- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona poster ya The Chanzo yenye picha ya Freeman Mbowe ikiwa na maelezo ya kwamba Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amemshukuru Rais Samia kwa kuungana na CHADEMA Kuomboleza msiba wa mzee Kibao, je taarifa hii ni ya kweli na chanzo chake ni The Chanzo.
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye alikuwa ni moja kati ya waasisi wa chama hicho mwaka 1992 na mwaka 2005 alikuwa mgombea wa urais kupitia tiketi ya CHADEMA, lakini pia mwaka 2010 hadi 2020 alikuwa mbunge wa jimbo la Hai mwaka.
Mnamo tarehe 11 septemba, 2024, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe aliongoza mkutano na waandishi wa habari uliokutanisha viongozi wa Chama na Mabaraza wa ngazi zote wa Kanda ya Pwani uliofanyika makao makuu ya chama hicho Mikocheni Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine mwenyekiti aliitaka serikali kuwajibika juu ya matukio ya watu kupotea, kutekwa na hata kuuwawa.
Kumekuwa na chapisho linalosambaa mtandaoni likionesha kuwa chanzo chake ni The Chanzo, huku likieleza kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuungana na CHADEMA katika kuomboleza msiba wa mjumbe wa sekretarieti ya chama hicho Ali Mohammed Kibao aliyetekwa Septemba 06 2024 na siku moja baadaye kupatikana akiwa ameuawa. Taarira hizo zinazosambaa mtandaoni unaweza kuzipata hapa, na hapa.
Ni upi uhalisia wa Chapisho hilo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna Mwenyikiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hakutoa kauli hiyo ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan juu ya kuomboleza msiba wa Ali Kibao.
Aidha, machapisho rasmi ya The Chanzo katika kurasa zake za mitandao ya jamii huweka tarehe ya siku husika tofauti na chapisho hilo ambalo halioneshi tarehe ya siku husika.
Chapisho la The chanzo likiwa na tarehe kama ambavyo huwa wanaweka
Chapisho lililohaririwa likiwa halina tarehe kama la hapo juu
Pamoja na hilo kumekuwa na utofauti wa nembo inayotambulisha mtandao wa X ambapo chapisho hilo limetumia nembo ya zamani ya alama ya Ndege wakati mtandao huo ukijulikana kama “twitter” tofauti na The Chanzo wenyewe ambao hutumia nembo yenye herufi X kuutambulisha mtandao huo.
Nembo ikionesha mtandao wa X ambao zamani ulikuwa unatumia alama ya ndege
Nembo ya zamani ya ndege ambayo kw sasa haitumiki tena na mtando wa X
Vilevile kurasa rasmi za The Chanzo zimeshapisha taarifa inayokanusha taarifa hizo ambazo zinasambaa mtandaoni na kwamba wao hawahusiki na taarifa hizo si za kweli.