kwamba, mwanafunzi anajifunza vizuri zaidi akifundishwa kwa lugha yake ya kwanza. Sisi Tanzania hasa maeneo ya vijijini lugha ya kwanza ni zile za makabila yetu baada ya hapo ni Kiswahili, hivyo tunapaswa kufundisha kwa lugha yetu ya Taifa,” alisema Chipalo.

Msomi huyo anabainisha kuwa, katika nchi zilizoendelea elimu inatolewa kwa lugha mama isipokuwa barani Afrika, ambapo nchi nyingi zimeendelea kukumbatia lugha za kikoloni katika mifumo ya ufundishaji.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Linkoping cha Sweden Dk Hawa Mnyasenga, anasema lugha inayofaa kufundishia ili mtoto aweze kuelewa anachofundishwa ni ile aliyoizoea na ambayo inazungumzwa na wengi.

Anasema kama Kiswahili kingetumika kufundishia na kuwekewa mkazo, watu wangeelewa zaidi kuliko ilivyo sasa, kwa sababu ndiyo lugha inayotumika hata kwa mawasiliano.

“Nilishakuwa mwalimu wa sekondari kwa miaka kadhaa nikifundisha masomo ya sayansi hapo Tanzania. Niliona ugumu wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wanavyohangaika kuelewa lugha ya Kiingereza na mada ya nadharia za sayansi kwa wakati mmoja. Yaani mwalimu unakuwa na mambo mawili kwa wakati mmoja, kwanza mtoto afahamu lugha ndipo aje ajue unachomfundisha” anasema Dk Mnyasenga.

Anafafanua kuwa licha ya Kiswahili kuonekana kuwa kichanga kwa kukosa baadhi ya misamiati, changamoto hiyo inaweza kutatuliwa kwa kuiga mifano ya baadhi ya nchi zilizoamua kufundisha kwa kutumia lugha zao na hatimaye kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Hapa Sweden lugha ya kufundishia kuanzia chekechekea ni Kisweden, ingawa kuna kozi chache zinazofundishwa kwa Kiingereza hasa vyuo vikuu kuanzia shahada ya pili na shule chache sana zinazofundisha Kiingereza; wenzetu waliamua tangu mwanzo,” anasema.

Naye mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St John cha jijini Dodoma, Fredrick Golden, alikosoa ufundishaji kwa lugha ya Kiingereza, akisema unachelewesha maendeleo ya nchi.

Anatoa mfano wa vijana wengi wenye uwezo wanavyofeli mitihani, kwa sababu ya kutojua lugha.

‘’Lugha inachelewesha wanafunzi na kuwafanya washindwe kwenye mitihani. Masomo wanayosoma kwa lugha ngeni yangeweza kutafutiwa misamiati ili yafundishwe kwa Kiswahili ambacho walianza kukijua wakiwa nyumbani kabla ya kwenda shule, ‘’ analeza.

Anaongeza: ‘’Huwachukua wanafunzi zaidi ya miaka miwili angalau kuanza kuelewa lugha wanayofundishiwa, hivyo wanajikuta wametumia muda mwingi kujifunza vitu ambavyo hawavijui jambo linalosababisha waingie kwenye mitihani kwa kukariri masomo ili wafaulu lakini si kuwa na uelewa.’’

Kwa mujibu wa Golden, masomo ya Kiswahili yakifundishwa kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu, Tanzania itakuwa na wasomi wengi kuliko ilivyo sasa.

‘’Wanaotaka Kiingereza ndiyo kitumike kufundishia, wakajifunze kwa nchi kama Japan, Korea, Ujerumani na Russia. Nchi hizi zimeendelea kwenye sayansi kuliko mataifa mengine yanayofundisha lugha za kigeni,’’ anabainisha.

Lugha mbili inawezekana

Kwa upande mwingine, wapo wasomi wanaopigia chapuo matumizi ya lugha zote mbili akiwamo Profesa Kitila Mkumbo ambaye Februari mwaka huu alizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jijini Dodoma na kueleza kuwa lugha zote mbili zinaweza kutumika katika mfumo wa elimu, kwa sharti kuwa ziwe zinafahamika kwa wanafunzi.

“Lugha gani si hoja. Kwa Tanzania lugha zote mbili zinaweza kutumika. Ukienda Afrika Kusini kuna lugha rasmi 11 na watoto wote wanazisoma. Maoni yangu watoto wajifunze lugha zote mbili,” alieleza.

Alisema kwa utaratibu huo, inawezekana mitihani ikatungwa kwa lugha zote na mwanafunzi akawa na uhuru wa kuchagua lugha anayoitaka.

