Freeman Mbowe apendekezwa mwanasiasa bora wa Upinzani

Freeman Mbowe apendekezwa mwanasiasa bora wa Upinzani

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Ikiwa ni takribani robo karne tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini watu kadhaa wasomi na wanasiasa wamependekeza iwepo nishani maalum kwa mwanasiasa bora wa upinzani nchini.

Kati ya watu maarufu waliozungumza katika kipindi maalum cha VOA kuhusu upinzani Tanzania ni Professor Gaudence Mpangala na mwasisi wa mageuzi Dr Emmanuel Makaidi.

Aliyeonekana kung'ara katika wanasiasa wa upinzani ni Mwanasiasa Tajiri mwenye ukwasi mkubwa Freeman Aikael Mbowe.

Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa amependekezwa kutokana na sababu kubwa mbili;

Moja ni Kwa jinsi alivyokiongoza chama chake cha Chadema kutoka chama kidogo kabisa cha upinzani kuwa chama kikuu cha upinzani kinachokaribia kabisa kupokonya mamlaka ya dola.

Pili ni kutokana na uvumilivu wake.Imedaiwa Freeman Mbowe ndiye mwanasiasa mvumilivu zaidi Tanzania.Kiongozi huyu amedaiwa kupitia vipindi vigumu sana ndani ya chama chake kwa baadhi ya viongozi wake kurubuniwa na watawala na kuanzisha makundi ya uasi.Imeelezwa Freeman Mbowe mara zote amekuwa mvumilivu na kuwapa nafasi ya kujirudi maadui zake.

Tukio lililoelezwa la karibuni zaidi ni Uasi uliiingozwa na wanasiasa watatu ndani ya chama chake Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.Waasi hawa walipanga kumpora mamlaka kwa njia ya mapinduzi na vijana wao walimtukana kila aina ya matusi Freeman Mbowe kupitia mitandao ya kijamii.

Hata hivyo ingawa mpango wao uligundulika mapema bado Freeman Mbowe aliwapa nafasi ya kujirudi na kuomba radhi.Ingawa walikataa kuomba radhi na kusonga mbele na hatua yao mpaka kamati kuu ilipowafukuzilia mbali.

Kuthibitisha uvumilivu wa Freeman Mbowe wanasiasa hao waliofukuzwa walikimbilia ACT na ikiwa hata haijapita miezi sita tayari wamefukuzwa kwa aibu kubwa kutoka ACT kwa madai yale yale waliyofukuzwa nayo Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Huwa na mponda sana Mbowe humu ili kwa hoja zako kidogo naanza kumuelewa ila sasa upole wake usiwe na mahusiano na kuhongwa na watawala
 
Mbowe akiwa rais wa nchi hii naihama,labda lipumba au slaa au lissu ndani ya ukawa ila sio mbowe.

una mawazo mgando kama akili yako imeandikwa wapi mbowe anataka kugombea uraisi????
 
Mbowe ni mroho ws madaraka ukiutamani uenyekiti anakusukia zengwe ufukuzwe au anaku Chacha Wangwe.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Umeanza vzr lkn mwishoni mwa hoja yako ni km una chuki na hao jamaa hivyo mwandishi nawe umekosa uvumilivu ! Namkubali sn Mbowe long live kamanda
 
mbowe ana karama ya uongozi wa kuzaliwa
 
Mbowe ni kiongozi mwenye ushawish sana, ata asimamapo bungen, wapunge wote hukaa kimia na kuanza kumsikiliza.
 
Back
Top Bottom