Freeman Mbowe atangaza kufanya Makongamano ya Katiba mpya nchi nzima, la Mwanza kufanyika wiki hii

Freeman Mbowe atangaza kufanya Makongamano ya Katiba mpya nchi nzima, la Mwanza kufanyika wiki hii

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mwamba mwenyewe Freeman Mbowe, Mtemi Isike ama Aboubakar Mbowe kama anavyofahamika huko Zanzibar, akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, ametangaza kuendelea kufanyika Makongamano ya ndani na ya amani ya Katiba mpya nchi nzima, huku lile la Mwanza lililohujumiwa likipangwa kukamilishwa wiki hii.

Akiongea kwa kujiamini na kwa msisitizo mkubwa huku akiwa kavaa kofia maarufu ya ukombozi, Laingwanan Mbowe kama anavyofahamika huko kwa Wamasai, amesema kwamba ikiwa kufanya makongamano ya ndani ya Kudai Katiba mpya ni uvunjifu wa katiba basi waanze kumkamata yeye leo hii.

Hatutaondoka_hapa_Mwanza_na_wiki_hii_tufanya_kongamano_kubwa_hapa_Mwanza,_sisi_viongozi_hatuta...jpg
 
Kama kufuata sheria siku hizi ni uvunjifu wa amani au vichokochoko ndio tujue, na inasikitisha zaidi pale polisi wanaotakiwa kusimamia sheria za nchi wao ndio wanatumika kuwakamata wanaotii sheria, lazima tujinasue kwenye huu mkwamo ili kama taifa tusogee mbele kidemokrasia.
 
Mbowe is the best, anajua wakati gani atumie hekima hata kama wengi watamuona muoga, na wakati gani atumie nguvu, huyu chairman namuelewa sana.

Halafu utawasikia vichaa fulani wanasema Chadema waache uanaharakati, wakati wao ndio wanawafanya Chadema waonekane wanaharakati kwa kuwalazimisha Chadema kupigania haki zao kisheria.
 
CCM hii hasara kweli kweli, yaani inaogopa hadi mikutano ya ndani aisee!
 
Mimi nilifikiri anasema kesho maandamano.

Yale yale, unasema halafu unasikilizia UPEPO 🤣
 
Kuruhusu mikutano ya kisiasa na katiba mpya ni kipimo kwangu kama mama anaupiga mwingi
Baba kashatishwa tayari, CCM hawana maana yoyote - wanamwambia ati kwa sasa ilani aliyorithi ya 2020 - 2025 haina kifungu chochote kilichoandikwa katiba mpya.
 
Back
Top Bottom