Alisema Watanzania wasidanganyike, kwani watoto wana uwezo wa kujifunza lugha zaidi ya moja na kwamba kitaalamu mtoto kuanzia miaka mitatu hadi 10, anaweza kujifunza lugha hadi saba bila changamoto yoyote.“Hoja ni watoto wetu wote wawe na uwezo wa kutumia lugha zote mbili halafu atachagua ipi sasa atafanyia mitihani. Ila tusiwafanye Watanzania wakawa wafungwa wa lugha ya Kiingereza,” alifafanua msomi huyo aliyebobea kwenye saikolojia ya elimu, huku akiongeza kuwa Watanzania wasidanganyike kuwa Kiswahili pekee kinawatosha.

Kwa upande wake, mdau wa elimu Richard Mabala, aliwahi kuzungumza na Mwananchi na kueleza kuwa Kiingereza kinaweza kufanya vizuri zaidi kwa mazingira ya Kitanzania kama kitafundishwa kama lugha ya pili au ya tatu.

‘‘... lakini sio kuwa lugha ya kufundishia kwa sababu kimekuwa kikwazo cha wanafunzi kukosa ujuzi na kuishia kukariri,’’ alisema Mabala.
Huyo anayejiita msomi, naye ni bure. Ni msomi wa kukariri.

Ajiulize:

Kwa nini nchini China, Uturuki, India, Ukraine, South Korea, Israel, Dubai, Qatar, kwa sasa vyuo vinavyotumia Kiingereza kufundisha vinazidi kuongezeka, na wanafunzi wengi wa kwenye mataifa hayo, kutoka familia zenye uwezo mkubwa wanapenda kuwapeleka watoto wao kwenye vyuo hivyo?
 
Laiti mngejua watoto wanaotoka English medium wanavyofanya vizuri huku sekondari msingethubutu hata kidogo kumpinga Mbowe ! Watoto wanaotoka shule zetu za kiswahili mateso wanayoyapata huku sekondari laiti mngewaona mngemsapoti Mbowe mia. Ni wajibu wa serikali kutoa elimu isiyo na ubaguzi,... Kwanini wengine wasome kwa kiingereza,, wengine kwa kiswahili!?!? Kwanini watanzania wengine wajihisi wanyonge ktk nchi yao eti kisa tu wanasoma public schools!? Nafikiri hii ndo,hoja kuu ya Mbowe, nami namsapoti 100.
Ndugu Data! Mitanzania mingi ni mijinga Sana. Mi ni mwl English medium. Watoto wanaelewa Sana. Tatizo Mwl Nyerere watu walimdanganya kuwa ukiendelea na Kiingereza watu wataerevuka na watajua mengi ya nje watakupindua! Akabadili gia angani Kiswahili tu tofauti na nchi zilizotawaliwa na Mwingereza. Sasa ccm inafurahia cnn, bbc world, sky news etc wakiongea watz ni hola! Shenzi type!
 
Mbowe hataki kukuza lugha ya Kiswahili ili iwe lugha ya kitaaluma?
Mbona wachina, Wajapan, Warusi, Waswede, Wajerumani, wafaransa wanatumia lugha zao kufundishia watoto wao kwa nini kiswahili kisiweze?
Lugha inaendana na uchumi wa inchi,kama.uchumi wako ni takataka unategemea nani atajifunza lugha yako,atakuja kwako kuomba nini?huyo Rais wako akienda kutembeza bakuli unazani huwa anaomba kwa kiswahili?

Au anaomba kiubububu?
 
Kingereza ni lugha muhimu kwa nchi kama Tanzania na haiepukiki. Serikali iwekeze kupata walimu wazuri wa kiingereza liwe ni somo kama ilivyo sasa kuanzia chekechea. Nilikutana na jamaa mmoja anakijua kingereza vizuri. Alisoma kijijini kwetu shule hizi za kawaida na alipofika sekondari huko huko kijijini mwalimu wao wa kiingilishi akawa ni raia wa Marekani valentia.

Hivyo tusikimbilie Kiswahili kwa kukataa uwekezaji kwenye Kiingereza. Lugha zote mbili zitumike kufundishia kwa level ya msingi kingereza kiwe somo. Na ikifika sekondari kiswahili kiwe somo. Maneno haya ya wenye maslahi ya miradi ya ulaji kwenye lugha ya kiswahili yataligharimu taifa hili.

Ujumbe kwa Mbowe, CDM haiwezi kubadilika kama itaendelea kuwa na akili hizi hizi za MKT. Ni wakati umefika wapishe wengine wao wawe washauri tu. Waache tabia za ujasiriasiasa.
 
