Mh Freeman Mbowe amekuwa ni kiungo muhimu kati ya siasa za upinzani na chama tawala ikiwemo serikali.
Ni mh Mbowe aliyemshawishi Dr Slaa agombee urais mwaka 2010 na kuachana na ubunge wa Karatu huku akijua kabisa hawezi kushinda mbele ya Rais Kikwete aliyekuwa anatetea kiti chake kwa muhula wa pili.
Na ni mh Mbowe huyu huyu aliyebadili gia angani na kumleta mzee Lowassa wa CCM wakati wana UKAWA wameshakubaliana Dr Slaa awe ndio mgombea wa vyama shirika vya Chadema, Cuf, Nccr mageuzi na NLD
Ni Mbowe aliyeongoza kikao cha kamati kuu kilichopelekea Chadema kususia uchaguzi wa serikali za mitaa na kusababisha CCM ipate ushindi " halali" wa kishindo wa 99.9% na leo ameunga mkono juhudi za kuimarisha demokrasia nchini.
Ninampongeza Freeman Mbowe kwa sababu kitendo chake cha kubadili gia angani ndicho kilichoisambaratisha Cuf na Nccr na kuiinua Chadema, maana licha ya kumpoteza Dr Slaa bado Chadema iliibuka na idadi ya kutosha ya wabunge huku Julius Mtatiro wa Cuf akichinjiwa baharini kiaina na Nccr kuambulia mbunge mmoja kama taa ya treni.
Freeman Mbowe ni akili kubwa vyuo vikuu vimtafiti na kumfikiria heshima ya Ph.D
Maendeleo hayana vyama!