Pre GE2025 Freeman Mbowe ashauriwa akichaguliwa amteue Tundu Lissu kwenye uongozi

Pre GE2025 Freeman Mbowe ashauriwa akichaguliwa amteue Tundu Lissu kwenye uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe akishachaguliwa tena hakuna hiyo kitu unasema. Alishaamua kwenda anavyotaka kuamini hilo angalia makamu wake wenje. Hapo kutakua na jipya lipi?
Mbowe anaongoza kwa vikao hafanyi maamuzi kutoka kichwani tu
 
Molemo acha kutumika. Wenzako wengi walikuja na gia kama hii ya kwako lkn wametulizwa.

Lisu hakamatiki.
Molemo Media haiwezi kutumika lakini pia haitaogopa kusema ukweli hata kama itakera baadhi ya watu
 
Mbowe anaongoza kwa vikao hafanyi maamuzi kutoka kichwani tu
Kwa maelezo ya Lissu, wajumbe wa kamati kuu wote walimpinga kuhusu maridhiano lakini bado aliwakatalia akaendelea nayo. Akaenda kutoa na tuzo bila kamati kuu kushirkishwa

Mbowe hawezi kufanya maamuzi kwa vikao. Anaamua vile anavyotaka
 
Mbowe anaongoza kwa vikao hafanyi maamuzi kutoka kichwani tu
Mchagueni Mbowe halafu mje kwa raia mtuambie habari ya katiba mpya, ukomo wa madaraka, kupinga Rais Samia kugombea au kujiongezea muda (akifanya hivyo) na mambo mengine ya aina hiyo muone mtavyozomewa na wananchi.
 
Ni takriban wiki 3 zimesalia pekee kushuhudia mpambano wa kukata na shoka kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu kukalia kiti cha Chama kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA.

Kumekuwa na mpambano mkali kwenye mitandao ya kijamii hasa nani anafaa kuchaguliwa kuongoza chama hicho katika uchaguzi wa Januari 21

Katika uchunguzi uliofanywa na Molemo Media Tundu Lissu anaonekana kuungwa mkono kwa wingi na makundi ya watu yaliyo nje ya chama hicho kama vile wanaharakati na Watanzania waishio nje ya nchi wanaojulikana kama Diasspora.

Freeman Mbowe anayetetea kiti chake anaonekana kuungwa mkono na wapiga kura wengi ndani ya chama hicho.Mpaka sasa ana uhakika wa kupata walau robo tatu ya kura zote zitakazopigwa kwenye mkutano mkuu.

Uchunguzi wa Molemo Media umegundua Freeman Mbowe anaweza kuzoa kura zote za Unguja na Pemba kutokana na kile wajumbe wanachodai matamshi tata ya Tundu Lissu kuhusu Muungano na kuonekana hapendelei sana upande wa Zanzibar.

Pia uchunguzi unaonyesha Freeman Mbowe anaungwa mkono na idadi kubwa ya wajumbe katika Kanda za Nyasa, Kusini, Kaskazini, Magharibi, Victoria na Kanda ya Kati.

Tundu Lissu anaonekana amejikita zaidi Kanda ya Serengeti na kwa uchache Kanda ya Pwani.

Uchunguzi zaidi uliyo huru wa Molemo Media unaonyesha wajumbe wengi wa mkutano mkuu wanaamini kumpigia kura Freeman Mbowe ni kukibakisha chama katika mikono salama na kumchagua Tundu Lissu ni kukiweka rehani kwa wanaharakati na watu waishio nje ya nchi.

Katika mahojiano yasiyo rasmi yaliyofanywa na Molemo Media pamoja na watu maarufu ndani ya Chadema, wamemshauri Freeman Mbowe endapo kama atachaguliwa kuwa Mwenyekiti basi amteue Tundu Lissu kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Wachunguzi wa mambo wanadai kumteua Tundu Lissu kuwa mjumbe wa Kamati Kuu kutasaidia kuimarisha umoja ndani ya chama hicho na pia kutaendelea kuwavuta wanaharakati waendelee kukiunga mkono chama hicho ambao wamekuwa wakikishabikia miaka mingi.