Huko "kufumua" hakutahusisha na kubadilisha lugha? nionavyo kama "utaifumua" lakini bado lugha itumikayo ikabaki kiswahili naona tutaendelea kuzunguka pale pale.
Hata kidogo.
Lugha ya kufundishia siyo tatizo kabisa. Kiswahili kimekua na kujitosheleza kabisa kuwa lugha ya kufundishia elimu iliyo bora kabisa.
 
Kama unazungumzia specialist ndio maana hupelekwa nje kujifunza, especially madaktari, na huko hukutana na walimu wazuri wa lugha wanaoweza kuwapa elimu yenye viwango.

Lakini usidharau umuhimu wa lugha kwa "kuponda ponda" hasa kwenye fani sensitive kama ya utabibu, bila daktari kumsikiliza mgonjwa na kumuelewa vizuri ni sawa na kutengeneza tatizo kubwa zaidi mbele ya safari.
Mkuu 'denooJ', niamini mkuu, ninaelewa ninachokizungumzia hapa.
Lugha siyo sehemu ya utaalam wowote hapa duniani, ni chombo tu, na kuna vyombo mbalimbali vinavyowezesha kupata matokeo mazuri.

'Surgeon' hahitaji kujua lugha kuwa 'surgion' mzuri hata siku moja. Anajua kazi yake, awe amejifunza kwa kichina, kihindu, kiingereza, kifaransa, n.k.

Lile swali langu naona umeliweka kapuni kwa maksudi mazima, kuhusu anayejifunza lugha kwa miezi mitatu na anayetumia lugha kwa miaka mitatu, bado asiweze kuitumia lugha hiyo.
 
Sipingi Kiswahili kinaweza kutumika, ila Kingereza ni muhimu zaidi, hivi leo utoke zako huko Musoma hujui Kiswahili ukifika Darisalama nani atakuelewa na kilugha,? je huoni faida ya kuongea lugha ya kikwenu pamoja na Kiswahili??? ... the same goes to English, nani atakuelewa ukitaka kupata kazi private sector ambapo ni waajiri wakuu ama ukitaka kazi nje ya nchi ama scholarship??? kwa nini tulimit horizon ya ajira kwa wahitimu?
 
Siungi mkono hoja. Lugha nzuri ya kufundishia mtoto ni ile Lugha Mama! Na kwa bahati zuri kwa Tanzania ni Kiswahili.
Hicho kigezo cha kusema Kingereza ni Lugha ya Kimataifa, hakina mashiko. Tunaweza kukisoma kama Lugha nyingine mfano Kichina, Kifaransa, nk. Kwa ajili ya hayo matumizi ya Kimataifa.

Kuhusu ubaguzi wa kielimu nchini, yuko sahihi kabisa! Elimu yetu inawabagua watoto kwa misingi ya mwenye nacho na asiye nacho! Elimu Bure kwa Tanzania ni kichaka cha watawala kuwapumbaza Watanzania masikini! Maana watoto wao hawasomi huko! Badala yake wanawapeleka shule binafsi za mchepuo wa kiingereza, na zenye gharama kubwa.

Na hata watoto wake Mh. Mbowe bila shaka wamesoma/wanasoma shule za gharama kubwa, kama ilivyo kwa wanasiasa wenzake wengi! badala ya zile za kata.
Kiswahili si Lugha Mama 99% ya Watanzaniani Kihaya Kisukuma, Kiluguru, Kizigua, Kiha, Kimakonde nk.
 
Mkuu 'denooJ', niamini mkuu, ninaelewa ninachokizungumzia hapa.
Lugha siyo sehemu ya utaalam wowote hapa duniani, ni chombo tu, na kuna vyombo mbalimbali vinavyowezesha kupata matokeo mazuri.

'Surgeon' hahitaji kujua lugha kuwa 'surgion' mzuri hata siku moja. Anajua kazi yake, awe amejifunza kwa kichina, kihindu, kiingereza, kifaransa, n.k.

Lile swali langu naona umeliweka kapuni kwa maksudi mazima, kuhusu anayejifunza lugha kwa miezi mitatu na anayetumia lugha kwa miaka mitatu, bado asiweze kuitumia lugha hiyo.
Hebu nikumbushe hilo swali lako, mambo yalikuwa mengi wakati mwingine ni rahisi kusahau jambo.

Bado kwangu nakushauri usidharau umuhu wa lugha kwenye fani yoyote kama chombo cha mawasiliano, hicho ndio kiunganishi kikuu.
 
Back
Top Bottom