Freeman Mbowe anatutukana watanzania kuwa sisi ni wajinga?

N
Mwamba Mbowe katoa neno mataga wote povu linatoka utazani mlevi wa gongo kutoka Buza

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Neno gani Hilo ndugu yangu unaloweza msifia, yaani matusi na dharau kwetu watanzania ndio neno, halafu anataka aungwe mkono na Nani? Watanzania Tupo na mh Rais wetu bega kwa bega
 
Mbowe yupo sahihi kwa sababu ujinga si tusi bali ni sifa/hulka! Ujinga unatokana na kutokujitambua!
Lakini hata kama neno ujinga lingekuwa tusi bado Mbowe angekuwa sahihi kabisa!
Ujinga upo! Na wajinga wapo!
Haiwezekani viongozi wa serikali waishi kifahari zaidi ya wafanyabiashara!
Haiwezekani viongozi wa serikali watumie nafasi zao kufanya uwekezaji mkubwa kama inavyotokea sasa.
Ni katika nchi ambayo wananchi ni wajinga hayo mambo ya kijinga yanaachwa yafanyike kijinga jinga!

Mbowe yupo sahihi sana!
Tatizo la Watanzania wengi ni ujinga!
Wanafikiri mtu akiwa kiongozi basi ni malaika au jini... wanamshitakia kwa MUNGU!
Ni waambie hivi... MUNGU hawezi kudeal na viongozi mliwachagua kijinga jinga!
 
Vitu alivyovifanya mh Rais wetu Ni vingi Sanaa ambavyo ukianza kuvielezea huwezi hata kuvimaliza
Eti WANANCHI wamejitoa kujenga nchi🤣 hii nchi inajengwa au inabimolewa📌
Kwenye hotuba nzima umeona kipande hiko Tu!!!
At least Mbowe kasema KERO zetu sio wewe na nyuzi zako za kumsifia kutwa mpaka zinapoteza maana
 
Vitu alivyovifanya mh Rais wetu Ni vingi Sanaa ambavyo ukianza kuvielezea huwezi hata kuvimaliza
Yes anafanya vitu vingi, kwenye kasoro lazima akosolewe kwa Sasa jambo lililopo kipaumbele kwenye midomo na akili za watanzania wengi ni Tozo ila sijawahi ona Uzi wako hata mmoja ukizungumzia hili zaidi ya kusifia utendaji wa rais.
 
Yes anafanya vitu vingi, kwenye kasoro lazima akosolewe kwa Sasa jambo lililopo kipaumbele kwenye midomo na akili za watanzania wengi ni Tozo ila sijawahi ona Uzi wako hata mmoja ukizungumzia hili zaidi ya kusifia utendaji wa rais.
Kwanza nakushukuru kwa kukiri kuwa mh Rais wetu anafanya na amefanya vitu vingi sana vizuri, pili Hilo suala la tozo nimelielezea Sana humu kuwa Ni wakati wetu watanzania kuona fahari katika kuijenga nchi yetu, ni wakati wakupita njia waliyopitia wenzetu walioendelea, Ni wakati wakujiinyima na kujibana kiasi katika vipato vyetu ili kuijenga nchi yetu,

Njia ya mafanikio Kama nchi siyo fupi Wala mkato, Tumuunge mkono Rais wetu mpendwa katika dhamira yake hii njema ya kuijenga nchi yetu
 
Yaani katika comments 27 zote zinakushambulia na kuungana na Mbowe kasoro comments 6 tu na katika hizo 6, nne ni za kwako mwenyewe mtoa mada

Jitafakari sana na wanaohusika watafakari mawazo ya watu walio wengi. Ni vyema kusoma alama za nyakati
 
Lucas si Bure nimenyanyua mikono🙌 endelea na kampeni
 
Yaani katika comments 27 zote zinakushambulia na kuungana na Mbowe kasoro comments 6 tu na katika hizo 6, nne ni za kwako mwenyewe mtoa mada

Jitafakari sana na wanaohisika watafakari mawazo ya watu walio wengi. Ni vyema kusoma alama za nyakati
Jambo jema au hoja ya ukweli haiangalii na Wala haipimwi Kama unavyotaka kutuaminisha,Nenda kasome habari za Galileo ndio utaelewa vyema hiki nachokueleza hapa
 
Hii nchi ina wajinga wengi sana!

Sasa hapa ndiyo umeandika nini? Maelezo marefu!! Pointi hakuna.
 
Ukishamaliza kutumika tutakukuta jalalani
 
Ila sasa kuna wajinga ambao pamoja na ujinga wao bado wanajiona wapo sawa hata wakifanyiwa mambo ya kijinga na wajinga!
Na kwa sababu ya ujinga wao hawana uwezo wa kuelewa chochote wenye akili wakitoa hoja za kutafakarisha!
Mfano mzuri hili jambo la kulazimisha tozo!
Akili ya kawaida ni dalili za wizi na ubadhirifu!
Lakini wengine hawaoni hilo hivi ninavyoandika wapo bize kuandaa maandamano matamko kwa ajili ya kuwapongeza watozaji!!

Aibu sana!
 
Kwamba Kujenga nchi yetu wenyewe Ni ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…