Yote kwa yote kilichobaki ni siku tu ya kupiga kura kwani inaonekana tayari idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu wameshachagua upande wa kuunga mkono.
Acha kuporosha labda ni kwa vile hamkusoma hesabu, ukiona poll. Ya lisu ana 84% na mbowe ana 16%

Kwenye statistical research hiyo ni sample space ambayo automatically inakuonyesha mshindi

logically waliopiga kura jf ni pamoja ja na wajumbe wa mkutano mkuu

Hiyo poll result ni pro rata na matokeo yatayotoka
 
Naona mleta mada umetumwa kuja kupima UPEPO na hicho kiutafiti chako uchwara
 
sampuli ya wahojiwa ilikuwaje? Mbona habari nusu nusu? Walihojiwa wangapi kutoka hizo kanda tajwa? ni wangapi walisema watamsapoti Mbowe na wangapi walisema lisu. Hivyo hivyo ni kati wajumbe wangapi waliowakataa wote. Wachunguzi wa mambo, ni akina nani hao? hawana majina, Identity au ni anonymous?
Hata mimi nilitoka Kyela majuzi hakika huko kote ni Mbowe,hawajui habari ya Lissu kabisa.

Ukitazama uungwaji mkono huku mitandaoni utafikiri Lissu atachukua uongozi asubuhi.

Hali ni tofauti kabisa huku site.

Ngongo kwasasa Idodomya.
 
sampuli ya wahojiwa ilikuwaje? Mbona habari nusu nusu? Walihojiwa wangapi kutoka hizo kanda tajwa? ni wangapi walisema watamsapoti Mbowe na wangapi walisema lisu. Hivyo hivyo ni kati wajumbe wangapi waliowakataa wote. Wachunguzi wa mambo, ni akina nani hao? hawana majina, Identity au ni anonymous?
hata samlping from silent people inatosha ku justfy matokeo .
Lisu yuko kimtandao na wanaharakati na sii wapiga kura.
 
Wacha wamchague Mbowe halafu watanzania waachane na CHADEMA kisha tuone 2025 watapata nini.
Kama wewe upo CDM kwasababu ya Lissu ni bora ukafungasha virago asubuhi.

Fikiria mtu wa kawaida anahoji siwezi kumchagua mtu kila mara yuko Belgium.

Kwanini Meneja wa kampeni wa Lissu ni Mch Msigwa?.Haya ni baadhi ya maswali niliyokumbana nayo vijijini.

Wananchi wengi wa kawaida ikiwemo wapenzi na wanachama wanahoji ni kwanini Lissu hana shukrani kama si Mbowe leo angeshasahaulika.
 
Hao wajumbe mkutano mkuu watakuwa ni wajinga wakiendelea kumchagua tena Mbowe baada ya miaka 21!.
Wakifanya hivyo baada ya uchaguzi tarehe 22 jan wanapaswa kupelekwa milembe hosp!!.
 
Hata mimi nilitoka Kyela majuzi hakika huko kote ni Mbowe,hawajui habari ya Lissu kabisa.

Ukitazama uungwaji mkono huku mitandaoni utafikiri Lissu atachukua uongozi asubuhi.

Hali ni tofauti kabisa huku site.

Ngongo kwasasa Idodomya.
uko kyela ipi mkuu mbona huku wote ni lissu au uko kyela ya Malawi.
Mbeya iliyojaa wanaharakati refer mwambukusi ndiyo wamchague mbowe?
 
Lissu amejiondoa mwenyewe kwenye uongozi CDM, ningekuwa Mbowe nisingempa hata ujumbe wa CDM kwenye shina.
Kwa taarifa yako muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wz cdm umepita.
 
Mnamfanya Lissu kaonekana mtoto sana... motives zake zinaonesha wazi hakutaka uchaguzi bali kuachiwa cheo kwenye sinia.... too low for him....
Lissu hajawahi kudai point za bure uwanjani acha kumlisha maneno!.
Ila sie wapenda mabadiliko ndio tunamshangaa huyo mbowe baada ya miaka 21 madarakani ana jambo gani jipya tena kwa maendeleo ya chama??
Busaratu ilitakiwa kumuongoza akae pembeni apishe wengine wagombee nafasi hiyo.

Hv pata picha baada ya miaka yote hiyo halafu itokee amebwagwa kwenye uchaguzi tarehe 21 jan si fedheha kwake hiyo?!.
Yaani atakiachia kiti kwa aibu tofauti angeamua kung'atuka mwenyewe.

Binafsi, nitawaona wajumbe mkutano mkuu ni wapumbavu wakimpigia kura mbowe hata kwa 35% achilia mbali kushinda uchaguzi kabisa!!.
 
Back
Top Bottom