Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mahakama inaenda kusikiliza madai ya Mwenyekiti kwamba amechafuliwa.

Hoja za msigwa zinapaswa kujibiwa na chama kupitia katibu mkuu kama ambavyo Lissu alipendekeza.
Nyie watu vipi?

Mbowe katajwa kama Mbowe. Sasa Msigwa hoja yake si ndiyo hiyo hiyo. Au wewe unataka hoja gani tena ijibiwe na CHADEMA?

Au hata hiyo barua yenyewe hujaisoma?
 
Solemba na Gundu juu. Leo hii kina Samson Mwigamba wapo wapi. Nani anayejali leo hii Vincent Mashinji anafanya nini huko alipo!?
Ni vyema Wanasiasa Vijana wakajifunza kuhusu hayo

Leo hii pamoja na kuandaa pamoja ule waraka wa kuwang'oa akina Mbowe madarakani, unaweza kukuta Kitila Mkumbo hana muda hata wa kupokea simu ya Samson Mwigamba Kwa kuhofia atapigwa Kibomu cha Hela
 
CCM ni chama cha Utulivu na amani, ukiwemo ukawekwa bench, Tulia kimya, elewa unapimwa imani, 😊, ukifaulu hapo elewa umefaulu. Kaa mkao, ona yule mkulima wa nyanya, mifano ni mingi sana.
Sio wote lakini

Unadhani hawa waliotoka CHADEMA na kuhamia kule unadhani watapitishwa kugombea Ubunge mwakani 2025?

We subiri ujionee
 
Hata kauli na misimamo yake kuhusu Wamasai kuhamishwa Ngorongoro zilionyesha wazi kuwa anataka kuwafurahisha watawala.

Kama ilivyoshauriwa busara ilikuwa kuzijibu hoja zake.

Kwamba:

IMG_20240906_122258.jpg


Huku ni kuendelea ku m entertain kwenye ligi zisizokuwa na mashiko.
 
Mkubwa tunaweza kuona chanzo cha habari yako kama hautajali?

By the way ni jambo jema kumtaka alipe hiyo fidia ama akathibitishe madai yake

Maana Mchungaji Msigwa Kila Siku yeye na Mbowe, Mbowe na yeye

Utasema wana ugomvi wa kuibiana mali ama Wapenzi 🙌
Shida ukishakua ccm akili sijui inaendaga wapi? Apa unaweza kuona Mzee wa watu Mzee Lowassa ( R.I.P) alivyokua smart. alipe tu ili akome
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

=====


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi, asipfanya hivyo ajiandae kulipa kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 Mahakamani kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia soma
View attachment 3088571View attachment 3088572View attachment 3088573View attachment 3088574View attachment 3088575View attachment 3088576View attachment 3088577



Mbowe shikilia hapo hapo.

Mbowe ni Kiongozi halali wa Chadema mana alichaguliwa na wajumbe zaidi ya 700 kwa kura . Waliona anafaa na anaweza kulingana na Wakati huu na Katiba iliyopo inayompa mamlaka Makubwa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM anayefanya kila mbinu kudhoofisha wapinzani wake kwa kutumia fedha na madaraka . Sasa chama kisipikuwa na Mwenyekiti imara na jasiri kama Mbowe basi ni rahisi kusambaratika na kupotea .

Chadema ina wanachama zaidi ya mil. 5 sasa Msigwa peke yake hawezi kuwa ndiye anayeona ubaya wa Mbowe.
 
CCM wamemtupia Msigwa mjusi wa hii kesi ili zile hela walizmlipa kwenye biashara ya kumnunua ziishe kwenye kesi maana wanaona hakuna la maana aliloleta CCM toka Chadema kwani yote anayosema yalishasemwa na wote walionunuliwa kama bidhaa. Msigwa ameyatimba, hili ni la kwake mwenyewe.
 
Mahakama inaenda kusikiliza madai ya Mwenyekiti kwamba amechafuliwa.

Hoja za msigwa zinapaswa kujibiwa na chama kupitia katibu mkuu kama ambavyo Lissu alipendekeza.
Katibu Mkuu akijibu kwa maelezo tu mtadai haaminiki; atoe ushahidi wa nyaraka. Nyaraka za chama haziwezi kutolewa kwenye media. Kuna confidentiality na pia wako watakaodai ni feki. Inabidi zitolewe na kuhakikiwa mahakamani kumaliza ubishi.

Hoja za Msigwa zinaakisi matendo specific ya kijinai ambayo Msigwa anadai ana ushahidi yametendwa na Mbowe. Hizo ni tuhuma za kijinai; sio siasa ya kuishia majukwaani. Katibu Mkuu si mtu sahihi kujibu hizo hoja, bali anaweza kuwa shahidi kuzithibitisha au kuzikanusha kwa vielelezo na nyaraka.
 
Seriously?!

Hili ni muhimu zaidi kuliko ya kutetea Taifa?
Mnahangaika na huyu mwenzenu yes mwenzenu badala ya kufungua kesi za kulikomboa Taifa, kuwarejesha waliotekwa kujua mstakabali wa Taifa mpo na kukimbizana na mjanja mwenzenu.


Tukisema hakuna upinzani bongo ni biashara za wachache hii ndio maana yake..
Mwenyekiti ajibu hoja za aliyemchafua sio hizi sarakasi

Mnajua kuwapanga wabongo duh!

Wanaofaidi keki ya Taifa ni wengi.
 
Huko alikojipeleka ndiyo kwenyewe sasa
 
Katibu Mkuu akijibu kwa maelezo tu mtadai haaminiki; atoe ushahidi wa nyaraka. Nyaraka za chama haziwezi kutolewa kwenye media. Kuna confidentiality na pia wako watakaodai ni feki. Inabidi zitolewe na kuhakikiwa mahakamani kumaliza ubishi.
.
Ushahidi wa nyaraka ndyo kitu muhimu, pia naamini mpaka Lissu kusema hayo anajua kinacho endelea ndani ya chama, kuna Madudu yanafanyika na yanachafua taswira ya chama kwa ujumla.
 
CCM wamemtupia Msigwa mjusi wa hii kesi ili zile hela walizmlipa kwenye biashara ya kumnunua ziishe kwenye kesi maana wanaona hakuna la maana aliloleta CCM toka Chadema kwani yote anayosema yalishasemwa na wote walionunuliwa kama bidhaa. Msigwa ameyatimba, hili ni la kwake mwenyewe.

Msigwa ni pandikizi la Kigogo fulani wa Upinzani ili amsaidie Kunusa siri za CCM ili kudhibiti watekaji na wauaji wanaopoteza wapinzani.

CCM wameanza kushtuka .
 
Yale yale kama ya kinana na Msigwa hadi akaomba poo... ndilo linaloenda kutokea... Msigwa fanya uungwana mapema kabla mambo hayajawa mambo... kuomba msamaha nayo ni heri, sijui kama unazo hizo billion tano, labda kama mpango ni kukufilisi hadi nyumba....
Ccm watamlipia ,apa ndo kuna mtego kama kweli ccm wanampenda msigwa au la, wasipo mlipia basi Msigwa ondoka ccm achana na siasa, ukiomba msamaha tu tiyari iyo ni pigo kwako na ccm waliokutuma,

Mara washa kijani ,sasa fuzi zimekata zote kila moja ipo hoi
 
Back
Top Bottom